Mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Simba SC yakaribia kumaliza kusuka upya kikosi chake

Mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Simba SC yakaribia kumaliza kusuka upya kikosi chake

Hizi zilikua ronyaronya mzee hauwezikulinganisha na talents wanazosajili Simba, hizi ni pure talent alafu bado ni vijana na ilitakiwa waende ulaya sema tu pochi la Mo limewavuta wakadondokea msimbazi
Unaimani kama wafuasi wa Mwaposa
 
Mabibgwa wa baharini na nchi kavu 👇😀

GR5V0hVX0AAL2P4.jpeg
 
Huu ususi mpya uliofanywa na Simba sijui tuuitaje, wasusi kina Kalpana na maras tulionao humu watatusaidia ila ni wazi hii ni Simba brand new tunaenda kuiona.

Misimu miwili iliyopita niliwahusia viongozi wa Simba waanze mchakato wa kuisuka upya kikosi cha Simba ili baada ya misimu mitatu, tuwe na timu mpya kabisa au walau kikosi cha kwanza kipya kabisa. Naona hili linaenda kutimia. Toka nimeyasema maneno hayo, nadhani ni mchezaji mmoja au wawili ndiyo wana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza. Haya ni mabadiliko makubwa saaana.

Pia jana wachezaji wamefanyiwa jambo la muhimu mnoo kwa kupewa orientation ili wawezi kuijua Simba vizuri. Hili ni jambo ambalo tumekuwa tunalililia kwa muda mrefu, wachezaji wengi wa kigeni hawakuwa wanajua uzito wa timu wanayochezea. Ni kama walikuwa wanasajiliwa, wanapewa mpira wanaambiwa haya nendeni mkacheze. Nadhani hili liwe zoezi endelevu ili liwaingie vizuri.

Huu ususi kama twende kilioni hiviii kwa masela tunaopenda pisi zisizo na mambo mengi.
Badilisha kichwa cha habari, Simba ni mabingwa wa kombe gani au ulimaanisha Mapinduzi?. Ligi ikianza tusisikie mambo ya bahasha au Mangungu aondoke.
 
Wachezaji waliosajiliwa na simba ukiwafuatilia mchezaji mmoja mmoja, ni ukweli usiopingika jamaa wamesajiri wachezaji wazuri sana. Kitu kimoja ningependa niwashauri viongozi na wanachama wa simba ni kulinda wachezaji wao dhidi hujuma mbalimbali kutoka kwa wapinzani wao. Kwa taarifa za kiintelejensia zilizopo simba kwa misimu miwili iliyopita ilihujumiwa na adui zake kupitia wachezaji wake. wake.
 
Back
Top Bottom