Inadaiwa kuwa mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).
Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.
TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.
Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020
Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)
EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRC kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)
Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRC hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.
TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC
Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.
TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk
Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk
Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.

- Tunachokijua
- Shirika la Reli Tanzania, TRC linakanusha taarifa iliyotolewa katika Gazeti la Jamhuri tarehe 22 Novemba, 2022 yenye kichwa cha habari ”MABEHEWA YA SGR YAZUIWA UJERUMANI"
TRC wanaeleza kuwa taarifa hiyo haina ukweli na ina lengo la kupotosha umma kuhusu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza na kuboresha Sekta ya miundombinu ya reli nchini.
Mkataba wa matengenezo ya behewa thelathini (30) na vichwa viwili (2) vya treni kati ya Shirika la Reli Tanzania na kampuni ya Euro Wagon ulivunjwa mnamo tarehe 25 Februari 2022 baada ya kampuni kushindwa kukidhi matakwa ya mkataba, hatua iliyopelekea TRC kutafuta mkandarasi mwingine ambaye ni kampuni ya LUCKEMEIER TRANSPORT AND LOGISTICS GMBH ya nchini Ujerumani.
Kazi ya matengenezo ya behewa inaendelea chini ya kampuni ya LUECKEMEIER TRANSPORT AND LOGISTICS GMBH na inaendelea vema.
Taarifa ya TRC kukanusha madai ya kuuzwa kwa behewa Nchini UjerumaniTRC haijapokea taarifa yoyote kuhusu kuzuiwa au kuuzwa kwa behewa kutoka kwa mkandarasi ambaye ni kampuni iliyopewa dhamana ya kuendelea na matengenezo ya behewa.
Shirika la Reli Tanzania linatoa huduma ya usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli, TRC imepewa dhamana ya kujenga, kuendeleza na kusimamia miundombinu ya reli.
Kwa sasa TRC inasimamia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa -SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam Mwanza na ujenzi unaendelea vema.
TRC inataraja kupokea behewa za SGR zilizotengenezwa na kampuni Sung Shin Rolling Stock Technology Limited (SSRST) kutoka Korea ya Kusini rasmi tarehe 25 Novemba, 2022 siku ya ljumaa, hivi sasa behewa hizo zimeshafika Bandari ya Dar es Salaam tayari kwaajili ya kushushwa.