Acheni utani jamani Mabere siyo ajenti wa TISS na wala hajawahi kuwa ajenti wa TISS.. kama makumi ya watu ambao wamekuwa wakijipitisha kuwa ni maajenti wa TISS.. ni wale wanaoitwa huku "starving artists"
Well said. Asipewe ''special treatment'' lakini pia asinyimwe haki zake.
Chadema iongozwe kwa ''principles'' na si kwa matakwa.
siasa mchezo hatari saana, jamani ni kwa sababu ya milioni mia moja? Cku zote walikuwa wapi hawa? Au ndo kuhaha kwenyewe?
Ndugu yangu De Novo, kweli unamjua Mabere? - Mabere Marando aliyekuwa na jeuri ya kumwambia Mwalimu kuwa kafilisika kisiasa wakati wa kudai vyama vingi, Mabere Marando aliyemkatalia Raisi Mwinyi kumteua kwenye kamati aliyoiita ya kufuja kodi ya wananchi kuwauliza kama wanataka haki yao ya kidemokrasia, Mabere Marando aliyeichachafya Bunge kwa hoja nzito nzito kati ya 1995 - 2000, Mabere Marando aliye.. Duh, De Novo humjui Mabere Nyaucho Marando. Huwezi kuongelea mageuzi ya mwanzoni mwa mwaka 1990 bila kumtaja Mabere.sawa lakini that doesnt clean Mabere na kumfanya awe trusted!!!! How can CHADEMA welcome such a negative energy into the party??? its simple, they are desperate to score in a cricket game that that take whatever throw sent
Kusema ukweli, Mabere is not a face of opposition, he is a puppet!!
Wanabodi wengi tu humu wanajiandikia vitu kwa kufuata mkumbo, hakuna lolote wanalolijua. Eti Chadema wamkatae Marando...kwa sababu gani hakuna anayeweka hoja zozote zenye akili!!!
Mabere Marando ni Mwana Mageuzi halisi. Amekuwa akipigania vyama vingi tangu mwishoni mwa 1980's.
Watanzania wanashindwa kuelewa kuwa katika chama au jumuiya yoyote ni lazima kuwe na timu inayoweza kuendesha chama katika mapinduzi mbalimbali bila ya kuangalia maslahi ya mtu binafsi. NCCR walikosea hapo, walipoangalia maslahi ya Mrema badala ya chama mambo yote yakaenda kombo...hakukuwa na Timu tena kulikuwa na watu wachache wanao angalia maslahi yao.
Naamini kabisa Marando ni asset kubwa sana kwa Chadema na upinzani Tanzania hasa katika kulipigania jimbo la Rorya lilirudi upinzani. Mabere angejitosa tu kugombea tena Rorya, alishinda 1995 tena kwa kura nyingi tu...itakuwa leo. Mbunge wa sasa wa Rorya Prof Sarungi ameshajichokea.
Chadema ni chama makini na kina muelekea mzuri sana wa kuwa chama imara mbadala.
Jambo moja tu linaloonyesha wana utaratibu mzuri wa kuongoza Chama chao. Hebu jiulizeni ni nani ndani ya Chadema aliyewahi kugombea uraisi zaidi ya mara moja?
Kuna mashushu wengi tu wamekuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi. To mention a few ni kuwa James Mapalala ni ofisa usalama wa Taifa aliyekuwa mstari wa mbele kupigania "mageuzi", Harold Jaffu ofisa usalama wa taifa mzuri tu aliyefanya kazi nzuri sana ya kuhakikisha TLP haipati nguvu hata kidogo, mabere marando amefanya azi nzuri sana ya kuhakikisha NCCR Mageuzi inakuwa kopo tu. Huwa Mabere hashindwi assignments zake, TISS wanajua kuwa yeye ni mtu smart na capable. He will deliver the goods and CHADEMA will go to their knees sooner than later.
Serikali iliposema inaruhusu vyama vingi vya siasa, ilifanya hivyo ili kuwaridhisha donors lakini ukweli ni kuwa haitaki na wala haikutaka. Mpaka leo watu wa usalama wa Taifa wanaambiwa kabisa kuwa mama ni CCM (sio Tanzania) so at any cost CCM itaendelea kulindwa na kuhakikisha inapata ushindi. Mnaosema kuwa mapandikizi ya CCM sasa hawako active TISS mnaota ndoto za mchana, just ask George Liundi atawaeleza. So if you think Marando is harmless you are dreaming, just wait and see.
Watu wenye mawazo kama yako ni sumu katika maendeleo ya aina yoyote achilia mbali siasa.
Huna hoja zaidi ya kuendekeza imani potofu ya woga ili mradi woga uliotokana na uzushi wa vijiweni.
Historia ya NCCR inajulikana wazi imewekwa hapa na wanabodi mbalimbali ambao wanamfahamu Marando na wapinzani wengine tangu miaka ya 1980's...kana kwamba hiyo haitoshi imefafanuliwa hapa kuwa kifo cha NCCR kilikuwa na sababu za msingi za kimuundo, ubinafsi n.k sababu za kisomi kabisa...lakini bado mnakuja na hizo hadithi za alfa ulela. Hadithi za kumtafuta mchawi anayeuwa upinzani.
Kalaghabaho...kwa fikra hizi CCM itaendelea kuwa madarakani milele.
Mkuu maoni yako nayaelewa vizuri sana, lakini I am entitle to my opinion whether am from kijiweni or mlimani. Kama unaona ni bahati mbaya CCM iko madarakani pamoja na mafyongo yote inayofanya utakuwa uanafanya makosa makubwa. If you think structural weaknesses are responsible for the demise of NCCR then you are dreaming. To tell you the truth, almost every party in this country, CCM included, have a lot of sturctural problems, can you tell why are they still kicking? We are living in really world, you need to be in the game to feel the heat of how is it being played. Waulize CCJ they will tell you. Ligthen up mkuu.
Kwanza we Bujibuji kwanini hukuwa patient kuliko kusaga, hatimaye huyo kaenada sasa. Kwa kweli CHADEMA Ipo mbioni kuvurugwa kwa ufupi wamkatae na kama ni Upinzani apigane huko huko NCCR alipo
Tumpe muda; tutaona mwisho wake; na Chadema haitasambaratika kwa sababy ya mtu mmoja; i propose akagombee au akapige debe rorya maana ni mpiga debe na mwenye sauti mzuri