RESOLVED Mabibo Sokoni (Dar): Mitaro iliyokuwa imeziba kwa taka yaanza kuzibuliwa

RESOLVED Mabibo Sokoni (Dar): Mitaro iliyokuwa imeziba kwa taka yaanza kuzibuliwa

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Nimepita katika eneo la Mabibo Sokoni, ambako awali kuliripotiwa kuwepo kwa mitaro iliyokuwa imejaa majitaka na kuziba kutokana na mrundikano wa taka. Katika kufuatilia nimebaini kuwa wahusika wameanza kuchukua hatua za kuzibua mitaro hiyo.

Mitaro hiyo ilikuwa kero kubwa kwa wananchi, hususan wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo hilo, kutokana na kujazwa na majitaka yaliyokuwa yakitoa harufu mbaya na kusababisha usumbufu kwa watu wanaopita na kufanya shughuli zao katika eneo hilo.

Hoja ya awali hii hapa ~ Mifereji ya maji taka Mabibo Sokoni (Dar) iboreshwe
Nimeshuhudia zoezi la kuzibua mitaro hiyo likiendelea kwa siku ya pili mfululizo. Nawapongeza wahusika kwa kuchukua hatua hiyo, licha ya kwamba utekelezaji wake umechelewa.

Hata hivyo, kutokana na nilichokishuhudia, napenda kutoa wito kwa mamlaka zinazohusika na zoezi hilo la usafi kuhakikisha kuwa taka zinazotolewa kwenye mitaro hiyo haziachwi pembezoni mwa barabara, bali zinakusanywa na kuondolewa mara moja.
photo_2026-10-30_15-50-23.jpg
photo_2026-10-30_15-50-26.jpg
photo_2026-10-30_15-50-42.jpg
Hii ni kwa sababu taka hizo zinapoachwa bila kuondolewa huendelea kuwa kero kwa wananchi, kwani hurundikana pembezoni mwa barabara na kuhatarisha usafi wa mazingira. Vilevile, mvua zinaponyesha, kuna uwezekano taka hizo kusombwa na maji na kuziba tena mitaro iliyokuwa imeshafunguliwa.\

Ni muhimu zoezi hili likakamilishwa kwa kuhakikisha kuwa si mitaro pekee inayozibuliwa, bali taka zote zinazotolewa zinaondolewa ili kuepusha tatizo hilo kujirudia.
photo_2026-10-30_15-51-05.jpg
 
Back
Top Bottom