Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

The Future.

Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
71
Reaction score
0
habari za kazi ndugu zangu wana jf?kwakweli nimepatwa na msongamano mkubwa wa mawazo amabyo mimi binafsi nimeshindwa kufanya maamuzi sahihi hivyo basi nimeona nilete matatizo yangu hapa jamvini kwani nina imani kubwa nitasaidiwa kimawazo kupata ufumbuzi wa mikasa hii nilionayo kwasasa.

mimi ni mtanzania mwenzenu ninaeishi kigali Rwanda, baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, huko nje nilirudi africa na pia baada ya mambo kutoniendea vizuri hapo Dar, ndipo nikapatwa na wazo la kuja Rwanda kutafuta ajira kiukweli namshukuru mungu nikafanikiwa kupata kazi, sababu mojawapo ya kuja rwanda nikwamba mama yangu mzazi ana asili ya huku na wazazi wake walikimbilia Tz mwaka 1959 wakati wa genocide ya mwaka 1959.

Ndugu mwaka jana nilipata bahati ya kukutana na binti mmoja wa kinyarwanda amabe nilivutiwa na e na hivyo sikusita kumwambia kua nimempenda ambae kwa upande wake ilikua vigumu kukubali hivyo basi nikamuomba namba ya simu akasema haa sim nimuomba basi nimnunulie sim aka kataa na kudai kuwa anaogopa wazazi wake wakimuuliza ameitoa wapi hatokua na jibu sahihi, nikampa busness card yangu na kumuomba tuwasiliane kama akipata simu baada ya miezi mi3 alinipigia na kuniambia tayari ameisha pata simu ila hayupo tayari kuwa mpenzi wangu bali tunaweza kua marafiki wa kawaida baada ya hapo akawa ananiomba nimpatie bongo movies kwani anazipenda sana na kwao wote wanaona filam za tz, baada ya muda flan akaniambia kuwa yupo tayari kua mpenzi wangu, kiukweli nilifurahi sana. then akaniambia kuna mtu anahitaji kuongea na mimi hivyo atanipigia sim, hazikupita siku 3, shangazi yake akanipigia simu na kunialika lunch nyumbani kwake, baada ya kwenda nilikaribishwa vizuri sana kwani mama huyo anajua kiswahili vizuri na hua anakuja tz kibiashara, then akaniambia sababu kuu ya kuniita kwake nikutaka tujadili kuhusu huyo binti, aliniuliza mara kadhaa kama kweli nampenda au nina nia nyingine nikamwambia kiukweli nampenda sana then akaniambia binti huyo ni yatima na wazazi wake wote pamoja na dada na kaka zake waliuawa wakati wa genocide, na hivyo kama kweli nampenda nihakikishe simuumizi kwani yaliomkuta ni makubwa katika maisha yake na pia yeye mwenyewe kamthibitishia kua ananipenda sana, kiukweli nilikubali na baada ya siku chache nikampeleka kwa babu yangu mdogo wake na baba wa mama yangu ambae ni mnyarwanda na kumtambulisha rasm, woote walimpenda sana na kutushauri kua makini na pia hasa mimi ambae ni mkubwa kua nimuongoze vizuri kimasomo na akimaliza shule tuangalie ustarabu mwingine.
tumekua na utamaduni wa kutembeleana na nimekua nikimsapoti mahitahji ya shuleni na siku moja alikuja kwangu jioni then nikahitaji kufanya nae mapenzi akakataa na kudai anaogopa na hajawahi hata siku moja na aliponiona nimekua disapointed ikabidi akubali na kudai kua hapendi kuniudhi ila tutumie condom, kiukweli baada ya kujaribu nikagundua kua ni bikra, nilifurahi na nikaamini kua ni binti muaminifu ikabidi niachane na wazo la kufanya mapenzi na matokeo yake nikampa zawadi na ku promise sintohitaji tena mpaka atakapokua tayari,
mambo yanaenda vizuri na hatukutani mara nyingi kwani nakua bize sana na kazi,

Upande wa pili wa story ni kwamba siku moja tulikua semina katika moja ya hoteli zilizopo remera hotel tek, hapo tulikutana watu wa makampuni mbalimbali ndipo dada mmoja mtoa mada mrembo na nilivutiwa na mitazamo yake na kwa bahati wakati wa lunch tulijikuta meza moja na katika hali ya kutaka kufahamiana ndio tukapeana facebook adress na namba za simu, kiukweli mwanzo tulikua tunashauriana mambo mbalimbali hasa jinsi ya kuandaa report kwa kiingereza za kampuni yao kwani yeye ni managing director, siku moja alini alika dinna kwake, theni tukaongea sana na mimi nikamualika lunch kwangu weekend iliofuatia, baada ya hapo tukawa tunapigiana simu mara kwa mara na siku moja aliniita gafla akidai kua ana tatizo na pia anaamini nitaweza kumsaidia ufumbuzi, nilipofika kwake ndio akanisimulia story yoote ya maisha yake na pia wazazi wake pamoja na kaka zake wa5 wealiuawa kwenye genocide na yeye alisalimika kimiujiza na pia amelelewa na mama yake mkubwa kiukweli alipata shida sana mpaka alipomaliza degree yake ya saikolojia na ushauri na akaapa maisha yake yoote atafanya kazi za kusaidia yatima, na pia imemchukua muda merfu kufikiri ni nani atakaemfaa kua mme wake na amekua akiwakataa wachumba wengi hasa wanyarwandaukizingatia kifedha na kielimu anajiweza na anaogopa kuishi na mtu ambae atakua na maslahi binafsi pia akaniambia anaipenda sana tz na wa tz pamoja na tamaduni zetu kwani tunapenda amani na pia ni watu wazuri, then akaniambia kama nipo tayari na kama ninahitaji mke yupo tayari muda woote tufunge ndoa na ahitaji chochote kutoka kwangu zaidi ya mapenzi ya kweli, nilishikwa na butwaa kisha akaniambia kua yeye ni bikra na haja wahi kulala na mwanamme na pia x boy friend wake walishindana kwakua alikua anahitaji sex badala ya kujadili mipango ya ndoa, nikamuuliza swali kua ana uhakika gani kama mimi ndio chaguo lake sahihi? akasema amenichunguza kwa muda mrefu na sasa anaamini mimi ndie mwanaume aliekua anamsubiri muda woote.
kiukweli mimi kiumri nina miaka 29 na yeye ana miaka 31 ila anaonekana mdogo na aliponiambia miaka yake siku amini mpaka aliponionyesha vitambulisho vyake, nikamuomba anipe muda nifikirie then tamjibu next time tukionana, ki ukweli nihitaji kumwambia haiwezekani kwani tayari nina mtu mwingine, nilipo mpigia simu kumwambia hivyo alilia sana na matokeo yake kesho yake nikapigiwa simu kutoka hospita kua amelazwa hospital na Dr anahitaji kuongea na mimi, nilishikwa na butwaa then nikakimbia hospital na hali niliomkuta nayo niliona huruma sana Dr akaniambia anasumbuliwa na msongamano wa mawazo na chanzo ni mimi kwani inaonekana kauli yangu ya kumwambia haiwezekani kumuuoa ndio ilio sababisha madhara yoote na pia ni muhanga wa genocide kuna uwezekano mkubwa kumbukumbu mbaya za wazazi wake zikamrudia kama nisipokua tayari kumfurahisha na kua karibu nae.

Ndugu zangu nilihisi kuchanganyikiwa na mwisho wake nikamwambia Dr hakuna tatizo takua karibu nae na baada ya siku 3 aliruhusiwa kurudi nyumbani kwake.
nimekua karibu nae sana na pia amekua na furaha muda wote ninapokua nae.

Sasa jana usiku mida ya saa 5, nilimpigia simu yule girl friend wangu kumtakia usiku mwema then nikashangaa kumsikia akiwa mchangamfu mida hiyo wakati nilitarajia kua atakua kitandani, then akaniambia yupo sebuleni peke yake na wote wamelala ila yeye anaona mpira kwani ni fan wa Manchester united, kiukweli sikuamini na nikapata mshangao mkubwa kwani hata mimi mwenyewe ni fan mkubwa wa football na club ni chelsea ili kutaka kujua zaidi nikamuomba anitajie wachezaji wa man u anaowahusudu ndio akanitajia berbetov, chicharito, nani pamoja na rooney, nilifurahi sana kuona tunahobie zinazo fanana, ndio nikapata wazo la kumuuliza kuhusu birth day yake ni lini hapo ndio nikachanganyikiwa kabisa kazaliwa tareh 18 mwezi wa 8 na hiyo ndio tarehe niliozaliwa, kiukweli sikuamini mpaka leo nimemfuata shule ili nione kitambulisho chake na ku prove ni kweli then nikamuonesha passprt yangu nayeye akazidi kushangaa, nashindwa kuelewa kwanini mambo yoote haya yananitokea tena ndani ya muda mfupi.
Ndugu zangu kwa heshima na taadhima naombeni ushauri wenu nifanyeje? ki ukweli nampenda sana huyu binti wa kwanza na pia sijui nitumie njia gani kumueleza huyu wa pili ili anielewe.

karibuni sana nahitaji michango yenu.
 
Dou!!! very touching story, ndugu yangu jambo lako linahitaji busara zaidi kuliko akili yetu ya kawaida ya kibinadaamu, kwanza kabisa ulikuwa tayari na uhusiano na msichana ambae mwenyewe ulimpenda kwa moyo mmoja mpaka alipokuwa tayari kuwa na wewe nakushauri uendelee nae huyo, huwezi jua huyo dada mwingine anakuhitaji umuoe sababu tu umri umekwenda. Ni bora umemwambia ukweli mapema. nakushauri endelea na yule wa kwanza kama mapenzi yako yako kwako na huyo mwingine mweleze tena akuelewe mbaki na uhusiano wa urafiki tu.
Pili haya mambo ya bikira yapo sana huko rwanda nilishasikia sijui wanafanya vitu gani inarudi na unahisi ni bikira kabisa kwa hiyo hilo swala lisikupe kichwa kabisa ingawaje linaweza kuwa ya kweli vilevile. mwisho kabisa mshirikishe mungu jitolee ufunge kwa maombi japo siku tatu mungu atakufungulua njia.mambo mengine hatuwezi kuyatambua kwa akili zetu za kibinadamu
 
ni ndefu mimi nimeishia katikati ntamalizia kesho.............
 
mimi ni mtanzania mwenzenu ninaeishi kigali Rwanda, baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, huko nje nilirudi africa na pia baada ya mambo kutoniendea vizuri hapo Dar, ndipo nikapatwa na wazo la kuja Rwanda kutafuta ajira kiukweli namshukuru mungu nikafanikiwa kupata kazi, sababu mojawapo ya kuja rwanda nikwamba mama yangu mzazi ana asili ya huku na wazazi wake walikimbilia Tz mwaka 1959 wakati wa genocide ya mwaka 1959.


Hiyo bluu sina kumbukumbu sana umesema huyo binti wa kwanza na wa pili wazazi wao walifariki wakati huo au??
 
Kwanza nimeshangaa kua muda wote ulikua hujui hobby za mpenzi wako pamoja na tarehe yake ya kuzaliwa!Newayz baki na huyo wa kwanza maana hapo ndipo moyo wako ulipo!Ukimkubalia huyo wa pili utakua unamuoa kwa huruma...bahati yako nzuri leo kuna mdau alianzisha thread inayohusu kumuoa/kuolewa na mtu kwa huruma!www.jamiiforums.com/mahusiano-mapen...uoneana-huruma-is-it-right-2.html#post1663047 pita hapo uone maoni ya wadau!Hopefully utapata muongozo kidogo!
 
Busara zaidi ndio inahitajika hapo mkuu.... huyu mwenye maisha yake at least anapakushika!!!!:A S 13:
 
kwa ufupi nakushauri ukae chini sali novena kama ww ni mkristo Mungu atakuonyesha ni yupi.ila kwa ufahamu wangu natumaini wa kwanza ndio Mungu aliokujalia huyo wa pili ni kama umewaka tamaa na unakaa nae karibu kwa kuogopa asijidhuru au kuchanganyikiwa.Kweli hizo figa ni nzuri nimekaa kigoma nimewaona hao watu si wa kawaida. Kuwa makini wasije kukua kama ukiwatenda
 
...natamani kukwambia ucheze 'sandakarawe, amina..mwenye kupata, apate!'

Anyway, la msingi unahitaji space baina ya wote wawili.
fikiria nini unachohitaji maishani, mfano;

Unahitaji mke wa aina gani, unayempenda/anayekupenda/mnayependana au? tabia zake, urembo wake, etc
unahitaji familia ya aina gani, ki imani, maadili, etc
unahitaji maisha ya aina gani, hali ya kawaida, hali ya kati, hali ya juu, etc

kisha oanisha majibu yako kulingana na sifa za hao wawili.
Don't rush into conclusion bana, NDOA ni kifungo cha maisha kaka.

Ukishapata jibu utuambie wanafamilia wenzio wa JamiiForums,
kuna Bachelors wanaguswa na hadithi kama yako.
 
Hi stori kama ya dayz of our lives.....billy, bo, hope, sammi, lucas, austin etc
 
Wewe ni muislamu au mkristo?oa wote wake 2 ruksa kama wewe ni muislamu
 
oa yeyote kwa sababu anaolewa mwanamke na sio inaolewa bikira.
 
duh!! kama vile hadithi za shigongo!! je itaendeleaje? songa nayoo
 
Hi stori kama ya dayz of our lives.....billy, bo, hope, sammi, lucas, austin etc

Umenikumbusha mbali sana halafu mtu anakufa halafu season nyingine eti anafufuka, bila kusaha amnesia du wanatudanganya sana hawa
 
nimeguswa sana na story yako ila kumbuka huruma yako haitakusaidia kuwa na wote mwisho wa siku mmoja atafurahi na mwingine kuhuzunika. binafsi nadhani upo zaidi kwa huyo binti wa kwanza anayesoma na natumaini kwa shule yupo level ambayo mkipanga kuoana inawezekana. dhumuni langu ni wewe ubaki na uliye nae na huyo mwingine mwisho wa siku atakuelewa kuumwa si kigezo kikubwa kwani ikiwa leo umetangulia mbele ya haki kwake itakuwaje? {samahani kwa mfaano ila najaka ufahamu kuwa mwisho wa siku atazoea tu}
 
Shost na Suzy mie niliona tangu mwanzo mwaka wa wazazi kukimbia na wengine kufa nilishapata wasiwasi na huo umri wa mabinti. Na thanx nimewagongea
 
Fuata moyo wako kaka yangu,kwani unampenda huyu wa kwanza na kuhusu wa pili usitake kumuonea huruma mtu kwenye suala la kuja kuishi pamoja si mzaha hata kidogo.
na kumbuka ulishamuaahidi wa kwanza hutamuumiza hivyo umuumize kwasababu ya kuogopa kumuumiza aliyemkuta mwenzake la msingi ni kuwa na msimamo haijalishi ni chenza au chungwa.
ulishaenda kumtambulisha wa kwanza kwa baadhi ya jamaa na kuhojiwa ukahojiwa na kujibu ndiyo utafanya hivyo naamini kwa msaada wa Mungu sasa leo uibuke tena sababu macho yako yamemuona mwingine na kuufanya moyo wako kutokujiamini
si mwenyeji wa Rwanda lakini naamini familia nyingi zimepata matatizo yakupoteza ndugu na jamaa katika mauaji ya kimbari.
huyo dada mwingine atakapopata nafuu kabisa mueleze msimamo wako na ulipofikia kwani mwanaume anayemtaka si wewe tu na asitumie kigezo cha kwamba watampenda sababu ya alicho nacho la msingi asiviweke hivyo kama kipaumbele kwake na atakayekuja atakuwa ameviona hivyo.
kwa suala la umri sina shida saana kuwa angekuwa yeye ndiyo wa kwanza halafu kakupita umri,siyo sababu kubwa saana.
kuna mambo ya msingi ya kuzingatia katika mahusiano kwani hata kwa wanaume ambao wamewazidi wanawake umri lakini hawana amani,upendo wa dhati namaendeleo kama familia.
Huo ni mchango wangu kwasasa nitaendelea kuchangia tena kila lakheri kaka
 
Back
Top Bottom