Mabibo,Manzese,Mburahati : Kisima cha mabondia nchini Tanzania

Mabibo,Manzese,Mburahati : Kisima cha mabondia nchini Tanzania

Lady Mwali

Senior Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
147
Reaction score
333
Nimefanya uchunguzi na kugundua maeneo hayo tajwa yamesheni mabondia chipukizi waliofufua mchezo wa ngumi kupitia Azam Tv inayoonesha mapambano ya ngumi moja kwa moja chini ya promota Selemani Semunyu.

Vijana wengi wanaocheza mchezo wa ngumi wamepata mafanikio makubwa katika mchezo huu hasa ktk maeneo tajwa.

Huwezi kutaja mafanikio ya ngumi bila kutaja kocha Baba Mzazi aliyezalisha mabondia wengi kama Nasibu Ramadhani anayewakilisha nchi yetu nje ya nchi kimataifa.

Vile vile kuna huyu kocha Rama Jah wa Naccoz anayefundisha mabondia zaidi ya 100 kutoka team Naccoz,kwa uchache kuna
mabondia maarufu kama Ali
Kasusu,Mfaume Mfaume (ame-
wakilisha nchi yetu kimataifa ktk nchi mbalimbali kama Urusi,
Ujerumani,Uingereza nk,vilevile
ameshiriki mapambano mengi ya ndani,kuna bondia mwingine
anaitwa Halima Vunjabei naye
amefanya vizuri katika ngumu kitaifa na kimataifa.

Mabondia wengine chipukizi ni Oscar Richard ambaye amewaki
lisha taifa letu kimataifa bila ya
kumsahau Adam Yahaya anaye-
pigana kimataifa.

Imefika wakati mbunge wa Ubungo kuwa karibu na mabondia hawa kwani wame-
kosa sapoti kutoka serikali na mbunge wao kupitia C.C.M.
Nasikia mbunge huyo ndugu Kitilya Mkumbo alionekana katika Gym ya Naccoz iliyopo Mabibo ktk kipindi cha kampeni
ya uchaguzi mkuu, alionekana akiongea na viongozi wa mabo-
ndia akiomba kura, baada ya ku-
shinda uchaguzi akawakimbia.
 
Ukiangalia maisha ya watu wanaoishi hizo sehemu utajua kwanini wanapenda sana Boxing.

Boxing is not a sport to them its a lifestyle. Wanapenda kubondana balaa
 
Back
Top Bottom