"Mabeberu" Marekani waanza mbinyo kwa Tanzania. Washawishi Serikali yao na Jumuiya ya Kimataifa kuanza vikwazo na kukata misaada

Kama unasema siyo lazima Lissu au Mbowe awe rais mbona Magufuli na wenzake wamelazimisha kuwa viongozi hata kama wamekataliwa na wananchi ?

Au hii " siyo lazima" yako ni kwajili ya Lissu na wapinzani wengine ?
Mkuu umenikusudia mie au umekosea?maana mie sijazungumza habari za Lissu.
 
Pamoja na maisha mazuri ya wa Libya kulikuwa na mbinyo sana wa kisiasa( binadamu unaweza kumpa kila kitu ila ukimnyima uhuru wa kisiasa umefeli human beings are political animals ).

Tukumbuke jamii ya watu wa Benghazi nchini Libya ambako machafuko yalianzia walikuwa wametengwa na kubaguliwa katika utawala wa Libya lakini pia Gaddafi wakati wa kuingia madarakani alimuua mfalme ambaye alikuwa mzaliwa wa Benghazi hivyo unaweza kuona sababu za machafuko yale
 

Yakwao tu huku yamewashinda.
Wapumbavu ninyi mnaowashabikia
 
Ndio maana nikasema kama utawala wa Saudia unaongoza vizuri tu na watu wanaishi vizuri sasa hao wakosoaji wanakosoa nini hadi wengine wanauliwa?
Hilo jambo Lina utata sana
Ila ukimuuliza RAIA wa kawaida atashangaa sana
 
Wewe utakuwa ni "millenial".
Kwa tuliokuwepo timamu kipindi cha miaka ya 1970s, tunatambua uwezo wa Tanzania ya kipindi hicho na viongozi wake,pamoja na "Westerners" wa kipindi hicho. Leo hii,kwa sisi tuliokuwepo kipindi hicho,tena tukiwa na akili timamu,hatuwezi kuibeza Marekani, "western", wala hao "juche".
Kuwavimbia US hakumaanishi wao wapo juu ya US.
Laiti kama ungekuwa na akili ya kawaida ya kujua gharama ambazo US analipa kwa tukio la Hiroshima,ungejua kuwa US ana kila sababu ya kuwa kiranja wa dunia.
Kwa kuwa uwezo wako ni kucheza ngoma unayopigiwa,yaani u msukule, sitakuwekea ushahidi wa jinsi US anavyoitazama Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atashangaa nini?
RAIA lazima ashangae....
Kama wewe ni RAIA halali wa nchi hio kuna kitu gani hupati mpaka kufikia kukosoa utawala
Kama kuna huduma Huna hapo sawa lakini kila kitu Kipo..... nchi haikubagui unaishi kama sultan bado tu unasema vibaya kuhusu utawala?
Anyways watu kama hao wapo kwenye jamii
Hata mtoto ambaye anafanyiwa kila kitu na wazazi wake baadhi hawaridhiki
 
Awamu hii ya Zimbabwe tutayaona kwa macho tujiandae kuishi kiuni kama Kwa Kim
 
😂 😂 😂 😂 Kwanza nimeanza na kucheka yaani Tzn huwa inaicheka Kenya kumbe inapokea misaada ya misosi licha ya kuwa na ardhi ya kutosha na mvua tele? hata hiyo wafyeke sioni maana
 
Wazungu wote hasa hawa mabalozi na maafisa wao wanajua mno kiswahili, maana wengi wao kipindi cha ujana walikuja kuishi Tanzania kama vijana wa kujitolea kwa mataifa yao kuisaidia Tanzania katika sekta za Kilimo, Elimu na Afya.

Sasa kitendo cha wao leo kuitwa MABEBERU aise kitakuwa kinawauma sana... hili neno litakuja kuighalimu Tanzania saana tu.
 
Ulitakiwa sasa ujue wanacholalamika ni nini?maana inawezekana kukawa na mambo yanafanyika ambayo si sawa na ndio maana kuna wakosoaji. Sasa wewe usiangalie tu kuwa wanapewa kila kitu.
 
Hakuna mfadhili wa demokrasia duniani acha ujinga yaani ntu atoke ulaya aje kukusaidia wewe kupata haki yako kwako?
Huelewi how it works,unawekewa vikwazo,mbinyo unakuwa mkali mpaka wananchi wanafeel hali ngumu ya maisha!Fikiri vitu kama madawa na vifaa tiba vinakuwa ghali au havipatikani!Wananchi lazima wataumia hivyo kuilaumu serikali yao!Kwa mazingira hayo,serikali itajirudi maana inajua wananchi hawawezi ichagua serikali inayowaletea maumivu!Baada ya hapo serikali itachukua hatua kurekebisha,na hilo ndio lengo la vikwazo!
 
Dona kantre huna hata kiwanda Cha kutengeneza pini.
Kifuatacho ni kupunguza kazi madaktari, manesi na watu wa maabara na kuajiri waganga was kienyeji, wachawi, wabashiri na wapiga ramli.

View attachment 1626014
Kitu mbadala kawaida huwa hakina uwezo wa, na wala huwa hakikusudiwi kwa namna yoyote ile, kupunguza ufanisi wa kile kilichopo sasa ambacho mbadala huo umekusudiwa au kuwekwa kwa ajili yake. Mbadala huwa unakuwepo kwa ajili ya kusaidiua tu kuongeza kasi pamoja na ufanisi wa kazi iliyokuwepo awali na si vinginevyto
 
Bwaka = bweka
Hiki kiswahili si lugha rahisi
 
Ulitakiwa sasa ujue wanacholalamika ni nini?maana inawezekana kukawa na mambo yanafanyika ambayo si sawa na ndio maana kuna wakosoaji. Sasa wewe usiangalie tu kuwa wanapewa kila kitu.
Mimi nimepata bahati ya kuishi huko na nimezungumza na RAIA wengi wa huko
Hali Halisi ni wale jamaa wanaishi maisha kama ya watoto We matajiri wakubwa wa tanzania yetu
Kama kuna wakosoaji wapo wapo tu
Amini nakwambia jamaa wamamaisha mazuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…