Mabilionea wenzangu wasomi tuliowahi kula boom la chuo likatupumbaza tukutane hapa

Mabilionea wenzangu wasomi tuliowahi kula boom la chuo likatupumbaza tukutane hapa

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Mambo yalivyo ndani ya kichwa cha binadamu ni tofauti kabisa na jinsi yalivyo nje ya dunia a.k.a mtaani,

Nikiwa chuo kichwa changu kiliniambia ntakuwa afisa mkubwa serikalini, nitapokea mamilioni, nitaoa mke mzuri sitafanya kazi za hovyo kama udalali boda boda au kuchoma chipsi. sitaajiliwa na mtu anilipe laki tano mimi na degree yangu, nikizunguka ofisi kadhaa sikosi kazi.

Likitokea kongamano au maadhimisho ya kitaifa nipo nawaona watu mashuhuri na viongozi wakubwa mara kwa mara namimi najiona Magufuli kwanza nmeshiba ugali dona, juisi ya ukwaju na kuku robo kwa pesa ya boom na mfukoni nna ATM tembo card ya CRDB account inasoma digit saba.

Mnaofeli maisha wote ninyi ni wajinga tu, inawezekana vipi usome SUA alafu uishie kuuza mkaa wa mafungu makole .

Baada ya miaka kadhaa sasa ivi nipo nanjilinji nauza dawa za mbu, mende, sumu ya panya, na dawa za kuua kunguni na kispika changu

😄😄😄😄 Mabilionea wenzangu mipango ilikuaje na sasa upo na mishe gani ktk ujenzi wa taifa?

Nawasilisha
 
😁😁😁😁 Dah afu bado serikali inakudai bado hujalipa hela yao uliyokuwa ukula bata batani na riba umeongezewa ku escape labda ufe.
 
Back
Top Bottom