Kuna na haya yenye mende pia. Kuna moja lina jina kubwa tu tena wanaliita semi luxury, linatokea na kwenda nchi ya jirani ambako hustler mmoja ameukwaa urais juzijuzi tu hapa. Seats zake ni kubwa, yaani ni 2 kwa moja. Cha ajabu sasa Giza likiingia, yaani mnapishana na mende tu huko ndani.
Jingine ni la kampuni inayobeba jina mojawapo la mikoa ya kaskazini, linafanya safari zake kati ya jiji hilo lililoko kaskazini na jiji kubwa la nyanda za juu kusini. Nalo lina mende haswaa.
Nadhani wangejitahidi mara moja moja kufanya fumigation. Hao viumbe wanashusha sana hadhi ya gari.