Ni kwasababu umechagua kufikiria kama mwanamke ambapo always ni kukwepa kuwajibika na kutaka kuonekana innocent and that's why unadhani wanaume wanafanya kitu hicho hicho ama kufikiria kama wewe namna unafikiria.
Wanaume huwa hatukwepi kuwajibika na ni kawaida yetu kubeba lawama sometimes hata kwa makosa ambayo chanzo chake ni wanawake.
Nyuzi ngapi hapa nimendika kuhusu wanaume na umeona namna wanapokea malalamiko positively?
Nadhani unafeli padogo sana katika hizi nyuzi za wanawake kuwajibishwa yaani unashindwa kuwa muelewa na kukubali kuwajibika.
Mimi hakuna mahali nimesema wanawake ni innocent ila ninyi wanaume ndio huwa mna hiyo kasumba ya kujiona innocent yani siku hizi mambo yamebadilika wanaume ndio mnaplay victims kwenye mahusiano, ni wanaume gani hao ambao wakisemwa maovu yao wanayapokea positively mbona mimi nikiwasema huwa wanashindwa hoja wanaishia kunitukana kama hivi ukweli ni kwamba wanaume wengi hampendi kuambiwa wala kukubali ukweli, kama hamuwezi kukemea maovu yenu basi nawashauri muache kabisa kukemea chochote maana mnajisumbua tu haiwezekani tendo linahusisha jinsia mbili halafu mmoja unamuambia akifanya ni kosa ila mwingine unamuambia akifanya ni sawa hivi wewe unaona kuna logic kweli hapo
Mimi nimegusia kipande cha wazazi na ndugu zake kuwa it was unnecessary wewe kugo that far hadi kushusha heshima na utu wako just because of a simple attack. Unajua mtu anayeleta panga kali katika ugomvi wa fimbo ni wazi ameover react. I was checking you on that part.
Unasema nipo biased kwakuwa umenichukulia hivyo but i know my limits kwenye mijadala hata kama utanikwanza hadi kiwango cha juu. But lengo sio kukuumiza hisia lengo ni kunyoosha au kupoint out ukweli.
Vitu kama kuitwa msagaji, mdangaji,mlevi,mwizi,sijui kitu gani si ni mtu tu ameamua kukulipua na wewe unatakiwa kuwa na "thick skin" why unachukulia serious vitu ambavyo havisemi ukweli wowote kuhusu uhalisia wa maisha yako my dear? I know unaweza kuwa katika badmood na maneno ya mtu yakakuprovoke then usiwe quickly irritated just be normal and handle the situation like a pro as u usually handle. Me nakuambia hivi coz i know you usually handle these situations politely why unadhani nimeku address directly?🤔
Mimi siwezi furahia hata wewe mtu akikuattack kwa namna ambayo sio fair na ya kukuharibia reputation yako.
But kama mtu ana kuattack kwa namna ya kukumaliza nguvu tu na kukuzingua why iwe big deal. C'mon bwana don't make this look like i am picking on you for no reason wakati u know that am not. Me siwezi furahia wewe ukiharibikiwa au ukidhurika.
Sasa wewe ukidhurika me nitagombana na nani hapa JF?
Tatizo siyo hayo maneno kuwa kweli au uongo tatizo ni kwamba hii ni public platform watu wengine wanaposoma wanaweza kudhani ni kweli, hasa ukizingatia kwamba mtu anafanya hivyo kwenye nyuzi zaidi ya moja huku akisisitiza kwamba ananifahamu mimi nje ya jf, na kama nilivyosema wengine usiwapowajibu wanaendelea mpaka uwajibu vibaya ndio wanaacha
Hebu imagine ungekuwa ni wewe mtu anapita kwenye nyuzi anaanza kuwatangazia watu kwamba wewe ni shoga anakufahamu nje ya jf wewe utachukuliaje, najua hapa utasema utachukulia kawaida lakini nakumbuka kuna uzi ulipanic ukaanza kutumia lugha kali na watu uliokuwa unawajibu wala hawakukutukana, lakini hapa unataka kuniaminisha kwamba mtu kunitukana matusi ya nguoni kwenye jukwaa kama hili ni kitu cha kawaida hivyo nichukulie poa tu
Kuna watu wanashitakiwa na kulipishwa faini au kufungwa kabisa kwa sababu kama hizi za defamation of character, hapa angekuwa ni mtu maarufu pengine angeshaenda kumshitaki jamaa kwa kumchafua na angeshinda kesi, halafu wewe uko hapa unasema hilo ni jambo la kawaida eti kisa halina ukweli wowote
Nimekuelewa sana mkuu,kuanzia leo sitamwimbia tena mke wangu kuwa nae alete hela
Mkuu inatakiwa tufike pahala tuchague moja kama tumeamua kwamba dunia imebadilika basi isibadilike kwenye majukumu ya mwanaume tu bali na ya mwanamke pia, lakini kama tumeamua kukomaa na tamaduni zetu basi wanaozifuata wahakikishe wanatekeleza ule mgawanyo wa majukumu kwamba mwanaume akatafute na ahudumie familia kisha mwanamke akae nyumbani, huu ubinafsi wa kutaka mke asaidie majukumu ya mume na bado afanye majukumu yake peke yake ndio inasababisha wanaume kutukana wanawake bila sababu
Asante dada nimekuelewa sana. Hapa kama jamii inabidi tu deal na chanzo na si matokeo. Kweli kabisa maisha yamebadilika ila matarajio juu ya kizazi cha kike hayajabadilika.
Yeah mkuu wanaume wengi wana matarajio mengi sana toka kwa wanawake, mwisho wa siku wakikosa yale waliyoyategemea wanaanza kutukana wanawake, wanademand vitu ambavyo hata wao wenyewe hawawezi kuoffer kwa wanawake
Sasa hapo inakuwaje ni kudeal na matokeo? 🤔 Kwasababu wanaume hawana shida mwanamke kukaa nyumbani shida ni je,wanawake wanakuwa cooperative kwa wanaume zao kipindi wakiwa nyumbani? Je wanasimamia misingi na maelekezo au wao wanakuwa wanapanga yao wakati mwanaume anapanga yake?🤔 Mfano unaacha mke nyumbani je anasimamia majukumu kisawa sawa,anakusaidia kumaintain pesa zako vema,anatunza watoto vema, anakulindia heshima yako kama mume vizuri na kukupa umuhimu wako kama mume maishani mwake? Wapo wanawake walikuwa wanafanya hivi,ila kwa miaka hii imekuwa very rare kupata mke wa kariba hii. Ukiweka mwanamke ndani we nenda kazini,kama hajaliwa na jirani hapo,basi ataliwa na boda boda au atakuwa anatoka kuliwa huko nje.
Tatizo ni kuwa wanawake wakibaki nyumbani mnawanyanyasa kwa kisingizio cha kwamba mnawahudumia ndio maana nao wanaona wajitafutie vyao ili walau wawe na sauti juu ya maisha yao, mpaka mwanamke ameenda kuliwa nje ujue kuna tatizo kwa mumewe kwa sababu umalaya siyo hulka ya mwanamke hata maandiko yanasema mungu alimuambia mwanamke kwamba tamaa yake itakuwa kwa mumewe tu, tofauti na wanaume ambao umalaya ni hulka yenu ninyi hata mke awe amekamilika kila mahali bado mtachepuka tu lakini ukiona mwanamke anachepuka ujue shida iko kwa mumewe ila kwa sababu wanaume huwa hampendi kuwajibika kwa mapungufu yenu na kazi yenu ni kuwatupia tu lawama wanawake basi huwa mnakataa hili
Huu sasa unaoleta hapa ni Uzungu,jambo ambalo ni kinzani kiutamaduni kwetu waafrika. Kufanya kazi na kutekeleza majukumu ya mke haijaanza leo labda kama haujui. Wanawake miaka yote wamekuwa wanafanya kazi nyingi lakini bado ndoa waliitumikia. Au haujui huko vijijini wanawake walikuwa wanakwenda shambani na mume na kushinda huko siku nzima, wanapika chakula wanakula na kuendelea kulima hadi jioni,wakirejea na wanapika kama kawa na mzigo usiku wanatoa na waliendelea na ndoa kama kawaida. Ila ninyi wa siku hizi kazi zenyewe hizi za kukaa siku nzima,ukirudi unasema umechoka kumbe ni uvivu tu plus mshahara wenyewe hauonekani na ukitumia tu mshahara wako Kwenye familia basi unahisi na wewe ni mwanaume unaanza kuleta mikosi kwenye ndoa.
Hivi kwanini huwa mnapenda kujustify ukandamizaji wa wanawake kwa kuwatolea mifano bibi zetu hivi una uhakika kwamba bibi zetu walikuwa wanafurahia hayo maisha, kwahiyo unataka kusema kwamba tamaduni kwa sababu tu zilifanywa na wazee wetu basi ni sahihi eti kisa tu maisha yalienda vizuri je yalienda vizuri kwa mujibu wa nani, na ni nani aliyewaambia kwamba bibi zetu kudumu kwenye ndoa maana yake walikuwa wanazifurahia hizo ndoa maana bibi zetu baadhi walikuwa wanapigwa na wananyanyaswa kwenye ndoa zao ila bado walidumu je unataka kusema walifurahia vipigo na manyanyaso
Yani ulitegemea bibi zetu wangekataa vipi hayo majukumu kwenye jamii ambayo mwanamke hana uhuru wala sauti na kuna mila nyingi za kumkandamiza yani zamani binti akishaolewa hatakiwi kurudi tena nyumbani hata afanyweje anatakiwa avumilie maana akirudi baba yake anamtimua arudi kwa mumewe, siyo kila tamaduni zilizokuwepo bibi zetu walizifurahia hata kukeketwa nao ulikuwa ni utamaduni lakini haukuwa na faida yoyote kwa wanawake bali ulikuwa na manufaa kwa wanaume na wanawake hawakuufurahia lakini hawakuweza kuukataa kwa sababu zilishawekwa sheria za kwamba binti asiyekeketwa hatakiwi kuolewa na binti usipoolewa unaonekana una mikosi
Hapa tunaongelea usahihi wa huo mfumo bila kujali ni kina nani waliufanya kwahiyo wewe unaona ilikuwa sahihi bibi zetu kufanya majukumu yote hayo huku waume zao hakuna cha maana walichofanya seriously unaona kabisa hili ni suala la kumsisitiza mtu huu kama siyo ubinafsi ni nini, yani wanaume bado mna ile mentality ya bora punda afe ila mzigo ufike yani ni heri mwanamke aumie asifanye yale yanayompa furaha ila mwisho wa siku mradi ndoa idumu na mume apate furaha halafu mnajitoa ufahamu mnakuja kusema eti mbona zamani wanawake walifanya hivi na vile na bado ndoa zilidumu, halafu mkiambiwa kuwe na mgawanyo fair wa majukumu mnasingizia eti ni uzungu ili muendelee kuwakandamiza na kuwabebesha mizigo wanawake wafanye majukumu mengi kuliko ninyi kwa kisingizio cha tamaduni
Kwanza sijui kama wanaume huwa wanawafosi wanawake kwenda kutafuta pesa siku hizi,inawezekana waliunga mkono hiyo ajenda miaka fulani hapo katikati ila walioruhusu hiyo kitu nadhani ni wachache wamefaidika ila wengi wamejutia na kuwapoteza wake zao na kuharibu mahusiano kabisa.
Lazima mkubali kwamba ili mwanamke awe chini yako basi uwe unamhudumia lakini ukishaanza kutaka ajihudumie mwenyewe kunakuwa hamna maana tena ya yeye kuwa chini yako, msingi wa utii wa mwanamke kwa mwanaume umejengwa kwenye wajibu wa kiuchumi wa mwanaume kwa mwanamke huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia hiyo ni kanuni ya kiulimwengu ila wanaume wa kiafrika mnalazimisha majukumu sawa ila hamtaki haki sawa, lazima mchague moja hamuwezi kupata vyote kila aina ya mwanamke hapo anakuja na package yake ukitaka mwanamke wa kukutii na kutimiza majukumu yote ya nyumbani basi oa mama wa nyumbani ila ukitaka mwanamke wa kukusaidia majukumu yako basi kuwa tayari akusaidie na nafasi yako pia vinginevyo mtaendelea kuwatukana wanawake hadi mwisho wa dahari wakati kumbe tatizo liko kwenu kuwa na matarajio makubwa kuliko uhalisia
Haya uliyosema hapa sio general occurrence kwenye jamii yetu. Unataka kunambia wanawake wangapi wanafanya hizi kazi Tanzania nzima au unatazama zile video za mitandaoni unahisi ndio uhalisia? Mwanamke abebe zege si atasogeza tu hapo na pale,anaweza balaa la kupandisha zege ghorofa ya 13 huko bila protection?
Hakuna mahali nimesema kwamba hiyo ni general au kwamba wanawake wote wanafanya hivyo ila nilikuwa najaribu tu kukuonesha kwamba siku hizi wanawake wapo kwenye kila field, ila wanaume kwenye suala la kazi za nyumbani bado wanasuasua wanajifanya wamegoma kubadili mentality yao halafu mnadai eti wanawake wanazingua hawako tayari kwa haki sawa wakati ni ninyi ndio ambao hamko tayari, kwahiyo unabisha kwamba hakuna wanawake wanaobeba zege wakati mimi nimeshawashuhudia kwa macho yangu sasa unashangaa nini kama kuna wanawake wananyanyua mavyuma gym hadi wanakuwa na mamisuli kama wanaume na wengine hadi wanakuwa mabondia inashindikana nini kubeba zege
Vita gani hizo ambazo wanawake wanakwenda na wanapigana front line au unasema wale wanaokwenda wanajificha vitengo vya IT,kuendesha drones,au kubaki kambini wakipeleka mafile huku na kule? Balaa la kupigana man to man unalijua wewe bi dada?
Kama mambo huyajui uliza kwa wanaoyajua utaambiwa kwa taarifa yako wapo wanawake wanaopigana vita frontline na wala hawajaanza leo, tangu vita ya pili ya dunia kuna wanawake walikuwepo kwenye vitengo vya kutengeneza silaha mbalimbali za kivita tena zile hatari na walijua kuzitumia hebu penda kujielimisha, hata kwenye vita ya kagera ya tanzania na uganda wauganda walikuwa na mwanamke mmoja aliwasumbua sana wanajeshi wetu kwenye ile vita hadi siku baadhi walipomkamata huko maporini na kumfanyia mambo mabaya
Hao wanaume ambao anafanya kazi halafu anamwambia mkewe na yeye afanye kazi kisha mwisho wa mwezi wote walipe bills ni wanaume wa wilaya gani hao? Nadhani unachanganya scenarios hapa,unamuongelea Mwanaume muwajibikaji kwenye sentence ya kwanza halafu ya pili unamuongelea Mwanaume marioo mtegeaji wa majukumu yake kwa familia yake. Mwanaume ambaye anasema mwanamke wake na yeye afanye kazi sababu itakuwa ameona mke ana mlalia sana eneo la gharama kwa vitu visivyo na ulazima. Mtu anataka mtoke out kila weekend,anakupiga virungu kila dakika akitaka kupewa pesa kununua vitu ambavyo havihitaji ila katamani tu. Mara atake kutatua matatizo ya ukoo wake na kuacha kufocus na familia yake na mume wake, mwanamke wa hivi kwann usimwambie akatafute kazi na yeye aone uchungu wa matumizi ya hovyo ya hela.
Tatizo lenu huwa mnaona matamanio yenu ndio yana umuhimu ila ya mwanamke hayana umuhimu ninyi mbona huwa mnatamani mambo ya kijinga huko nje na hamjishangai ila mwanamke akitamani mambo yake mnaona kama anafanya utoto, kwani mtu kutatua changamoto za ukoo wake kuna shida gani ndio maana siku hizi wazazi wanasomesha mabinti zao ili waje wawasaidie siyo kama zamani ndio maana nikasema chagueni moja ni either muoe wamama wa nyumbani ili wawatii huku mkitakiwa kuwajibika kwao, au muoe wanawake watafutaji huku mkisacrifice suala la utii kwa sababu mnakuwa mmepunguziwa majukumu yani sijui kwanini wanaume hamtaki kukubali kwamba mamlaka mliyojipa yanakuja na wajibu hakuna mamlaka ya bure dunia hii ni lazima uwajibike kwa unaowatawala cause with great authority comes great responsibility
Umemjibu kwa hekima sana, kama ni muelewa atakuwa ameshakuelewa kwamba misimamo yake ni hovyo ila ashike kile ulichomwambia.
Sisi kwetu tulifundishwa mtu mzima akikuelewesha jambo kisha ukajiona umemjibu harsh, akikujibu sawa nimekuelewa, yaani amekubali kusikiliza pumba zako maana yake anataka yaishe sababu amekuona wewe ni jeuri na sio muelewa.
Mnapenda sana kujifariji asee, comment yake iko clear kabisa kwamba ameelewa nilichomuambia, ila wewe unataka kulazimisha kwamba amenikosoa kwa mafumbo ili tu uifariji nafsi yako
Unatumia nguvu kubwa kumuelewesha huyo mtu, hakuna mwanaume anaweza kuishi na mwanamke mjuaji, kiburi namna hiyo.
Achaneni na hizi personal attacks haziwasaidii zaidi ya kudhihirisha uwezo wenu mdogo wa kufikiri na kujadili hoja, tatizo lenu mmekaririshana kwamba kila mwanamke yuko desperate na ndoa na hawezi kuishi bila mwanaume ndio maana mnatoa kauli kama hizi mkidhani mnatutisha na tutaogopa, sasa mkikutana na wanawake kama sisi ambao hatutishiki mnaanza kututukana na kutuita feminists mara wajuaji kumbe wengine tunajua tunachokitaka yani tunaona kuliko kuwa na wanaume wenye inferiority complex design yenu ni heri tuwe single mpaka tunakufa