Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Upande wa wanyama naelewa, ila hapa kwenye shangazi kaja haijaingia akilini kabisa! Kwamba anayetumia begi/mfuko wa shangazi kaja, huo mfuko unahesabika kama silaha? Au mtu akibeba shangazi kaja anakuwa halipi nauli? Yeye siyo mlipa kodi ambaye pesa yake imechangia kwenye kukamilisha ujenzi wa mradi huu? Au yeye ndio hana hadhi ya kutumia usafiri huu?
Gen Z hilo hapo ndio begi la shagazi kaja
===
Wazee wa kubeba zawadi kwa ndugu jamaa na marafiki hii ni ya kwenu, hasa kwa wale mnatumia mabegi/mifuko hii ya shangazi kaja.
Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.
Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.
Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.
Mwananchi