Mabeki wa pembeni wa England

Mabeki wa pembeni wa England

mikedean

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
3,267
Reaction score
4,634
England ina utajiri wa kikosi kipana kama zilivyo nchi nyingine za ulaya kama vile Ujerumani, Spain na Ubelgiji.

Hata hivyo kwa upande wa England suala hilo linaleta utamu zaidi badala ya changamoto kwa sababu ya performance ya wachezaji wengi kuwa sawa. Nafasi pekee ambayo imehakikishwa ni ya golikipa ambaye ni Pickford wa Everton.

Tukirudi kwenye mada, England ina mabeki wa pembeni rightback 4 bora nao ni Trend Arnod wa Liverpool, Kieran Tripier wa Atletico madrid, Aaron Bissaka wa Manchester United na Mkongwe Kyle Walker wa Manchester City. Hawa wote kwa mtu anayefuatilia vizuri mpira wa majuu anajua performance zao katika timu zao.

Lakini baadhi wanasema kuwa Arnod na Trippier hawa ni wing-back zaidi kuliko kuwa full-back (right-back) kama ilivyo kwa Bissaka na Walker wakimaanisha kuwa Arnod na Trippier ni wazuri kupandisha mashambulizi kuliko kukaba huku Bisaka na Walker wakiwa wazuri kukaba kuliko kupandisha mashambulizi.

Walker na Trippier walicheza Euro 2018 na kuishia nusu fainali na Arnod pia, lakini Bissaka huenda haya ndo yatakuwa mashindano yake ya kwanza makubwa kwa timu ya taifa.Hata hivyo Southgate alikuwa amemwacha Walker kwenye baadhi ya mechi za kufuzu Euro japo hatujui kama hata kwenye Euro yenyewe atampiga chini tena.

Je, wewe unaonaje kati ya wao ma right- back wanne,ungekuwa ndo kocha wa England ungechukua wapi (2) na kuwaacha wengine wawili na kwa sababu (z)ipi?

Mimi ningechukua Arnod na Bissaka na ningewapanga kulingana na aina ya mchezo wapinzani wetu wanacheza.kama tunashambuliwa mfano tunacheza na Belgium au spain na Ujerumani lakin kama ni timu mfamo ufaransa, Italy, Croatia, Wales na zinginezo naanza na Trent ili sisi tushambulie zaidi na kwa nguvu kubwa.

IMG_20200303_111944.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Wan Bissaka kwenye pecking order yuko chini hukoo mtu gaani hata cross kupiga shida unakimbia kama una mdondo? Nadhani list iko ivi

1. Trent Alexander Arnold
2. Kyle Walker
3. Trippier
Na nadhani hao wawili wa juu ndo wataenda Euro
 
  1. Trippier ni majeruhi kwa sasa
  2. kama southgate atakuja tena na mfumo wa 3-5-2 upo uwezekano mkubwa wa kumtumia kyle walker eneo la ulinzi wa kati
  3. hivyo basi upo uwezekano wa kuwachukua walinzi watatu wanaocheza upande wa kulia (arnold + walker) na mmoja kati ya hao wawili waliobakia.
  • kwenye eneo la goalkeeper umemsahau dean henderson anayechezea sheffield united
  • huo upana wa kikosi unaupima kwa kutumia kigezo cha kuwa na kundi kubwa la wachezaji au kwa kuangalia ubora wa wachezaji husika?
kama ni ubora wa wachezaji basi england hawana kikosi kipana ila kama umetumia kigezo cha kuwa na kundi kubwa la wachezaji basi ni kweli england wana kikosi kipana kama ilivyo Taifa stars.
 
Wewe mtoa mada huna taarifa sahihi hasa hasa hapo golini utahamaki sana ukifika mwezi wa sita. Ktk nafasi iliyo ngumu kwa Gareth kufanya maamuzi ni hapo golini, Dean Henderson na Nick Pope wapo moto sana.

Jordan Pickford sina hakika kama atakuwa namba moja. Dean au Nick mmoja wao ndiye atakaa golini akisaidiwa na Jordan.
 
kwa mfumo wa mabeki wanne nyuma ,fullback right nawaona walker na trent nd wapo vzuri zaidi japo southgate amekua akimuamin trent sna.. sion nafas y AWB kwnye iyo nafasi kwa form waliy nayo hao jamaa msimu hu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sawa unachosema lakin taarifa sahihi ninazo sema unajua makocha wakati mwingine huwa wanapanga vikosi kwa mazoea.Kwa hiyo ndo maana nimeona kuwa pickford bado atapewa nafasi ya kuendelea kukaa langoni.
Ila maamuzi ya mwisho ya nani apangwe na nani abaki mwisho wa siku yako kwa kocha.Ila huyo kipa wa sheffild sinamwangalia sana ila Nick pope yuko vizuri sana
Wewe mtoa mada huna taarifa sahihi hasa hasa hapo golini utahamaki sana ukifika mwezi wa sita. Ktk nafasi iliyo ngumu kwa Gareth kufanya maamuzi ni hapo golini, Dean Henderson na Nick Pope wapo moto sana.

Jordan Pickford sina hakika kama atakuwa namba moja. Dean au Nick mmoja wao ndiye atakaa golini akisaidiwa na Jordan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro hapo unaposema wakicheza watatu nyuma huenda Walker akacheza beki ya kati kwa maana kwamba kulia, Trent Arnod ,katikati kayle Walker na kushoto Dani Rose au Shaw? Nadhani kama atacheza watatu katikati atacheza Maguire au Stones.Lakin ni vema kama Engaland wakawa wanatumia 4-3-3 hiyo ndo itawafanya kuwa bora zaidi.
  1. Trippier ni majeruhi kwa sasa
  2. kama southgate atakuja tena na mfumo wa 3-5-2 upo uwezekano mkubwa wa kumtumia kyle walker eneo la ulinzi wa kati
  3. hivyo basi upo uwezekano wa kuwachukua walinzi watatu wanaocheza upande wa kulia (arnold + walker) na mmoja kati ya hao wawili waliobakia.
  • kwenye eneo la goalkeeper umemsahau dean henderson anayechezea sheffield united
  • huo upana wa kikosi unaupima kwa kutumia kigezo cha kuwa na kundi kubwa la wachezaji au kwa kuangalia ubora wa wachezaji husika?
kama ni ubora wa wachezaji basi england hawana kikosi kipana ila kama umetumia kigezo cha kuwa na kundi kubwa la wachezaji basi ni kweli england wana kikosi kipana kama ilivyo Taifa stars.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubora wa kikosi upo kaka Eneo ambalo wanashida sana ni kiungo cha akina Dier na Henderson chambErlain na wengine bado quality sio kubwa wakikutana na vigogo kama ufaransa,ujerumani,na ubelgiji.Lakin mabeki na washambuliaji wako vizuri magolikipa pia sio sana.Kikosi chao ukikirate unaweza kuwapa 7.5/10 Ukilinganisha na nchi nyingine mfano ureno pia wana kikosi kizuri sana safari hii

Back
Top Bottom