Mabasi ya Majinjah ni mabovu, msithubutu

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,108
Reaction score
1,132

Habarini,

Leo ndugu yangu kaingia cha kike baada ya kuchelewa basi la Newforce kutoka Dar kwenda Sumbawanga na kupanda basi la Majinjah special.

Alikata tiketi ya Newforce siku 2 kabla leo asubuhi akafika stand ya Magufuli saa 10:45alfajiri na kukuta Newforce imeshatoka.

Alipandishwa Newforce ya Songea ili kuiwahi Newforce ya Sumbawanga lakini hadi anafika Chalinze hakuipata hivyo akaamua kushuka Chalinze ili atafute usafiri mwingine hata wa kuishia Tunduma ili kesho aunge Sumbawanga ndipo akaambiwa Majinjah ya Sumbawanga haijapita hivyo apande hiyo akapanda lakini hadi muda huu hawajafika Mafinga linaharibika kila baada ya hatua chache.

Angalizo: Majinjah haifai kwa safari za Sumbawanga kwa sasa bali Newforce ambapo inakubidi ufike stand ya Magufuli Mbezi saa 10:00 alfajili.

Asante.
 
Lazima utakua wewe tu maana unaelezea kwa masikitiko
 
Hivi kweli hata kwa muonekano unaanzaje kupanda majinja? Yale ni masufuria au gonga nyundo

Over
 
Aaaahhaaahaaaaaaaa
Jinjah boy anawaswaga wasukuma Dar-Mpanda utafikiri mbuzi zizini
Alishawahi kutufikisha mpanda saa 10 alfajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…