Nikiangalia thread hii,namkumbuka hakimu mmoja mhaya Mtakyamirwa,uyu dada yake aliolewa Uchagani na kuachika. Uyu mama akadhulumiwa mali zote na kurudi Bukoba,baadae maisha yake yakawa magumu akaamua amstaki mmewe ili wagawane mali,kuna nyumba ambayo uyu mama aliijenga moshi kwa ela yake akiwa na mume wake. Uyu mama akamwomba mtakyamirwa amtumie nauli aje dar kuanzisha kesi,kakake kamtumia na uyu mama akaja dar na alikuwa anakaa kwa kakake wakati wa kesi. Bahati mbaya au nzuri kesi ikapangiwa hakimu,hapa akapangwa kakake Mtakyamirwa. Kaka akamwita dadake wakati wa dinner,akamhoji kama ana ushaidi wa kutosha au kesi ifutwe wakaelewane nje. Kwa kujua kuwa kaka ndo kashika mpini dadake akagoma kuitoa kesi mahakamani. Kwa kufuata vifungu vya sheria,siku ya hukumu kaka mtu aliamuru kuwa mshitaki ameshindwa kuihaminisha mahakama na ivo yule Mchaga akashinda kesi. Kurudi nyumbani kila mtu alimshangaa bwn Hakimu kwa kumsaliti dadake,ila jamaa akawaeleza kuwa iyo ni sheria wala si hakimu,jamaa alimpa nauli dadake arudi bukoba kuendelea na maisha yake. Mwanzøni hata mi nlishutuka na nkaona bora kakake angejitoa kusikiliza kesi ila advocate mmoja maalufu dar alinitoa dukuduku kuwa inawezekana mwenye taaluma akasimamia haki bila dhuluma. Mkileta ya mabere marando naona yale yale inawezekana!