Kipindi ambacho watoto wanatoka shuleni wakiwa katika mabasi yao kuelekea nyumbani tunawatengenezea mfumo wa kuwaweka bize kuangalia katuni au sinema zinazowafurahisha wakati huo zinawapa maadili ya msingi kabisa katika Maisha yao, pia kuwaonesha madhara ya baadhi ya vitendo ambavyo vinaleta mmomonyoko wa maadili yetu ya kitanzania mfano: kushiriki vitendo Vyovyote vya utovu wa nidhamu pindi wawepo shuleni nyumbani au kwenye mkusanyiko wa watu mfano kanisani, msikitini au popote kwenye mkusanyiko wa watu wengi, mapenzi ya Jinsia moja, namna ya uvaaji wa mavazi yao, kuongea.. N.k.
Lakini pia kuwawekea katuni zinazohamasisha uwajibikaji, uzalendo, umoja na mshikamano. Mtazamo huu ni Kama jinsi tunavyosafiri kwenye mabasi tunapendezwa na video nzuri zinazotufanya kuwa Makini kuangalia Licha ya uchovu tu tunaokuwa Nao. tutatengeneza maudhui ya katuni zenye kulenga kutimiza lengo moja moja, mfano tutaanza na katuni au video zenye kuonesha heshima kwa wakubwa na madhara yake endapo Mtoto hataonesha heshima. Lakini pia katuni au video hizi zitakuwa fupi fupi na zenye maudhui ya mvuto wa Hali ya juu kanakwamba zitakuwa na uwezo wa kukamata hisia za watoto za namna zote iwe huzuni hadi walie au furaha hadi wacheke lengo nikufukisha ujumbe na kuwafanya wabadilike kwa kufikiwa na ujumbe madhubuti.
Kutokana na hili Natumaini watoto wana muda mwingi sana katika mabasi yao pindi wanapotoka shuleni kuelekea majumbani kwao, hivyo Tutumie muda huo kuwaburudisha au kuwasikitisha kupitia katuni au video husika hivyo tutakuwa tumewapa Elimu kupitia katuni au video Mfano kuna katuni au video zinazotumiwa katika vipindi vya televisheni maalumu kwa kuwasaidia watoto kujifunza kuhesabu, kuandika, na kusoma, katuni au video hizi zimefanikiwa kwa kiasi Kikubwa Sana kufikisha ujumbe tarajiwa kwa watoto na kuwafanya wawe na amu ya kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu. Lakini pia katika vitabu mbalimbali picha za katuni na zinazofanana na katuni hutumika kuhamasisha na kulahisisha katika ujifunzaji kwa watoto.
Hii pia inakuwa mbadala wa watoto kupiga kelele kwenye mabasi wakati wa kurudi nyumbanI Hii husaidia kuepukana kumchanganya dereva na Wenda kasababisha ajali za kizembe. Lakini pia kutokana na watoto kuangalia katuni kipindi hicho cha kurudi nyumbani katika basi hii itawaepusha kusikiliza au kuangalia vitu ambavyo haviwasaidii katika Maisha yao ukilinganisha na umri wao.
Pia utafiti unaonesha kuwa katika uvunjikaji wa Maadili, eneo linaloathiriwa zaidi ni watoto wa mjini yaani watoto wa kishua Kwani Mara nyingi wazazi wao hawazingatii kuwasaidia watoto wao kukua kimaadili Mara nyingi huwasaidia tu kufanya kazi zao wanazoachiwa shuleni na waalimu wao yaani homework.
Lakini pia watoto hao Mda mwingi Wanashinda na dada wa kazi Kwa hiyo suala la kujifunza maadili linakuwa gumu sana au wazazi wanakuwa wamesafili kikazi hivyo hawana Mda wa kukaa na watoto wao au muda mwingine hurudi nyumbani mda ukiwa umeenda hivyo hawapati mda wa kuzungumza na watoto wao pia kujua mienendo ya kitabia ya watoto wao na baadae mambo yanakuja kugundulika yameearibika mda ukiwa umeenda waswahili wanasema samaki mkunje ingali mbichi .
Watoto wa kitajiri kama waswahili wasemavyo watoto Wakishua wana uhuru Sana wa kufanya chochote Kwani wazazi wao wanakuwa na rasilimali hivyo wana uhuru wa kufanya Jambo lolote wanalotaka hata kujali kama linachangia katika mmomonyoko wa Maadili hivyo muda huo wanapokuwa katika mabasi yao Tutumie muda huo kuwaelimisha kupitia kuangalia katuni zinazowafunza kujitambua na mwisho wa siku watakuwa na maadili mazuri na hata kisomo chao kitakuwa na tija katika Jamii. Hivyo natumaini Jambo hili tukilifanyia kazi .
Pia tumelenga watoto wanaotumia mabasi ya shule kwani watoto hao ndio wanaoongoza kwa mmomonyoko wa maadili kwani wengi hutumia simu janja ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa Maadili mfano wengi hujifunzia huko baadhi ya tabia kuanzia swala la mavazi, no mitindo mingine ya tabia isiyofaa katika jamii yetu ya kitanzania.. Zikiwemo picha za ngono.... yaani ponography.
Najua pia sio watoto wadogo tu hutumia mabasi ya shule lakini hata pia wanafunzi wakubwa hasa wanafunzi wa secondary Nao pia tunaweza kuwatengenezea programu yao yenye mtazamo Kama huo ili pia kuwaweka Sawa kimaadili ya kitanzania.
Basi kwa sababu wazo hili linaendana na miundombinu ya kuweka vifaa vya kutazamia kwenye magari basi huu utakuwa mpango utakaowahusisha wamiliki wa hayo mabasi ya wanafunzi lakini pia itawahusisha wamiliki wa mashule ambao watakubaliana na huu mpango au mradi katika wazo na kuwa Kitendo hivyo natumaini hata pia wadau wa Maadili Elimu pamoja na wizara ya elimu inayojishughulisha pamoja na tawala za mikoa na serikali za mitaa yaani TAMISEMI pia tunaweza kuwahusisha katika kukamilisha swala hili.
Ni tumaini langu suala hili litafanikiwa kubadili kizazi chetu kwa hatua moja au nyingine, kwa pamoja tuungane kusaidia kizazi hiki Kuwa na maadili mema kupitia Digitali kama ilivyo kizazi hiki ni cha Digitali.
NASHUKURU SANA KWA KUPATA NAFASI HII KUWASHIRIKISHA WAZO LANGU. ASANTE

Upvote
0