Mabeberu wanafanikiwa kirahisi kwa aina ya marais wetu Afrika

Mabeberu wanafanikiwa kirahisi kwa aina ya marais wetu Afrika

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Nilimsikia Rais wetu Samia akihutubia mkutano wa kimataifa huko Quatar hivi majuzi. Alilalamika kuhusu kutokuwa na usawa wa ugawaji wa chanjo duniani.

Nikacheka kimoyoni nikasema hata Rais wetu kaingia mkenge au kaamua kushiriki hila za mabeberu kutuundia magonjwa na kisha kujidai ukarimu kutuuzia dawa au chanjo.

Wametufikisha mahali pa kugombea dawa au chanjo huku magonjwa mengine kama ilivyokuwa covid 19 yakiwa bandia. Bandia kwa vile kulikuwa na utiaji chumvi na vitisho vya athari vilivyofanyika. Tukaibiwa fedha zetu kununua makorokoro ya kila aina pia kuzuiwa lockdowns ambazo zilidhuru sana uchumi wa nchi zetu. Tanzania tushukuru ujuzi na ujasiri wa Magufuli kukataa ulaghai na kukataa lockdowns ndio maana uchumi wetu haukuathirika sana.

Samia anatakiwa kuwa mjanja asiingie kichwakichwa kwenywe ulaghai wa mabeberu. Nchi kama Cuba na Urusi waliepa kuibiwa na mabeberu kwa kutengeneza chanjo zao na vifaa vyao wenyewe huku wakielewa ugonjwa wenyewe vizuri.

Sisi chini ya JPM tulifanya kwa kiasi ila mama kuingia tu akasalimu amri baada ya haraka kutembelewa na maajenti wa ubeberu kina Tony Blair na kuwapa dili eti kuitangaza nchi yetu upya kutokana na sifa mbaya chini ya JPM kitu wala sio kweli.
 
anatakiwa kua mjanja asiingie kichwakichwa kwenywe ulaghai wa mabeberu. Nchi kama Cuba na urusi waliepa kuibiwa na mabeberu kwa kutengeneza chanjo zao na vifaa vyao wenyewe huku wakielewa ugonjwa wenyewe vizuri
Wewe nawe uwage unaangalia na watu! Kuna ubongo humo?
 
Nilimsikia rais wetu samia akihutubia mkutano wa kimataifa huko Quartar hivi majuzi.
Alilalamika kuhusu kutokua na usawa wa ugawaji wa chanjo duniani.
Nikacheka kimoyoni nikasema hata rais wetu kaingia mkenge au kaamua kushiriki hila za mabeberu kutuundia magonjwa na kisha kujidai ukarimu kutuuzia dawa au chanjo.
Wametufikisha mahali pa kugombea dawa au chanjo huku magonjwa mengine kama ilivyokua covid 19 yakiwa bandia. Bandia kwa vile kulikua na utiaji chumvi na vitisho vya athari vilivyofanyika. Tukaibiwa fedha zetu kununua makorokoro ya kila aina pia kuzuiwa lockdowns ambazo zilidhuru sana uchumi wa nchi zetu. Tanzania tushukuru ujuzi na ujasiri wa Magufuli kukataa ulaghai na kukataa lockdowns ndio maana uchumi wetu haukuathirika sana.
Samia anatakiwa kua mjanja asiingie kichwakichwa kwenywe ulaghai wa mabeberu. Nchi kama Cuba na urusi waliepa kuibiwa na mabeberu kwa kutengeneza chanjo zao na vifaa vyao wenyewe huku wakielewa ugonjwa wenyewe vizuri. Sisi chini ya jpm tulifanya kwa kiasi ila mama kuingia tu akasalimu amri baada ya haraka kutembelewa na maajenti wa ubeberu kina tony blair na kuwapa dili eti kuitangaza nchi yetu upya kutokana na sifa mbaya chini ya jpm kitu wala sio kweli.
COVID 19 eti ni bandia. Wewe shukuru Mungu hukulipata wewe au ndugu, jirani, rafiki hata jamaa yako.
 
COVID 19 eti ni bandia. Wewe shukuru Mungu hukulipata wewe au ndugu, jirani, rafiki hata jamaa yako.
Hebu fikiri kidogo. Tuliambiwa afrika watu watakua wanaokotwa barabarani wamekufa kwa covid 19. Huku afrika kwa mfano tanzania uliona wapi watu wote mitaani kama kariakoo wamevaa mabarakoa?Kwenye madaladala na mitaani watu kwa kiasi kikubwa waliendelea na maisha yao bila kujali sana. Hayo mabarakoa tuliona viongozi wetu kwenye tv kuanzia rais wamejifunga huku wanateseka kwa kukosa hewa safi. Kama hivyo mbona umma wakabakia salama hatukuona hivyo vivyo vya kuokotwa watu barabarani?
Jirani zetu waliyotii maelekezo ya wajanja wazungu wanajuta jinsi lockdowns zilivyoharibu uchumi wao. Viongozi wao wakala mabilioni yaliyoletwa kwa mkopo eti kama msaada kuwalisha chakula wakiwa lockdown😂😂😂😂🏃🤸💃🚶
Kikwete mtu bhana😂. Alisema cha kuambiwa changanya na chako.
 
Nani alisema hayo wewe Kasuku?
Hebu fikiri kidogo. Tuliambiwa afrika watu watakua wanaokotwa barabarani wamekufa kwa covid 19. Huku afrika kwa mfano tanzania uliona wapi watu wote mitaani kama kariakoo wamevaa mabarakoa?Kwenye madaladala na mitaani watu kwa kiasi kikubwa waliendelea na maisha yao bila kujali sana. Hayo mabarakoa tuliona viongozi wetu kwenye tv kuanzia rais wamejifunga huku wanateseka kwa kukosa hewa safi. Kama hivyo mbona umma wakabakia salama hatukuona hivyo vivyo vya kuokotwa watu barabarani?
Jirani zetu waliyotii maelekezo ya wajanja wazungu wanajuta jinsi lockdowns zilivyoharibu uchumi wao. Viongozi wao wakala mabilioni yaliyoletwa kwa mkopo eti kama msaada kuwalisha chakula wakiwa lockdown[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji125][emoji1732][emoji126][emoji124]
Kikwete mtu bhana[emoji23]. Alisema cha kuambiwa changanya na chako.
 
Siasa za kimataifa zinahitaji busara sana...
 
Nani alisema hayo wewe Kasuku?
Unamjua mke wa bill gates? And then katikati ya hii pandemic ya covid 19 wamedivorce kisa gani unajua? ..huyo sasa kama hujui ndio kasema wala usiniite kasuku mtu mjinga hujui.
 
Hivi hao unaowaita "Mabeberu" wakiamua kutumaliza mbona hakuna hata haja tuna mamilioni ya Watanzania ambao tunatumia Dawa za "Mabeberu" na hivi ninavyoongea kila sekunde kila saa watu wanapata maambukizi mapya.

"Mabeberu" wakiamua kuzuia Dawa zao hapatakalika hapa, harufu za Maiti zilizotupwa na kutelekezwa kwa maana tutazidiwa na Mizoga.

Kama ni "Njama" tayari tumeshajaa kwenye nyavu zao hatuna ujanja kwa sababu ya uhafifu wa IQ zetu.

Tena nasema kama wakiamua (Mabeberu) tutakuwa tunakufa huku tunajiona.
 
Unamjua mke wa bill gates? And then katikati ya hii pandemic ya covid 19 wamedivorce kisagani unajus? ..huyo sasa kama hujui ndio kasema wala usiniite kasuku mtu mjinga hujui.
Hata mimi nafahamu wameachana , lakini sababu za kuachana sizifahamu. Unaweza kutumegea mkuu?
 
Hivi hao unaowaita "Mabeberu" wakiamua kutumaliza mbona hakuna hata haja tuna mamilioni ya Watanzania ambao tunatumia Dawa za "Mabeberu" na hivi ninavyoongea kila sekunde kila saa watu wanapata maambukizi mapya.

"Mabeberu" wakiamua kuzuia Dawa zao hapatakalika hapa, harufu za Maiti zilizotupwa na kutelekezwa kwa maana tutazidiwa na Mizoga.

Kama ni "Njama" tayari tumeshajaa kwenye nyavu zao hatuna ujanja kwa sababu ya uhafifu wa IQ zetu.

Tena nasema kama wakiamua (Mabeberu) tutakuwa tunakufa huku tunajiona.
Kama hujui siku hizi sio wao tu wanatengeneza dawa. India na china ni watengenezaji wakubwa wa dawa. And then nchi nyingi zimeweka kipaumbele kwenye dawa kwa kujua wanaweza angamizwa na maadui. Ila watu waliyokata tamaa na kusalimu amri kama wewe kwa mabeberu wa magharibi ndio tatizo.
 
Wewe ndio huelewi, India na South Afrika wameachiwa under licence baada kilio kutoka Nchi masikini na haswa za Kiafrika hakuna kitu cha bure.
Afadhali kuliko kua mnunuzi tu. Na hakika ndio mwanzo wa kutengeneza dawa zao.
Wakati wa jpm ziko dawa zetu tulianza kutengeneza. Pia sio kweli kila dawa inatengenezwa india china brazil egypt cyprus na nchi zingine ni under licence.
 
Hata mimi nafahamu wameachana , lakini sababu za kuachana sizifahamu. Unaweza kutumegea mkuu?
Ukweli sijui. Ila nahisi huenda wametofautiana kuhusu ulaghai wao kwa walimwengu kuhusu mambo mbalimbali.
 
Ukweli sijui. Ila nahisi huenda wametofautiana kuhusu ulaghai wao kwa walimwengu kuhusu mambo mbalimbali.
Kilichoelezwa ni kukosekana uaminifu kwenye ndoa kwa upande wa Bill.

Labda kuna mengine yamefichwa, hatujui.
 
Back
Top Bottom