Elections 2010 Mabere Marando kuibukia CHADEMA?


Uko sahihi kabisa Devils Advocate, tatizo ni kuwa wengi hawajui Marando ameplay role gani Chadema hadi leo na mahusiano yakoje kati yake na viongozi wa Chadema. Ningependa niwaulize tu kitu kimoja tu nacho ni hiki, ikiwa Uongozi wa Chadema hauoni taabu yoyote kushirikiana na Marando, wanaopinga uwepo wake Chadema wanatuambia nini - kwamba tayari leo hii hawana imani na maamuzi ya hao viongozi pamoja na kipenzi chetu Dr. Slaa ? Je wanafikiri wanamfahamu Marando kuliko Dr. Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika na wengineo ? Kama mnaanza kukosa imani na Dr. Slaa kwenye hili swali dogo la Marando kweli mko tayari kuwa wapiganaji anaowahitaji ?

Marando wengine tunamfahamu vizuri kuliko wengi wenu mnaomfananisha na Mrema na tuna hakika he is a big big asset kwa Chadema. Binafsi ningewaomba wana JF na hasa walioko tayari kuunga mkono jitihada za kuiondosha CCM madarakani, tuachane na haya mambo ya kuungaunga bila ushahidi kamili. Katika wasemaji wanaoweza kuvutia umati Marando ni mojawapo, he is a polished and convincing public orator ambaye ungependa umsikilize hadi mwisho akiwa jukwaani - ni wachache wenye kipaji kama chake. Huu utakuwa ni mchango wangu wa mwisho kwa sababu sitaki kuonekana kama nina ajenda iliyojificha ya namfagilia sana. Go Dr. Slaa, go !
 
Atavuruga tu kama akipewa uongozi wa ngazi ya juu, lakini akiwa mwananachama wa kawaida as I predict atavurugaje????????

Siyo kweli kuwa mwanachama wa kawaida hawezi kuvuruga. Mifano iko mingi. Anaweza kukiburuza chama mahakamani au kufanya vurugu kwenye chama hasa ikiwa ametumwa na serikali kufanya hivyo. Sasa akiwa tena wakili aliyebobea ni tatizo moja baada ya lingine. Chadema na vyama vingine viunde kamati ya uthibiti, na siyo kumpokea kila mja. Mnamkumbuka Lenin? Better few but Better!
 

Anaweza kukiburuza chama kortini bila makosa? Kuwa wakili aliyebobea hakumpi nafasi ya kufinyanga kesi ili mradi tu akifikishe chama mahakamani, kwa kosa lipi?

Mwanachama wa kawaida ni ngumu sana kufanya fujo kwenye chama kwa kuwa hayuko kwenye kikao cha aina yoyote ama hahusiki na kufanya maamuzi mazito yanayogusa uhai ya chama.

Watu wa kuogopa ni wale wanaokuja na wafuasi/mashabiki wao, maana wafuasi/mashabiki wanafuata mtu hawaangalii sera za chama husika. Makosa kama hayo waliyafanya zama za Mrema na hao wafuasi wakapewa uongozi, so linapokuja swala nyeti wafuasi hawaangalii hoja, bali wanaangalia huyo mtu wao msimamo wake ni upi?

Marando ametamka wazi kwamba hataki kugombea Ubunge wala hataki uongozi ndani ya CHADEMA, anachotaka yeye ni kuwaongezea nguvu CHADEMA.

Pamoja na hayo, kila chama kina taratibu zake, nina imani CHADEMA ni watu makini sana na hivyo kabla ya kumruhusu kuingia kwenye Timu ya Kampeni watakuwa wamefanya vetting ya kiwango cha kwao na kujiridhisha kwamba Marando ana nia njema au la.

Kitu kingine ambacho tunasahau ni kwamba, ukiona watu maarufu kama Marando wanatangaza kuhamia chama fulani lazima anakuwa alishaongea na top brass ya chama husika na wamekubaliana na kwamba chama hakina tatizo. Kwa hiyo baraza la wadhamini na baraza la wazee wanajua, kamati kuu inajua na wameishafanya uchunguzi wao wa kina na kujiridhisha kwamba wanamkaribisha. Asingeweza kukurupuka bila kupata go ahead ya top brass ya CHADEMA.
 
Ama kweli mipandikizi imejaa JF. Cha kupoza moyo ni kuwa idadi ya Wazalendo JF bado ni kubwa zaidi na mipandikizi inajulikana kwa magamba yao. Enzi za huko nyuma ilikuwa inasemwa nusu ya WaTz walikuwa ni mashushushu. Wanafanyia ushushushu ile nusu iliyosalia. Gharama zote hizo ili kudumisha ulaji wa watu wachache tu? Ndiyo maana nchi nyingine huwezi kuwa kiongozi kama wewe ni njaa kali.
 
Nampa MIA kwa MIA kwani kule alipo NCCR aliyekuwa mbaya mnamjua na mvurugaji kwani Mrema ni KADA wa CCM na mimi ni Swahiba wangu nalijua hilo anayo kadi tokea TANU sasa ilipokuwa sasa huko TLP mnaona kunavyofukuta lakini angalia NCCR kwa Mabere Kimya. Msidanganyike na MAGAZETI ya BONGO noma kwa kuchafuliana kwani wakiandika ukweli watu hawanunui, MH.MABERE MARANDO MIMI NIPO NA WEWE BEGA KWA BEGA SAFI SANA LETE CHACHU KWA CHADEMA, HAO WALIOKOMENT AGAINST NA WEWE NI KADA WA SISIEMU. BIG UP MTU MZIMA
 
Nfikiri Watanzania tuna matatizo makubwa sana, kama kweli watu wanasema Marando asikubaliwe CHADEMA eti atakisambaratisha inanisikitisha sana. Inaoonyesha jinsi ambavyo watanzania waanamini katika personality (mtu) zaidi kuliko mfumo. Kama CHADEMA kitavurugwa na Marando asiye na uongozi wowote ndani ya Chama basi hicho chama chenyewe hakifai.

Kwa maana nyingine mashabiki wa CHADEMA mnaomhofia Marando mnatupa signal tusio wanachama wa CHADEMA kuwa chama chenu dhaifu sana ( fragile). Yaani mtu mmoja asambaratishe chama?. Mimi naona Marando ni rasimali kubwa sana kwa CHADEMA kulingana na jinsi mtakaavyomtumia. Mimi nadhani kuna watu hatari zaidi ndani ya CHADEMA kuliko Marando.

Nyerere alipokufa watanzania walikuwa wanasema nchi imekwisha nani atakemea viongozi, nani atafanya hivi, sijui vikao vya CCM vitakuwaje bila Nyerere etc. Hata leo utawasikia watu wanasema Nyerere angekuwepo haya yasingetokea. Mimi nasema wanaosema hivyo bila kujijua wanaonyesha jinsi gani Nyerere alikuwa na mapungufu, maana kiongozi mzuri ni yule anayejenga mfumo ambao hata yeye asipokuwepo mambo yanaenda bila shida.

CHADEMA nafikiri kina mfumo unaoshughulikia watu au matatizo yanotaka kukivuruga chama chao bila matatizo. Mfano ni jinsi walivyoshughulikia suala la Chacha Wangwe na ule mtafaruku wa Zitto Kabwe.

Hata kama kuna watu wana hofu na Marando, mpeni benefit of doubt, msimuhukumu kwa mambo ya 1996 ambayo leo tunaona kabisa kuwa chanzo alikuwa ni Mrema, maana kama watu wanavyosema mtu anaweza kujificha asijulikane kuwa ni mlozi, lakini anapokaribia kufa lazima itakuwa wazi tu.

Wiki ijayo CCM tutaanza ku off load wengine jiandaeni kuwapokea.....................................wengine ni vifaa ile mbaya maana hata Slaa tulimtema sasa tu(najuta)
 


Heshima kwako Luteni,

Mkuu hoja zako zimesimama kweli na zitaendelea kusimama kwasababu moja kubwa haujaweaka hata chembe moja ya unafiki.Mkuu kuna watu wanajaribu kuipotosha historia ya mageuzi hapa Tanzania kwasababu eti Mabere kahamia CHADEMA !.Nikikumbuka jinsi Marando alivyosaidiwa na dola Tanga ili uchaguzi usifanyike leo hii anaitwa mwanamageuzi nazidi kuwashangaa kama sio kustaajabu.Nikikumbuka vyama vyama vya upinzani vilikuwa na mgombea wao wa nafasi ya ubunge wa EA lakini Marando kwa msaada mkubwa wa CCM na dola alishinda ubunge nazidi kuwashangaa wanaomwona Mabere ni shujaa wa mageuzi.

Mabere Marando atabaki kuwa ni mtu hatari sana katika siasa za mageuzi hapa Tanzania hajalishi kama kaenda CHADEMA au karejea CCM.
 
Mhhh................kazi kweli kweli, lakini MMJ katusaidia kuwa yeye sio ajenti wa TISS. Labda yeye anaweza kujenga hoja vizuri kiasi cha kufanya hata dola au CCM (ubunge wa EAC) wamuunge mkono. Kuna sredi mmoja nilisema niliwahi kumuuliza Marando kama Mrema anatumiwa na CCM alikataa kabisa, alisema ila anweza kuwa anatumika bila yeye kujijua. Mimi namuamini Marando maana angeweza kumpakazia Mrema kuwa anatumika na CCM( bila shaka wakati huo hakujua). Kumbukeni vurugu za NCCR mageuzi zilikuwa baada ya uchaguzi wa 1995, kama Marando angetaka kumhujumu Mrema angefanya wakati huo, mbona alimuunga mkono kwa dhati?. Shida ilianza alipoambiwa akasome ili ajiandae kwa uchaguzi wa mwaka 2000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…