Mabinti hebu mjifunze ku normalize haya yafuatayo

Mabinti hebu mjifunze ku normalize haya yafuatayo

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
  1. Normalize kutokuwa muhitaji kiasi kwamba uhitaji wako ukaifunga akili na hekima yako na kukufanya ukawa mwehu kuweka mwili wako rehani sababu ya shida za kupuuza na kupita. Ishi kwa kutokutegemea favours kutoka kwa wanaume tofauti tofauti kwa vitu vidogo vidogo ambavyo unaweza jifanyia mwenyewe. Wewe ni msomi, una nguvu za mwili na akili, mwili wako hauna ulemavu, unashindwa hata kubuni kakitu kakukuingizia elfu 2 kwa siku ili usisumbue watu na kuhitaji sijui vocha, umeme, sijui nini.
  2. Normalize kuwa positive kwenye negative situations zozote za kimahusiano na Maisha ya pamoja. Inasaidia kumfanya mwanaume akuone wewe ni corner stone au chachu ya mabadiliko yake na yenu kuelekea maendeleo. Kuwa negative kwa mwanaume kipindi anapitia magumu ni toxic behavior achana nayo haraka sana. Wanawake wengi wanaachika au kutodumu katika mahusiano sababu ya negative behavior wakati wa negative situations.
  3. Normalize kuwa mwili wako na sex sio bargaining chip ya mahusiano na wanaume. Utakuwa mjinga sana kuamini sex ni kitu mwanaume hawezi pata popote isipokuwa kwako. Normalize kuona sex ni sehemu ya mahusiano na usipende kubembelezwa ili utoe. Kuwa simply accessible kwa mwenzako bila masharti ya kitoto. Zingatia unacholeta katika meza ya mahusiano ni kitu gani, wanaume wanathamini zaidi akili ya Maisha kuliko mwili wa ngono.
  4. Normalize kujadili issues na conflicts ndogo ndogo badala ya kuwa mwepesi kususa na kuondoka au kuanzisha mahusiano mapya haraka haraka. Kumbuka unayedhalilisha mwili wako na kushusha hadhi yako ni wewe, wanaume kadili wanavyokuchungulia ndio unazidi kushuka thamani kwenye jamii.
  5. Normalize kufix mahusiano badala ya kutafuta perfect partner kila uchao, miaka 24 upo na mwanaume wa 45,wewe huko chini ni choo cha stendi hadi kila mwanaume apakojolee. Body count ina matter kwa wanaume serious. Usijidanganye kuwa utakuwa salama baada ya kulala na wanaume zaidi ya watatu. Dunia haina siri.
  6. Normalize kumuombea na kuwa bega kwa bega na partner wako kama sehemu ya uanaumke na sio kujiongeza. Kasumba ya mabinti wa kisasa ni kujiona wao wanazero responsibility kwa mwanaume ila wanataka huyo mwanaume awe responsible kwao kwa 100% niseme tu huo ni utoto.
  7. Normalize kukua kiakili na sio kujiona binti kila siku. Umri wako uendane na matendo na haiba yako. Binti wa miaka 23 au 24 TikTok kujipost mitandaoni,kuforce viral trends za kipuuzi,kutaka kila kiwanja cha bata uende ili iweje sasa.
  8. Normalize kuwa na marafiki wenye mitazamo ya kiutu uzima na wanaoheshimu mahusiano yako hata kama wao wanamuona mtu wako hana swaga. Kumbuka wewe ndie unaeishi na kufanya nae maisha, wao watashauri na kukaa kando moto utakuwakia wewe.
  9. Normalize kwenda nyumba za ibada badala ya nyumba za starehe katika umri huu wa ubinti. Soma vitabu vya MUNGU sio page za udaku Mitandaoni. Kumbuka ukisomacho ndicho kitakachokuja kuwa matendo yako ya baadae. Jiweke karibu na mafunzo ya MUNGU na sio mitandao ya udaku.
  10. Normalize kutii mwanaume badala ya kushindana nae au kujihami ukidhania hiyo itakupa Heshima kwake. Wanaume humjali na kumpenda mwanamke mwenye kutii na kuheshimu wao kuliko mwanamke mwenye combative, aggressive , egomaniac,arrogant character.
  11. Normalize kujiwekea akiba yako ambayo utaitumia kutatua shida ndogo ndogo na hata pale boyfriend wako akiwa amekosa kabisa mfukoni then huna haja ya kupanic utumie akiba yako kutatua shida zako za lazima wakati ukishikamana nae nyakati ngumu badala ya kutokuwa na akiba na kumuona mwanaume wako ni useless kumbe wewe ndie useless partner kwenye mahusiano.
  12. Normalize kuwa na mwanaume m'moja bila kuwa na wengine nje kwasababu yoyote ile iwe shida ya uchumi, utajiri, mali, usiwe mjinga kiasi hicho unamdhalilisha baba yako aliyekulea uje kuwa mwanamke na sio kahaba. Chochote kile cha kudhalilisha jina la baba yako ndicho kitachomdhalilisha mwanaume wako pia. Linda heshima yako.
  13. Normalize kufanya therapy kila baada ya kupitia heartbreaks badala ya kujiona victim na kuwa na victim mentality na kuja kubebesha partner mpya msalaba wa dhambi ulizotendewa kwenye uhusiano wa awali. Therapy ni tiba ya akili na ni muhimu sana. Kama ukiumwa maralia haukai nayo kimya unakwenda hospital mbona hayo maumivu ya moyo unakaa nayo sasa ukiamini kuwa hayatakuwa na madhara.
  14. Normalize kuanzia Maisha katika level ya chini, its okay kuanza life ya mahusiano na kijana mwenye chumba kimoja, bafu nje, godoro sakafuni na stuli moja. MUNGU hubariki maono, shetani hukuletea mitego kulingana na tamaa zako. Jua tofauti ya mitego ys shetani na baraka za MUNGU. Shetani hukupa unachotaka kwanza then atakutaka u sacrifice kitu ambacho anajua kwako ni irreplaceable kama ndoa, familia na mume bora. MUNGU hukuletea mume wakujenga nae familia na kupata nae mali kisha anaanza kuwabariki na utapata zaidi ya ulivyotarajia kupokea. Subira muhimu.
  15. Normalize kuwa na tabia ya kujali na kujitoa hata pale usipopokea au kupata chochote kwa mwanaume hautakufa. Mwanamke anayejali huwa anatengeneza makao ya kudumu kwenye moyo na akili ya mwanaume. Kwasasa kila mwanamke anapambania shida zake, unaona ndoa namna imekuwa kitu adimu kwao, umeona namna wanaume wamepunguza kujali na kupenda wanawake badala yake wanawatumia na kusepa. Sababu ni hiyo nimekupa.
 
Hii 5 ni kweli kabisa, huwezi kuwa mdangani kisha watu wasijue, watajua tu, hakunaga siri duniani.
 
Haki ya nani vile hapa sasa nipo safe maana sitaona sketi ikipita.
 
Kaziii ipooo, hapoo badooo, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yote uliyoandika hapo kwa asilimia kubwa yanawanufaisha zaidi wanaume kuliko wanawake wenyewe yani ukiona jambo wanaume wengi wanali support ujue lina maslahi kwao bila kujali upande wa pili, ifike pahala muwaambie mabinti wafanye yale yanayowapa furaha wao na si yanayowapa furaha wanaume yani furaha yao ndio iwe kipaumbele, acheni huu ubinafsi wenu uliojificha kwenye kivuli cha kuwasaidia wanawake na kujifanya eti ninyi hampati hasara yoyote wanawake wanapoharibikiwa
 
Kwanza huo muda wa kusoma wanao? Kumbuka andiko lako kw asilimi kubwa limelenga hawa wa alfu mbili. Wangekua na angalau dakika kumi za kusoma na kutafakari wangeenda extra miles
Ngoja tuache ushahidi kwaajiri ya wajukuu zetu vizazi vijavyo waje kushuhudia maonyo na mafundisho tuliyokuwa tunatoa kila siku ili iwe ushahidi kuwa wanaume tulikuwa na misimamo ila wanawake wakachagua kukengeuka wasijekusema hawakufunzwa na walimwengu.
 
Watapita kimya kama hawauoni.

Maslahi yao ya kipato yamewekwa under attack.

Uchi wanaotumia kama kivutia pesa wanaambiwa wa normalize kuutoa bila masharti😂😂
Hawawezi kufikiria nje ya kujiuza miili. Hatari sana hii.
 
Hongera kwa andiko zuri hata wasipocomment lakini wamesoma na limewakolea
Muhimu ni wasome tu. Hata wasipochangia kitu maana yake ni wameelewa vema somo. 😂😂😂 Elimu iendelee kutolewa kwa nguvu bila kudekezana wala kubembelezana.
 
Back
Top Bottom