Mabibi na uleaji mbaya wa wajukuu

  • Thread starter Thread starter Deleted member 485868
  • Start date Start date
Basi bibi yangu alikua tofauti aisee, Bibi alikua anafinya yule daaaah no kudeka yani
Bibi yangu mzaa Mama nae yuko ivyo..hapendi ujinga..no madeko tofauti na bibi wa upande wa Baba

Ila ukakasi wake umesaidia kwakweli
 
Yaan ukitaka mtoto wako aharibike kwa madeko mpeleke kwa bibi yake,
Utashangaa kosa ambalo alikua anakupiga wewe ukilifanya wakati mdogo mjukuu akifanya anamtetea wala hamuadhibu.

Ila inatokana na ile kauli ya,
"Mtoto wa Watu" kumbuka wewe unamuona mwanao lakini yeye anamuangalia mumeo ndio maana wanasemaga mtoto wa watu.

Ila sio kwa mama yangu mie, wajukuu wakienda kumuona likizo wakirudi makwao heshima na adabu, hatakagi ujinga kabisaaaa.
 
Haha umenikumbusha mbali sana,mimi nilikua najuaga yule monkey ni jet le na yule kingurue ni samo hang
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mimi nilijuaga ndivyo walivyo vilevile yani sio kama sisi
 
Na ndivyo anavyofanya Mama angu..Bibi anadekeza huyu..kuna wakati mtoto anakosea ukitaka tu kuadhibu utasikia muache huyo bado mdogo aelewi kitu wakati kipindi niko umri wake nilikua napigika acha...na mjukuu alivyo na sifa utakuta anafanya kosa kusudi anakimbilia kwa Bibi anajua mtetezi yupo

Utakuta mnagombana kisa tu umemuadhibu mjukuu wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…