Mabehewa 264 ya SGR ya kubeba Mizigo yawasili nchini

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Screenshot_2024-12-25-15-21-19-353_com.instagram.android-edit.jpg

Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa - SGR yamewasili Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China Disemba 24, 2024.

Zoezi la ushushaji kutoka kwenye Meli litakapokamilika litafuatia zoezi la majaribio ambalo litajikita katika kutembeza mabehewa hayo kwenye Reli yakiwa tupu na kisha yakiwa yamebeba mizigo. Mabehewa hayo yatakuwa yanatembea kwa kasi ya kilometa 120 kwa saa.

Majaribio hayo yatakamilika mara tu wataalamu wa Shirika la Reli wakishirikiana na wale wa mkandarasi watakaporidhika kuwa utendaji kazi wa mabehewa hayo umekidhi viwango kulingana na Mkataba.

Tarehe rasmi ya kuanza operesheni za mabehewa hayo, Shirika litauujulisha Umma.
Katika mabehewa hayo 264 yaliyowasili, 200 ni ya kubeba makasha (makontena) na mabehewa 64 ni ya kubeba mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Shehena hiyo ya mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba yanatengenezwa na kampuni ya CRRC ya nchini China.

Novemba 15, 2024 Shirika liliutaarifu umma kuwa utengenezaji wa mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa SGR umekamilika nchini China na Meli iliyobeba mabehewa hayo iling'oa nanga katika Bandari ya Dalian, China Novemba 12, 2024.
 
Kuna mtu aliwahi hoji kwanini Hi reli isingekuwa yaelekea Zambia then DRC maana kwa njia ya huko ndo Salama kwa mizigo inayotoka Congo ,Ikiwa lengo la Reli ni kwaajili ya Kusafirisha mizigo.

Mabehewa 1400 yatakuwa na kazi gani kwa reli ya kati (kwa mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi?)
 
Tumejipanga vipi kukabiliana na
  1. Hujuma za wamiliki wa bundi na ngedere
  2. Kukatika kwa umeme kila siku
 
Kuna mtu aliwahi hoji kwanini Hi reli isingekuwa yaelekea Zambia then DRC maana kwa njia ya huko ndo Salama kwa mizigo inayotoka Congo ,Ikiwa lengo la Reli ni kwaajili ya Kusafirisha mizigo.

Mabehewa 1400 yatakuwa na kazi gani kwa reli ya kati (kwa mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi?)
Kupeleka sgr kanda ya ziwa badala ya kusini ilikuwa ni uamuzi mbovu sana, labda kwa sasa wajikite kujenga bandari kavu dodoma ili burundi na rwanda waweze kichukua makontena yao pale, msongamano wa malori mjini upungue.
Again mizigo ya huko ni one way traffic hakuna kinachotoka burundi na rwanda labda mikungu ya ndizi pale bukoba.
 
Kuna mtu aliwahi hoji kwanini Hi reli isingekuwa yaelekea Zambia then DRC maana kwa njia ya huko ndo Salama kwa mizigo inayotoka Congo ,Ikiwa lengo la Reli ni kwaajili ya Kusafirisha mizigo.

Mabehewa 1400 yatakuwa na kazi gani kwa reli ya kati (kwa mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi?)
Huu ndo mwanzo mzuri kwa bandari kavu ya kwala kuanza kazi,

Magari ya kupeleka mizigo mikoani yataishia pale vigwaza, huku mjini tutapunguza foleni hususani barabara ya mandela
 
Njia iliyopelekwa ndio ina faida. Maana ina nchi nyingii.

Sgr inapelekwa mpaka kigoma na mipakani mwa nchi jirani, sio mwanza peke yake
 
Kuna mtu aliwahi hoji kwanini Hi reli isingekuwa yaelekea Zambia then DRC maana kwa njia ya huko ndo Salama kwa mizigo inayotoka Congo ,Ikiwa lengo la Reli ni kwaajili ya Kusafirisha mizigo.

Mabehewa 1400 yatakuwa na kazi gani kwa reli ya kati (kwa mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi?)
Screenshot_20241225-215106_Gallery.jpg

Route iko fresh. N nchi jirani na wao kuanza ujenzu wakifikiwa
 
Huu ndo mwanzo mzuri kwa bandari kavu ya kwala kuanza kazi,

Magari ya kupeleka mizigo mikoani yataishia pale vigwaza, huku mjini tutapunguza foleni hususani barabara ya mandela
Hiyo icd ni bora ingejengewa morogoro kabisa mana pale ndio kuna junction ya mikoa mbali mbali.
 
View attachment 3184742
Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa - SGR yamewasili Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China Disemba 24, 2024.

Zoezi la ushushaji kutoka kwenye Meli litakapokamilika litafuatia zoezi la majaribio ambalo litajikita katika kutembeza mabehewa hayo kwenye Reli yakiwa tupu na kisha yakiwa yamebeba mizigo. Mabehewa hayo yatakuwa yanatembea kwa kasi ya kilometa 120 kwa saa.

Majaribio hayo yatakamilika mara tu wataalamu wa Shirika la Reli wakishirikiana na wale wa mkandarasi watakaporidhika kuwa utendaji kazi wa mabehewa hayo umekidhi viwango kulingana na Mkataba.

Tarehe rasmi ya kuanza operesheni za mabehewa hayo, Shirika litauujulisha Umma.
Katika mabehewa hayo 264 yaliyowasili, 200 ni ya kubeba makasha (makontena) na mabehewa 64 ni ya kubeba mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Shehena hiyo ya mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba yanatengenezwa na kampuni ya CRRC ya nchini China.

Novemba 15, 2024 Shirika liliutaarifu umma kuwa utengenezaji wa mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa SGR umekamilika nchini China na Meli iliyobeba mabehewa hayo iling'oa nanga katika Bandari ya Dalian, China Novemba 12, 2024.
Jamaaa watakua wamekula commission nzuri Sana Sana
 
Hiyo icd ni bora ingejengewa morogoro kabisa mana pale ndio kuna junction ya mikoa mbali mbali.
Umeongea jambo la msingi sana mkuu lakini kwa sababu fulani fulani hili halitokaa litokee...hata hii SGR kama siyo jiwe kukomaa ingekuwa stori kama ilivyo kwa katiba mpya...
 
Back
Top Bottom