Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Naungana nawe Mwanakijiji kuwa Marando si TISS na wala hajawahi kuwa agent. Maagent wa TISS tunawafahamu na CHADEMA pia inawajua na wnegine tayari wapo ndani ya Chama.
Mimi nimemfahamu Marando kwa muda na nilijua kuwa atasuport CHADEMA kwenye uchaguzi toka mwezi wa tatu. Ila sikujua kuwa atajiunga rasmi kama Mwanachama.
Sasa tuongelee potentiality ya Marando:
1. kwanza kuwepo kwake kutahakikisha jimbo la Rorya linaenda CHADEMA (atakayebisha kwenye hili asubiri Octoba 31).
2. Ataisaidia sana CHADEMA kurejesha jimbo la Tarime ambalo kwa bahati mbaya sana CHADEMA ina kila dalili ya kulikosa kutokana na migongano isiyo ya lazima (infighting kati ya Mwikabe, heche na Mwera).
3. Mabere atakuwa msaada mkubwa sana kwa SLAA kwa kanda ya Ziwa maana anaheshimika sana.
4. Marando is a reputed public orator na anaweza kuteka masikio na kura za wasomi.
5. Marando hagombei uongozi wowote katika CHADEMA wala nchi so CHADEMA haina cha kupoteza.
Mimi si mshabiki wa personalities za watu ila imenibidi niseme kuweka records straight.
Uko sahihi kabisa Devils Advocate, tatizo ni kuwa wengi hawajui Marando ameplay role gani Chadema hadi leo na mahusiano yakoje kati yake na viongozi wa Chadema. Ningependa niwaulize tu kitu kimoja tu nacho ni hiki, ikiwa Uongozi wa Chadema hauoni taabu yoyote kushirikiana na Marando, wanaopinga uwepo wake Chadema wanatuambia nini - kwamba tayari leo hii hawana imani na maamuzi ya hao viongozi pamoja na kipenzi chetu Dr. Slaa ? Je wanafikiri wanamfahamu Marando kuliko Dr. Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika na wengineo ? Kama mnaanza kukosa imani na Dr. Slaa kwenye hili swali dogo la Marando kweli mko tayari kuwa wapiganaji anaowahitaji ?
Marando wengine tunamfahamu vizuri kuliko wengi wenu mnaomfananisha na Mrema na tuna hakika he is a big big asset kwa Chadema. Binafsi ningewaomba wana JF na hasa walioko tayari kuunga mkono jitihada za kuiondosha CCM madarakani, tuachane na haya mambo ya kuungaunga bila ushahidi kamili. Katika wasemaji wanaoweza kuvutia umati Marando ni mojawapo, he is a polished and convincing public orator ambaye ungependa umsikilize hadi mwisho akiwa jukwaani - ni wachache wenye kipaji kama chake. Huu utakuwa ni mchango wangu wa mwisho kwa sababu sitaki kuonekana kama nina ajenda iliyojificha ya namfagilia sana. Go Dr. Slaa, go !