Mabegi ya 'shangazi kaja' marufuku kwenye kwenye treni ya SGR

Lazima kuwe na standard, wamechelewa tu, wangepiga marufuku watu kuvaa madela, ndala na kuongea ongea hovyo

Kuna watu hawana ustaarabu kabisa, unalikuta jitu kubwa jinga linaongea na simu kwa sauti kama vile linatoa muhadhara au linafungulia ma-video bila ya kuvaa earphones, ushamba ni mwingi sana Tanzania
Hakika
 
Kwahiyo kuvaa mini skirt kwako ndio ubora kuliko anayevaa dera
 
Kuna mtu kafungulia redio yake ndogo anasikiliza kwenye train hana wasiwasi SGR ikiianza kwenda mwanza na kigoma wasipoweka standard itakuwa shida.
 
Lazima kuwe na standard, wamechelewa tu, wangepiga marufuku watu kuvaa madela, ndala na kuongea ongea hovyo

Kuna watu hawana ustaarabu kabisa, unalikuta jitu kubwa jinga linaongea na simu kwa sauti kama vile linatoa muhadhara au linafungulia ma-video bila ya kuvaa earphones, ushamba ni mwingi sana Tanzania
Hii ya kufungulia video au music bila eaphones ilinikuta siku moja.
Nimepanda zangu bus luxury..kijana kakaa nyuma yangu anasikiliza music wake kwa sauti ya juu. Kumbuka hapo kuna Tvs zipo on.

Nilivumilia uzalendo ukanishinda maana niliona kichwa kinadata kwa makelele mchanganyiko.
Nikamwita yule dada konda nikamwambia huyo mtu hapo nyuma anapiga kelele either azime mziki wake au avae eaphones. Nilikereka sana..
 
Huo mfuko ukijazwa sawasawa, ni ngumu kuuweka kwenye 'keria' ya ndani ile...

Pili, huu ni mfuko kwa ajili ya lumbesa, huenda imeamriwa hivyo ili kudhibiti usafirishaji wa vitu kama vyakula pasipo kuvifunga vizuri...

Upande wa wanyama naelewa, ila hapa kwenye shangazi kaja haijaingia akilini kabisa! Kwamba anayetumia begi/mfuko wa shangazi kaja, huo mfuko unahesabika kama silaha? Au mtu akibeba shangazi kaja anakuwa halipi nauli? Yeye siyo mlipa kodi ambaye pesa yake imechangia kwenye kukamilisha ujenzi wa mradi huu? Au yeye ndio hana hadhi ya kutumia usafiri huu?

View attachment 3038608
Gen Z hilo hapo ndio begi la shagazi kaja

===

Wazee wa kubeba zawadi kwa ndugu jamaa na marafiki hii ni ya kwenu, hasa kwa wale mnatumia mabegi/mifuko hii ya shangazi kaja.

Kati ya vitu vilivyopigwa marufuku kwenye usafiri wa treni ya umeme (SGR) ni mabegi ya shangazi kaja, wanyama wakiwemo wa kufungwa (wazee wa kuagiza kitoweo tumefikiwa), mifuko ya plastiki, silaha, chakula, vinywaji, ndoo na mapipa pamoja na mizigo inayozidi kilo 30.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kila kinachofanyika kinalenga kulinda usalama wa abiria, kadhalika viwango vya ubora wa treni na huduma kwa ujumla.

Kwa sasa treni hiyo tangu ilipoanza kutoa huduma wiki tatu zilizopita, inafanya safari za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwamba kufikia Julai 25, mwaka huu safari zitaongezwa hadi Dodoma.

Mwananchi
 
Huo mfuko ukijazwa sawasawa, ni ngumu kuuweka kwenye 'keria' ya ndani ile...

Pili, huu ni mfuko kwa ajili ya lumbesa, huenda imeamriwa hivyo ili kudhibiti usafirishaji wa vitu kama vyakula pasipo kuvifunga vizuri...
Watu hawaijui SHANGAZI KAJA IKIJAA. Kuna watu nimesoma wanasema mbona ndege wanaruhusu. Hawajui mabegi makubwa kwenye ndege yanawekwa sehemu ya chini huko na bag moja halitakiwi kuzidi 30kg. La kuingia nalo kwenye cabin ni 10kg only. Sasa hio treni haina sehemu ya mizigo kama ndege. Imagine kila mtu aingie na begi lake kubwa huko itakuwaje? Wengine waingie na kuku mbuzi viroba vya mahindi au viroba vya mihogo si balaa hio
 
Aaah bwana weh! Watuletee lenye kubeba shangazi kaja zetu.
 
Back
Top Bottom