mikedean
JF-Expert Member
- Mar 15, 2018
- 3,267
- 4,634
England ina utajiri wa kikosi kipana kama zilivyo nchi nyingine za ulaya kama vile Ujerumani, Spain na Ubelgiji.
Hata hivyo kwa upande wa England suala hilo linaleta utamu zaidi badala ya changamoto kwa sababu ya performance ya wachezaji wengi kuwa sawa. Nafasi pekee ambayo imehakikishwa ni ya golikipa ambaye ni Pickford wa Everton.
Tukirudi kwenye mada, England ina mabeki wa pembeni rightback 4 bora nao ni Trend Arnod wa Liverpool, Kieran Tripier wa Atletico madrid, Aaron Bissaka wa Manchester United na Mkongwe Kyle Walker wa Manchester City. Hawa wote kwa mtu anayefuatilia vizuri mpira wa majuu anajua performance zao katika timu zao.
Lakini baadhi wanasema kuwa Arnod na Trippier hawa ni wing-back zaidi kuliko kuwa full-back (right-back) kama ilivyo kwa Bissaka na Walker wakimaanisha kuwa Arnod na Trippier ni wazuri kupandisha mashambulizi kuliko kukaba huku Bisaka na Walker wakiwa wazuri kukaba kuliko kupandisha mashambulizi.
Walker na Trippier walicheza Euro 2018 na kuishia nusu fainali na Arnod pia, lakini Bissaka huenda haya ndo yatakuwa mashindano yake ya kwanza makubwa kwa timu ya taifa.Hata hivyo Southgate alikuwa amemwacha Walker kwenye baadhi ya mechi za kufuzu Euro japo hatujui kama hata kwenye Euro yenyewe atampiga chini tena.
Je, wewe unaonaje kati ya wao ma right- back wanne,ungekuwa ndo kocha wa England ungechukua wapi (2) na kuwaacha wengine wawili na kwa sababu (z)ipi?
Mimi ningechukua Arnod na Bissaka na ningewapanga kulingana na aina ya mchezo wapinzani wetu wanacheza.kama tunashambuliwa mfano tunacheza na Belgium au spain na Ujerumani lakin kama ni timu mfamo ufaransa, Italy, Croatia, Wales na zinginezo naanza na Trent ili sisi tushambulie zaidi na kwa nguvu kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app