Mabeef ya mastaa yanayoshamiri nchini sio burudani tu, ni kioo cha hali ya jamii tuliyonayo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Siku hizi ukiangalia mitandao ya kijamii Tanzania kuna kitu kinaonekana wazi sana, ma-beef kati ya watu maarufu yameongezeka kwa kiwango kikubwa. Kila wiki kuna mtu kagombana na mwenzake, wengine wanachambana kwenye podcast, wengine Instagram story, wengine wanafichuana siri live kabisa mbele ya watu. Mwanzoni watu walikuwa wanaona kama ni burudani tu, lakini ukiangalia kwa undani unaweza kugundua hii ni zaidi ya entertainment. Inaonekana kama kuna hali fulani ya sintofahamu ndani ya jamii yenyewe.

Jamii yenye amani huwa haipendi sana migogoro ya kila siku. Lakini jamii yenye presha, msongo na kuchanganyikiwa huwa inaanza kuvutiwa zaidi na drama, hasira na mashambulizi ya maneno. Ndiyo maana leo ugomvi ndio unaopewa attention kuliko vitu vya maana. Watu wakikaa vizuri hawa trend, lakini wakitukanana au kufichuana ndipo kila mtu anakusanyika kusikiliza. Taratibu ugomvi umegeuka bidhaa ya kuvutia watu.

Mitandao ya kijamii nayo imeongeza moto zaidi. Zamani mtu angekasirika angekaa kimya au angeongea na mwenzake pembeni, lakini leo hasira zinawekwa public ndani ya dakika chache. Kila mtu anataka aonekane, asikike na apate engagement. Matokeo yake hata mambo madogo yanageuzwa vita kubwa kwa sababu drama inalipa attention kuliko utulivu.

Lakini nyuma ya haya yote kuna kitu kikubwa zaidi. Watu wengi kwa sasa wanaishi na stress ambazo hazionekani kirahisi. Ugumu wa maisha, pressure ya mafanikio, kutaka kuonekana muhimu, mashindano ya maisha ya mtandaoni, yote haya yanajenga hasira za ndani kwa ndani. Ndiyo maana hata uvumilivu umepungua. Mtu anachukizwa na kitu kidogo tu, tayari anaona ni sababu ya kuanzisha vita ya maneno mbele ya umma.

Kinachotisha zaidi ni kwamba hali hii inaanza kuhamia kwa jamii nzima. Sasa hata watu wa kawaida wameanza kuona kugombana ndio njia ya kujieleza. Ukifungua comment section kila mtu ana hasira, kila mtu anataka kushambulia mwenzake. Ni kama jamii imeanza kupoteza utulivu wa kuzungumza bila vita.

Inawezekana kabisa haya mabeef ya mastaa sio tatizo lao pekee, bali ni picha ya hali halisi ya jamii ya sasa. Kadri maisha yanavyozidi kuwa na pressure na watu wanavyozidi kutafuta attention kuliko kuelewana, ndivyo migogoro itakavyoonekana ya kawaida. Mwisho wa siku tunaweza kujikuta tunaishi kwenye jamii ambayo ugomvi ndio burudani, na utulivu unaonekana kama kitu kisicho na thamani.
 
Mtazamo wako ni sahihi, ingekuwa bora kama akina Samia na ccm na majeshi yao wangeliona hili. Wanajidanganya kuna Amani, ilhali jamii imejawa na ghadhabu, msongo wa mawazo na kughafilika.
 
Back
Top Bottom