Ukiwa unatoka asubuhi kuelekea kwenye mihangaiko yako utaipenda mabibo ndani ya daladala,iwe ukiwa unaelekea makumbusho ,kariakoo au mnazi mmoja ndani ya daladala utakutana na watu wamependeza wastaharabu afu wananukia marashi mazuri , mabibo imekuwa nzuri na kitovu cha kuunganisha sehemu nyingi sana ,hii route naifananisha Na ile ya kutoka tegeta kupita mbezi beach kwenda Posta ndani ya daladala unaweza usitamani kushuka kabisa ,kwa masikitiko makubwa sasa imefika Muda wa kuhama mabibo na kuelekea uelekeo mwingine nitakukumbuka sana mabibo,tumekuwa wote kwa miaka mitano sasa ni Muda wa kusaka maisha sehemu nyingine