HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 1,108
- 1,132
Habarini,
Leo ndugu yangu kaingia cha kike baada ya kuchelewa basi la Newforce kutoka Dar kwenda Sumbawanga na kupanda basi la Majinjah special.
Alikata tiketi ya Newforce siku 2 kabla leo asubuhi akafika stand ya Magufuli saa 10:45alfajiri na kukuta Newforce imeshatoka.
Alipandishwa Newforce ya Songea ili kuiwahi Newforce ya Sumbawanga lakini hadi anafika Chalinze hakuipata hivyo akaamua kushuka Chalinze ili atafute usafiri mwingine hata wa kuishia Tunduma ili kesho aunge Sumbawanga ndipo akaambiwa Majinjah ya Sumbawanga haijapita hivyo apande hiyo akapanda lakini hadi muda huu hawajafika Mafinga linaharibika kila baada ya hatua chache.
Angalizo: Majinjah haifai kwa safari za Sumbawanga kwa sasa bali Newforce ambapo inakubidi ufike stand ya Magufuli Mbezi saa 10:00 alfajili.
Asante.