SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna hii trend imeibuka ya wachezaji kushuka viwango (na wengine hawajawahi kuonyesha hivyo viwango) kutokana na tabia zao mbofu mbofu za nje ya uwanja halafu wanadai wamerogwa, wanakimbilia kuombewa badala ya kurudisha kwanza nidhamu ya kazi.
Itakuwaje mabeki pamoja na magolikipa nao wakidai wamerogwa wakafurika katika maombi, huu mpira wetu utakuwaje? Hatuoni kuwa tutakuwa tunakosea kumpa Mungu majukumu ya kuamua mechi?
Atukuzwe Mwenyezi Mungu ila tuwe pia na nidhamu katika kazi zetu.