Mabeberu wanaendelea kutuhujumu: Kwanini hawataki kubadilisha data za COVID19 zinazohusu nchi yetu?

Mabeberu wanaendelea kutuhujumu: Kwanini hawataki kubadilisha data za COVID19 zinazohusu nchi yetu?

Huyu bwana hataki hata kuisikia korona japo korona haiwezi ondoka kwa yeye kutotaka kuisikia.Nahisi Siku moja ataamrisha mtu akipatikana na korona apigwe shaba.Mtu amevaa barakoa anajikinga wewe unamkosoa
 
Barakoa inazuia hewa safi oksijeni ,seli (kingamwili) kufa kwa kukosa hewa.mkuu hujasoma biolojia munakwamaa sana mabalakoa yenu, tafute biashara ingine ya kufanya.
 
Baada ya usingizi kukata nikaamua kuingia kwenye mtandao maarufu wa
Coronavirus Update (Live): 6,844,705 Cases and 398,141 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer unaotoa taarifa za corona kwa kila nchi. Nimestaajabu kuona wanasema Tanzania bado tuna wagonjwa 305. Nachojua ni kuwa mtandao huu huwa unabadirisha taarifa kila wanaposikia serikali ya nchi husika imetoa update. Na kama nakumbuka vizuri taarifa ya mwisho ilisema wagonjwa wamebaki 3, sasa ni kwanini hadi leo hawajabadirisha? Mbona nchi nyingine wanazifanyia update kila siku?

Je, wamegoma kutuamini, wameamua kutususa, hawatuelewi au wanatuonea wivu wanajisikia vibaya kuandika Tanzania is free from corona virus?
View attachment 1469840
Hivi kuna taarifa rasmi ya Wizara inayoonesha sasa hiv tuna wagonjwa wanne? Au ni zile porojo za kwenye majukwaa Na madhabahuni ya viongozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameona hatueleweki ndio maana wameamua kutoweka detail zetu. Tunasema corona kwetu imeisha lakini tunataka pesa za hao hao mabeberu kwa ajili yakupambana na hili gonjwa. Corona kwetu imeisha lakini mpakani namanga na holili hapatoshi. Huku tunaamini hofu ndio inaua kuliko ugonjwa wenyewe, ndio maana tumeamua kutoana hofu hata watu wakifa tusiogope tuone ni kawaida tu. Acha ukimya uwepo ili maisha yaendelee atakae kufa itakua ni changamoto za upumuaji tu na maisha yanaendelea kwa wengine.
 
Hivi kuna taarifa rasmi ya Wizara inayoonesha sasa hiv tuna wagonjwa wanne? Au ni zile porojo za kwenye majukwaa Na madhabahuni ya viongozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Una maanisha wizara gani mkuu? Hii nchi imekuwa ya mtu mmoja tu, ndie mwenye mamlaka yote yakuamua nini chakusema na nini cha kufanya. Unajua kwa nini taarifa za covid-19 zinatoka kupitia nyumba za ibada? Hii maana yake ni kwamba kuna kitu hakipo sawa sasa ujumbe ukitokea sehemu hizo utaaminika kwamba ni mpango wa mungu. Amini usiamini mkuu kama taarifa za kweli zinatolewa utashtuka sana jinsi hali ilivyo, achana na hizi porojo zakuulizana kama kweli corona ipo nani ameugua/amefariki nyumbani kwenu? Kwa mfumo wa maisha ya afrika nivigumu sana kuamini nchi jirani hali ni mbaya lakini kwa jirani kuwe na usalama wakutosha kiasi hiki?
 
Kile kimama chausiku ukikiangalia usoni naona kinatamani kiwe kinataja data za ndoo za maji tiririka mpaka zilizopo mitaa ya mtondoroni
 
Baada ya usingizi kukata nikaamua kuingia kwenye mtandao maarufu wa
Coronavirus Update (Live): 6,844,705 Cases and 398,141 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer unaotoa taarifa za corona kwa kila nchi. Nimestaajabu kuona wanasema Tanzania bado tuna wagonjwa 305. Nachojua ni kuwa mtandao huu huwa unabadirisha taarifa kila wanaposikia serikali ya nchi husika imetoa update. Na kama nakumbuka vizuri taarifa ya mwisho ilisema wagonjwa wamebaki 3, sasa ni kwanini hadi leo hawajabadirisha? Mbona nchi nyingine wanazifanyia update kila siku?

Je, wamegoma kutuamini, wameamua kutususa, hawatuelewi au wanatuonea wivu wanajisikia vibaya kuandika Tanzania is free from corona virus?
View attachment 1469840
Nikisikia hizi ngonjera kwamba mabeberu wanatuhujumu, nacheka sana,
Yaani watu wapo ulaya wanaandika, sisi mishuzi tele, je wakiamua kuja kabisa, kwa mbinu zote, wahujumu miundombinu, wafanye mauaji itakuaje
Viongozi wa Africa wa miaka ya 50+ndio wanajua muziki wa mabeberu sio hawa mafisadi wa sasa hv,
Beberu akuhujumu harafu kesho anakupa mkopo na msaada wa miradi yako,
Anayetuhujumu ni yupi? Yule yule anayefadhili fly over ya ubungo au ni yule aliyetupa mkopo wa kujenga miradi ya maji?
Let's be serious,
 
Hizo takwimu hazipo kwa sababu viongozi wameamua kutokutoa takwimu zozote rasmi, ingia tovuti ya Wizara ya Afya halafu uangalie ni wapi wametoa taarifa kuwa wamebaki wagonjwa wanne tu. Inamaana na Wizara inaendeshwa na mabeberu ?

Link hiyo hapo chini
Covid-19
 
ni kwa sababu serekali yetu imeshindwa kufuata instruction rahisi ya kuzingatia format ya utoaji data.....

wangapi wamepimwa
wangapi wamepatikana na maambukizi
wangapi wamekufa
wangapi wamepona

serekali haitaji hata kimoja kati ya hivyo hapo juu kwenye taarifa zake ambazo huzitoa kupitia hotuba za wanasiasa!

utawalaumu "mabeberu" kwa lipi?
Kwani roho zetu zinashikiliwa na hao.....ule mwezi wa kufa ni wao sema mama bill gate hakuangalia vizuri
 
Ugonjwa feki wa kutengenezwa wa corona haupo kwa waafrika.
Ungekuwa fake.. leo S.Afrika wasingekuwa na 40000+ maambukizi.
Ungekua fake tusinge funga mashule wala kusimamisha baadhi ya shughuli.
Ungekuwa fake.. leo brazil asingekuwa wa pili kwa maambukiz dunian?
Ungekuwa faka dunia isingepoteza watu 393000 mapaka sasa.
 
Barakoa inazuia hewa safi oksijeni ,seli (kingamwili) kufa kwa kukosa hewa.mkuu hujasoma biolojia munakwamaa sana mabalakoa yenu, tafute biashara ingine ya kufanya.
Kwa hiyo ww ni mtaalam kuliko madkatari walio toa tahadhari?
Nadhani hufaham barokoa inatumika wapi.
Only ukiwa kwenye mikusanyiko. Ukiwa sehem peke yao hutumii.
Wataalam si wajinga kutoa mapendekezo hayo.
 
Back
Top Bottom