Mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Simba SC yakaribia kumaliza kusuka upya kikosi chake

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Huu ususi mpya uliofanywa na Simba sijui tuuitaje, wasusi kina Kalpana na maras tulionao humu watatusaidia ila ni wazi hii ni Simba brand new tunaenda kuiona.

Misimu miwili iliyopita niliwahusia viongozi wa Simba waanze mchakato wa kuisuka upya kikosi cha Simba ili baada ya misimu mitatu, tuwe na timu mpya kabisa au walau kikosi cha kwanza kipya kabisa. Naona hili linaenda kutimia. Toka nimeyasema maneno hayo, nadhani ni mchezaji mmoja au wawili ndiyo wana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Haya ni mabadiliko makubwa saaana.

Pia jana wachezaji wamefanyiwa jambo la muhimu mnoo kwa kupewa orientation ili wawezi kuijua Simba vizuri. Hili ni jambo ambalo tumekuwa tunalililia kwa muda mrefu, wachezaji wengi wa kigeni hawakuwa wanajua uzito wa timu wanayochezea. Ni kama walikuwa wanasajiliwa, wanapewa mpira wanaambiwa haya nendeni mkacheze. Nadhani hili liwe zoezi endelevu ili liwaingie vizuri.

Huu ususi kama twende kilioni hiviii kwa masela tunaopenda pisi zisizo na mambo mengi.
 
Mwanachama wa simba hapa nasema hivi, wachezaji wa kimataifa wamaana tuliosajili ni wawili tu, wengine ni takataka, wandani walau tumepata. Moo tuachie timu yetu.

Vichekesho hichi nacho Kichekesho..!

Tucheke..?
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Subiri msimu uanze kaka...yani nakuhakikishia Simba msimu ujao ni ya moto...
Hili ni kosi la maangamizi...
Wataita maji mmaaa...
Screenshot_20240708-120510_Instagram.jpg
 
Yanga tumetoka huko miaka 6 iliyopita.
Sibomana, balinya, kiiza, sadney, yikpe, molinga, ally ally, Kaseke, kindoki, nk.

Mbumbumbu team haijengwi na wachezaji zoa zoa
Hizi zilikua ronyaronya mzee hauwezikulinganisha na talents wanazosajili Simba, hizi ni pure talent alafu bado ni vijana na ilitakiwa waende ulaya sema tu pochi la Mo limewavuta wakadondokea msimbazi
 
Mwanachama wa simba hapa nasema hivi, wachezaji wa kimataifa wamaana tuliosajili ni wawili tu, wengine ni takataka, wandani walau tumepata. Moo tuachie timu yetu.
😀😃😂😂😂 Kweli wewe ni vichekesho.
 
Makolo ni mabigwa wa Nini sasa? Ujinga ni kipaji mleta mada kajaliwa.
Wanadai wao ni mabingwa wa Jamhuri ya muungano Tanzania, ......kombe la muungano linawapa kiburi.
 
Huu ususi mpya uliofanywa na Simba sijui tuuitaje, wasusi kina Kalpana na maras tulionao humu watatusaidia ila ni wazi hii ni Simba brand new tunaenda kuiona.

Misimu miwili iliyopita niliwahusia viongozi wa Simba waanze mchakato wa kuisuka upya kikosi cha Simba ili baada ya misimu mitatu, tuwe na timu mpya kabisa au walau kikosi cha kwanza kipya kabisa. Naona hili linaenda kutimia. Toka nimeyasema maneno hayo, nadhani ni mchezaji mmoja au wawili ndiyo wana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Haya ni mabadiliko makubwa saaana.

Pia jana wachezaji wamefanyiwa jambo la muhimu mnoo kwa kupewa orientation ili wawezi kuijua Simba vizuri. Hili ni jambo ambalo tumekuwa tunalililia kwa muda mrefu, wachezaji wengi wa kigeni hawakuwa wanajua uzito wa timu wanayochezea. Ni kama walikuwa wanasajiliwa, wanapewa mpira wanaambiwa haya nendeni mkacheze. Nadhani hili liwe zoezi endelevu ili liwaingie vizuri.

Huu ususi kama twende kilioni hiviii kwa masela tusiopenda pisi zenye mambo mengi.
Mnaanzaga hivi hivi, ila ligi ikishaanza mnaishia kupeleka lawama kwa Mangungu
 
Onana km anabakii, bas abadilikee, yaan aoneshe anastahili kuwepo ktk kikosi cha mnyamaa.
Tena nilisahau kukutag. Embu tuambie huu msuko wa Simba hii tuuitaje?
 
Back
Top Bottom