Kinachotrendi mitandaoni kwa sasa ni Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Line kupewa tenda ya kusafirisha staff wakiwemo wanasoka kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 ambayo yanafanyika mwaka huu 2025.
Kwa mujibu wa taarifa, tenda hiyo amepata Mkenya ambaye alipewa uamuzi wa kukagua mabasi yote katika nchi zinazoandaa mashindano hayo (Tanzania, Kenya, Uganda) ili kupata kampuni ambayo ina mabasi bora zaidi.
Imeelezwa kuwa, Mkenya huyo baada ya kukagua mabasi ya Tanzania na Kenya, akayaona mabasi ya Shabiby Line yanafuzu vigezo vya ubora unaohitajika.
Mabasi hayo yameshabandikwa stika inayosoma kuhusu mashindano hayo ya Chan mwaka huu (rangi na logo) yakitumika Tanzania na Kenya.
Mmoja wa wafanyakazi wa mabasi hayo amesema kuwa, mabasi yote ya Shabiby Line ambayo yamepewa tenda ya shughuli hiyo ni mapya kabisa yakiwa na sifa zote ya mabasi ya kisasa nchini Tanzania na Afrika Mashariki yote.
"Mabasi yote yana vyoo ndani. Milango miwili ya kupanda na kushuka abiria. Intaneti ya bure yenye kasi zaidi, viti vyenye ngozi inayokidhi sifa ya viti vya ndege za abiria," alisema mfanyakazi huyo wa mabasi hayo.
Aliendelea kusema kuwa, mabasi ya Shabiby yamepata tenda hiyo kwa vile yote ni mapya yakiwa na namba za usajili wa EM...na kuendelea.