Mabegi ya 'shangazi kaja' marufuku kwenye kwenye treni ya SGR

Mabegi ya 'shangazi kaja' marufuku kwenye kwenye treni ya SGR

nazani wangeweka saizi ya shangazi kaja lisiwe kubwa kama lobota la nguo viwe vidogo vidogo sio kukataza kabisa
 
Oi! Kama watu hawataki kuacha Uswahili willingly basi itabidi iwe mandatory ili kuelekea kuwa moja ya nchi zilizostaharabika. Gradually mpaka tufikie viwango vya first world country. Hahahah!

But seriously ni amani sana ukienda nchi kama Japan na kukuta kila mtu ni mstaarabu ukipanda zile bullet train. We have to get there!
 
Upande wa wanyama naelewa, ila hapa kwenye shangazi kaja haijaingia akilini kabisa! Kwamba anayetumia begi/mfuko wa shangazi kaja, huo mfuko unahesabika kama silaha? Au mtu akibeba shangazi kaja anakuwa halipi nauli? Yeye siyo mlipa kodi ambaye pesa yake imechangia kwenye kukamilisha ujenzi wa mradi huu? Au yeye ndio hana hadhi ya kutumia usafiri huu?

View attachment 3038608
Gen Z hilo hapo ndio begi la shagazi kaja

===

Wazee wa kubeba zawadi kwa ndugu jamaa na marafiki hii ni ya kwenu, hasa kwa wale mnatumia mabegi/mifuko hii ya shangazi kaja.

Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.

Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.

Mwananchi
Wacha weeee
 
Tumeanza unyanyapaa mapema mno.

Imagine hata mihogo,mahindi ya kuchemsha na viazi mmekataa tusipande navyo???mnataka tufe njaa jamani,mtu bila kula anaishije???
View attachment 3038625
Mtu utapokelewa nini na wenyeji wako hapo DSM, tulishazoea kubeba kuku, bata, mahindi mabichi, mchele, maharage, maboga, kisamvu, samaki wakavu n.k. Hii sasa imeshakuwa ngumu kwa kweli.
 
Baridi tutakuja na hii kariakoo Bazar
image.png
 
Back
Top Bottom