Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

kaka lete kwetu pia tuuzie ..... ila watamu kama wabongo we si umeshatest vyote
 
Ndugu zangu napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru saaana, woote kwa ushauri wenu na maoni yenu mbalimbali, pia vilevile naomba niwajulishe ya kwamba mimi sio muandishi wa hadithi na pia hii ni mara yangu ya kwanza kuja katika jukwaa hili na kutaka msaada kutoka kwenu. wanajamvi habari hii ni ya kweli kabisa ila sina njia ya kumuaminisha kila mtu, ila kama kunayoyote atahitaji uhakika zaidi hii namba yangu ya simu+250722344064,

nipo tayari kupokea ushauri wowote na kuufanyia kazi na yeyote atakae ni sms nitamjibu haraka,
mwisho kabisa napenda kutoa msimamo wangu kama ifuatavyo.....baada ya kusoma ushauri kutoka kwenu kwa kina na pia baada ya kushauriana na baadhi ya rafiki zangu mbalimbali waliopo nchi tofauti wengi wamenishauri niamue kuwa na wa kwanza kwani ndio chagua langu.
hivyo basi nimeamua kubaki wa kwanza na pia kwa vile tumezaliwa mwezi na tareh moja basi hata ndoa yetu tutafunga siku ya kusherehekea birthday yetu kwa pamoja. naahidi kuendelea kuawajuza muendelezo wa hadithi hii ya maisha yangu na Mungu akipenda baada ya kufunga ndoa tutakwenda honeymoon Zanznibar hivyo naamini naweza pata nafasi ya kuonana na wanajamvi mbalimbali waliojitolea kunishauri,

Asante sana sina cha kuwalipa ila nawaombea kwa Mungu heri na baraka, kazi njema na maisha mema ndugu zangu.
 
habari za kazi ndugu zangu wana jf?kwakweli nimepatwa na msongamano mkubwa wa mawazo amabyo mimi binafsi nimeshindwa kufanya maamuzi sahihi hivyo basi nimeona nilete matatizo yangu hapa jamvini kwani nina imani kubwa nitasaidiwa kimawazo kupata ufumbuzi wa mikasa hii nilionayo kwasasa.

mimi ni mtanzania mwenzenu ninaeishi kigali Rwanda, baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, huko nje nilirudi africa na pia baada ya mambo kutoniendea vizuri hapo Dar, ndipo nikapatwa na wazo la kuja Rwanda kutafuta ajira kiukweli namshukuru mungu nikafanikiwa kupata kazi, sababu mojawapo ya kuja rwanda nikwamba mama yangu mzazi ana asili ya huku na wazazi wake walikimbilia Tz mwaka 1959 wakati wa genocide ya mwaka 1959.

Ndugu mwaka jana nilipata bahati ya kukutana na binti mmoja wa kinyarwanda amabe nilivutiwa na e na hivyo sikusita kumwambia kua nimempenda ambae kwa upande wake ilikua vigumu kukubali hivyo basi nikamuomba namba ya simu akasema haa sim nimuomba basi nimnunulie sim aka kataa na kudai kuwa anaogopa wazazi wake wakimuuliza ameitoa wapi hatokua na jibu sahihi, nikampa busness card yangu na kumuomba tuwasiliane kama akipata simu baada ya miezi mi3 alinipigia na kuniambia tayari ameisha pata simu ila hayupo tayari kuwa mpenzi wangu bali tunaweza kua marafiki wa kawaida baada ya hapo akawa ananiomba nimpatie bongo movies kwani anazipenda sana na kwao wote wanaona filam za tz, baada ya muda flan akaniambia kuwa yupo tayari kua mpenzi wangu, kiukweli nilifurahi sana. then akaniambia kuna mtu anahitaji kuongea na mimi hivyo atanipigia sim, hazikupita siku 3, shangazi yake akanipigia simu na kunialika lunch nyumbani kwake, baada ya kwenda nilikaribishwa vizuri sana kwani mama huyo anajua kiswahili vizuri na hua anakuja tz kibiashara, then akaniambia sababu kuu ya kuniita kwake nikutaka tujadili kuhusu huyo binti, aliniuliza mara kadhaa kama kweli nampenda au nina nia nyingine nikamwambia kiukweli nampenda sana then akaniambia binti huyo ni yatima na wazazi wake wote pamoja na dada na kaka zake waliuawa wakati wa genocide, na hivyo kama kweli nampenda nihakikishe simuumizi kwani yaliomkuta ni makubwa katika maisha yake na pia yeye mwenyewe kamthibitishia kua ananipenda sana, kiukweli nilikubali na baada ya siku chache nikampeleka kwa babu yangu mdogo wake na baba wa mama yangu ambae ni mnyarwanda na kumtambulisha rasm, woote walimpenda sana na kutushauri kua makini na pia hasa mimi ambae ni mkubwa kua nimuongoze vizuri kimasomo na akimaliza shule tuangalie ustarabu mwingine.
tumekua na utamaduni wa kutembeleana na nimekua nikimsapoti mahitahji ya shuleni na siku moja alikuja kwangu jioni then nikahitaji kufanya nae mapenzi akakataa na kudai anaogopa na hajawahi hata siku moja na aliponiona nimekua disapointed ikabidi akubali na kudai kua hapendi kuniudhi ila tutumie condom, kiukweli baada ya kujaribu nikagundua kua ni bikra, nilifurahi na nikaamini kua ni binti muaminifu ikabidi niachane na wazo la kufanya mapenzi na matokeo yake nikampa zawadi na ku promise sintohitaji tena mpaka atakapokua tayari,
mambo yanaenda vizuri na hatukutani mara nyingi kwani nakua bize sana na kazi,

Upande wa pili wa story ni kwamba siku moja tulikua semina katika moja ya hoteli zilizopo remera hotel tek, hapo tulikutana watu wa makampuni mbalimbali ndipo dada mmoja mtoa mada mrembo na nilivutiwa na mitazamo yake na kwa bahati wakati wa lunch tulijikuta meza moja na katika hali ya kutaka kufahamiana ndio tukapeana facebook adress na namba za simu, kiukweli mwanzo tulikua tunashauriana mambo mbalimbali hasa jinsi ya kuandaa report kwa kiingereza za kampuni yao kwani yeye ni managing director, siku moja alini alika dinna kwake, theni tukaongea sana na mimi nikamualika lunch kwangu weekend iliofuatia, baada ya hapo tukawa tunapigiana simu mara kwa mara na siku moja aliniita gafla akidai kua ana tatizo na pia anaamini nitaweza kumsaidia ufumbuzi, nilipofika kwake ndio akanisimulia story yoote ya maisha yake na pia wazazi wake pamoja na kaka zake wa5 wealiuawa kwenye genocide na yeye alisalimika kimiujiza na pia amelelewa na mama yake mkubwa kiukweli alipata shida sana mpaka alipomaliza degree yake ya saikolojia na ushauri na akaapa maisha yake yoote atafanya kazi za kusaidia yatima, na pia imemchukua muda merfu kufikiri ni nani atakaemfaa kua mme wake na amekua akiwakataa wachumba wengi hasa wanyarwandaukizingatia kifedha na kielimu anajiweza na anaogopa kuishi na mtu ambae atakua na maslahi binafsi pia akaniambia anaipenda sana tz na wa tz pamoja na tamaduni zetu kwani tunapenda amani na pia ni watu wazuri, then akaniambia kama nipo tayari na kama ninahitaji mke yupo tayari muda woote tufunge ndoa na ahitaji chochote kutoka kwangu zaidi ya mapenzi ya kweli, nilishikwa na butwaa kisha akaniambia kua yeye ni bikra na haja wahi kulala na mwanamme na pia x boy friend wake walishindana kwakua alikua anahitaji sex badala ya kujadili mipango ya ndoa, nikamuuliza swali kua ana uhakika gani kama mimi ndio chaguo lake sahihi? akasema amenichunguza kwa muda mrefu na sasa anaamini mimi ndie mwanaume aliekua anamsubiri muda woote.
kiukweli mimi kiumri nina miaka 29 na yeye ana miaka 31 ila anaonekana mdogo na aliponiambia miaka yake siku amini mpaka aliponionyesha vitambulisho vyake, nikamuomba anipe muda nifikirie then tamjibu next time tukionana, ki ukweli nihitaji kumwambia haiwezekani kwani tayari nina mtu mwingine, nilipo mpigia simu kumwambia hivyo alilia sana na matokeo yake kesho yake nikapigiwa simu kutoka hospita kua amelazwa hospital na Dr anahitaji kuongea na mimi, nilishikwa na butwaa then nikakimbia hospital na hali niliomkuta nayo niliona huruma sana Dr akaniambia anasumbuliwa na msongamano wa mawazo na chanzo ni mimi kwani inaonekana kauli yangu ya kumwambia haiwezekani kumuuoa ndio ilio sababisha madhara yoote na pia ni muhanga wa genocide kuna uwezekano mkubwa kumbukumbu mbaya za wazazi wake zikamrudia kama nisipokua tayari kumfurahisha na kua karibu nae.

Ndugu zangu nilihisi kuchanganyikiwa na mwisho wake nikamwambia Dr hakuna tatizo takua karibu nae na baada ya siku 3 aliruhusiwa kurudi nyumbani kwake.
nimekua karibu nae sana na pia amekua na furaha muda wote ninapokua nae.

Sasa jana usiku mida ya saa 5, nilimpigia simu yule girl friend wangu kumtakia usiku mwema then nikashangaa kumsikia akiwa mchangamfu mida hiyo wakati nilitarajia kua atakua kitandani, then akaniambia yupo sebuleni peke yake na wote wamelala ila yeye anaona mpira kwani ni fan wa Manchester united, kiukweli sikuamini na nikapata mshangao mkubwa kwani hata mimi mwenyewe ni fan mkubwa wa football na club ni chelsea ili kutaka kujua zaidi nikamuomba anitajie wachezaji wa man u anaowahusudu ndio akanitajia berbetov, chicharito, nani pamoja na rooney, nilifurahi sana kuona tunahobie zinazo fanana, ndio nikapata wazo la kumuuliza kuhusu birth day yake ni lini hapo ndio nikachanganyikiwa kabisa kazaliwa tareh 18 mwezi wa 8 na hiyo ndio tarehe niliozaliwa, kiukweli sikuamini mpaka leo nimemfuata shule ili nione kitambulisho chake na ku prove ni kweli then nikamuonesha passprt yangu nayeye akazidi kushangaa, nashindwa kuelewa kwanini mambo yoote haya yananitokea tena ndani ya muda mfupi.
Ndugu zangu kwa heshima na taadhima naombeni ushauri wenu nifanyeje? ki ukweli nampenda sana huyu binti wa kwanza na pia sijui nitumie njia gani kumueleza huyu wa pili ili anielewe.

karibuni sana nahitaji michango yenu.

mkuu kwanza pole sana maana nimejaribu kuvaa viatu vyako nimeona jinsi vinavyobana.ila kwa upande mwingine hongera sana maana wote waliokuzunguka wanavigezo vya kuwa mke mwema.cha msingi kaa chini then shirikisha halmashauri zako zote za kichwa pamoja na moyo ikiwezekana na roho pia ninahakika utapata ufumbuzi wa yupi anaekufaa zaidi kutokana na vigezo vya mwanamke unaemtaka kua nae maishana.it is only you who can provide the right answer for this riddle
 
....:rain:very interesting jamani. kuoa ni try and error tu. jifunze kutojibu " no " sikuzote, kuna professional No na sio direct "no" kiivyo bana. oa wa kwanza wapili ukiendelea kumliwaza nae utampotezea muda kazi ipo hapo.......fuata hisia
 
Tulia na huyo wa kwanza nadhani ndiyo chaguo halisi.
 
Good story but confusing a bit!!! Mmoja wazazi wake walikufa kwenye Rwandan Genocide of 1959 lakini umri wake ni miaka 31 hadi sasa!!!!!! Pamenichanganya mno hapa..... Hebu pafafanue mkuu...unless kama ulimaanisha ile Rwandan Genocide ya 1994 hapo utakuwa consistent.
 
Oyaaaa mzee wa bikra vipi mwendelezo
 
icon1.png
Re: Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

Good story but confusing a bit!!! Mmoja wazazi wake walikufa kwenye Rwandan Genocide of 1959 lakini umri wake ni miaka 31 hadi sasa!!!!!! Pamenichanganya mno hapa..... Hebu pafafanue mkuu...unless kama ulimaanisha ile Rwandan Genocide ya 1994 hapo utakuwa consistent.

hardwood sory mkuu usichanganye maelezo walioondoka wakati wa genocide ya 1959 ni mama yangu na wazazi wake ambao walikimbilia Tz, ila hao akina dada wazazi wao waliuawa mwaka 1994 wakati wa genocide ambayo intarahamwe chini ya rais habyarimana waliazimi kulitokomeza kabila la kitutsi. nadhani umenisoma ndugu yangu
 
Gaga nadhani hakuna muendelezo zaidi ya maelezo haya ambayo niliyatoa asubuhi

Ndugu zangu napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru saaana, woote kwa ushauri wenu na maoni yenu mbalimbali, pia vilevile naomba niwajulishe ya kwamba mimi sio muandishi wa hadithi na pia hii ni mara yangu ya kwanza kuja katika jukwaa hili na kutaka msaada kutoka kwenu. wanajamvi habari hii ni ya kweli kabisa ila sina njia ya kumuaminisha kila mtu, ila kama kunayoyote atahitaji uhakika zaidi hii namba yangu ya simu+250722344064,

nipo tayari kupokea ushauri wowote na kuufanyia kazi na yeyote atakae ni sms nitamjibu haraka,

mwisho kabisa napenda kutoa msimamo wangu kama ifuatavyo.....baada ya kusoma ushauri kutoka kwenu kwa kina na pia baada ya kushauriana na baadhi ya rafiki zangu mbalimbali waliopo nchi tofauti wengi wamenishauri niamue kuwa na wa kwanza kwani ndio chagua langu.
hivyo basi nimeamua kubaki wa kwanza na pia kwa vile tumezaliwa mwezi na tareh moja basi hata ndoa yetu tutafunga siku ya kusherehekea birthday yetu kwa pamoja. naahidi kuendelea kuawajuza muendelezo wa hadithi hii ya maisha yangu na Mungu akipenda baada ya kufunga ndoa tutakwenda honeymoon Zanznibar hivyo naamini naweza pata nafasi ya kuonana na wanajamvi mbalimbali waliojitolea kunishauri,

Asante sana sina cha kuwalipa ila nawaombea kwa Mungu heri na baraka, kazi njema na maisha mema ndugu zangu.
 
Niekusoma ndugu. Yaelekea huko Rwanda kunahitajika watanzania wengi vijana kwa kazi moja muhimu ya kuwafariji mabinti wa huko ambao wengi wao ni wahanga wa yale mauaji ya halaiki. Pili, naweza kuona dhahiri kabisa desperation ya huyu dada wa pili. Nothing simple u can do to avoid her. Utaingia gharama kidogo (yoyote ile) hadi akuelewe kuwa hutanii. Nadhani sasa hivi unawaza na kusema I wish tusingekutana

Muweke tu wazi kuwa tayari una mwenza. Mpe na vielelezo. Hali aliyo nayo japo ni ya muda, ni hatari. Itapita. Tumia akili na uzoefu wako kwenda nae hadi atakielea. Cha msingi huna kosa lolote katika kutokuwa naye
 
icon1.png
Re: Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

Niekusoma ndugu. Yaelekea huko Rwanda kunahitajika watanzania wengi vijana kwa kazi moja muhimu ya kuwafariji mabinti wa huko ambao wengi wao ni wahanga wa yale mauaji ya halaiki. Pili, naweza kuona dhahiri kabisa desperation ya huyu dada wa pili. Nothing simple u can do to avoid her. Utaingia gharama kidogo (yoyote ile) hadi akuelewe kuwa hutanii. Nadhani sasa hivi unawaza na kusema I wish tusingekutana

Muweke tu wazi kuwa tayari una mwenza. Mpe na vielelezo. Hali aliyo nayo japo ni ya muda, ni hatari. Itapita. Tumia akili na uzoefu wako kwenda nae hadi atakielea. Cha msingi huna kosa lolote katika kutokuwa naye

Raia fulani nimekusoma kaka, you are in my mind jhata mimi nafikiri the same, hata leo kanipigia sim mara 6 akihitaji tuonane nnimetoa excuse kadhaa na ameelewa, ila bado naamini nahitaji busara zaidi kumbadilisha kifikra ila naamini kwa nguvu za Mungu mambo yatakaa sawa, kweli sometimes najuta kwanini nilikutana nae lakini hakuna jinsi yote namuachia Mungu. thanks once again Raia fulani.
 
[/I]Raia fulani nimekusoma kaka, you are in my mind jhata mimi nafikiri the same, hata leo kanipigia sim mara 6 akihitaji tuonane nnimetoa excuse kadhaa na ameelewa, ila bado naamini nahitaji busara zaidi kumbadilisha kifikra ila naamini kwa nguvu za Mungu mambo yatakaa sawa, kweli sometimes najuta kwanini nilikutana nae lakini hakuna jinsi yote namuachia Mungu. thanks once again Raia fulani.
[/COLOR][/QUOTE]
You are welcome, bro. Cha msingi yatapita ukitumia akili yako vya kutosha. Na MUNGU pia
 
yaap, nimekusoma kaka nimejaribu kutuma pm kwako, from there we can stay intouch.good night and enjoy your weekend, urakaza neza
 
Pole sana the Future; lakini nikupe hongera pia maana inaonekana wewe ni kijana mtulivu mwenye maadili mazuri...nakupa BIG UP kwa hilo!

Nami niungane na wengine kwamba, please usije ukamuumiza yule binti wa kwanza! Nakuombea Mungu akusaidie kukupa hekima katika kumsaidia huyo mwingine wa pili! Naomba usimdanganye kwamba utamuoa, mwambie tu ukweli; mwambie unaweza ukawa rafiki kwake...lakini sio mume! Kwa kweli kama unamwamini Mungu, basi mwombe atakusaidia!
Nakutakia kila la heri!
 
yaap, nimekusoma kaka nimejaribu kutuma pm kwako, from there we can stay intouch.good night and enjoy your weekend, urakaza neza

haya bwana! Naona hapo mwisho nami umeniacha kwenye mataa. Wkend njema nawe pia, ndugu
 
Vipi jamaa na mabikira? au kaamua kuwachukua wote?
 
Back
Top Bottom