Mkanganyiko kukanganya
JF-Expert Member
- Jun 26, 2022
- 1,204
- 5,053
Haya mabasi yamegeuka kuwa mabanda ya machinjio na kuwapa abiria ulemavu wa maisha.
Hawa madereva ni sikio la kufa daima na sio mambo ya kusadikika, wenyewe tunayaona huko road wanavyoyafyatua mabasi. Mfano:
~ Ukiwa na kagari kadogo utaletewa basi hapo nyuma honi zote, taa kali, kama muoga utapagawa presha au uingie mtaroni.
~ Wao wanajua ku overtake popote ni haki yao, kama unakuja kwa mbele hawajali hasa ukiwa na kagari kadogo, itabidi kuingia porini kuepuka kifo.
Huko maporini mwendo wao ni roho kiganjani, dereva ni mwendo wa kusimamia tu, kwao ni marufuku kubaki nyuma ya gari lingine hasa aone bus mwenzie mbele; yaani hatameza mate mpaka ampite 😂😂.
Mabasi ya wilayani utakuta juu limebeba kilemba cha mizigo mizito, ndani abiria, ilihali barabara ni mbovu na ni milima, bado gali linapigwa mwendo hatari.
IGP na Rais wameshawaonya mara kadhaa ila wanaviburi na dharau na mara nyingi ajali ikitokea madereva hawafi, wanasepa😂😂.
Ingefaa ifike mahala tupate wanaume wachache kutoka JWTZ waratibu zoezi hili angalau kwa miezi sita tu, then tuone matokeo.