Mabingwa wa ligi kuu (VPL) 2019/2020 mbioni kuweka rekodi ya kibabe

Mabingwa wa ligi kuu (VPL) 2019/2020 mbioni kuweka rekodi ya kibabe

Mhimili uliojichimbia

Senior Member
Joined
Jul 2, 2017
Posts
172
Reaction score
191
Mabingwa wa soka Tanzania bara(VPL) msimu wa 2019/2020, pia wakiwa ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo ambao wamechukua ubingwa wa msimu huu kwa kuweka rekodi mpya ya kutawazwa ubingwa wakiwa na jumla ya mechi sita mkononi wapo mbioni kuweka rekodi nyingine ikiwa tu watachukua kikombe cha shirikisho (FA) .

Wakiwa wametoka kuwatoa Yanga sc kwenye mchezo wa nusu fainali na Azam fc kwenye mchezo wa robo fainali kwa vichapo vikali na kandanda la viwango vya juu, wapo mbioni kuendeleza ubabe huo kwa Namungo fc kwenye mchezo wa fainali na kuweka rekodi ya kutoa vichapo kwa timu tatu za juu za ligi kuu nyuma ya bingwa huyo katika mechi muhimu mfululizo( quarter final, semi-final and final)

Rekodi hiyo ya kibabe itamaliza ngebe zote za mahasimu wake ambao wamekuwa wakaidi kwa muda mrefu kukubali uhalisia kuwa mabingwa hao wapo kwenye viwango vya juu kisoka tofauti na timu zote za VPL.
 
Very true;
Azam atakuwa mshindi wa pili wa VPL alipigwa Goli 2
Yanga atakuwa mshindi wa nne wa VPL Alipigwa goli 4
Namungo atakuwa Mshindi wa Tatu wa VPL atapigwa Goli 3.
Kazi wanayo hao Namungo huko Mandela Stadium Sumba- Wanga
 
Tunachukua
1. VPL
2. FA
3.Ligi ya Wanawake
3. Mfungaji bora
4. Kipa bora
5.
 
Back
Top Bottom