Mabinti, kuna la kujifunza hapa

Mabinti, kuna la kujifunza hapa

Nimepita pita huko mtandaoni nikakutana na hii video ya mwanadada wema sepetu a.k.a Tanzanian sweetheart akilia mtandaoni na kumwaga chozi la maumivu linaloashiria anapitia hatua ngumu sana ya maisha yake.

Sijajua hasa alikuwa specific na maumivu gani ila nakumbuka juzi ya juzi kuna on-line media interviewer alimuuliza swali kali sana na la kikatili kuhusu swala la wema kuwa na mtoto,swali ambalo wema sepetu alijikaza sana kulijibu kistaarabu ila macho na uso wake uligubikwa na huzuni mzito sana na muonekano wa aibu uliochanganyika na maumivu ya kutoneshwa hisia.

Asije akakudanganya mtu, furaha ya kila mwanamke by age 30+ ni kuwa na familia yake ya Baba,mama na watoto. Haya yasipotimia mwanamke huwa anakuwa katika msongo wa mawazo usiokwisha ambao huendelea kukua kadiri umri unavyokwenda.

Wema kama wanawake wengine anaonekana kupitia hiyo hali sasa kwasababu yupo nje ya wakati kwenye ndoa na familia. Wanafiki wanajitahidi sana kumfariji kuwa hakuna shida bado hajachelewa ila hata yeye anajua amefika kituni saa moja kasoro kupanda basi la saa kumi na moja alfajiri.

Huko juu hakutakuwa na wa kukutetea. Najua mnajifariji kuwa utakwenda nyumba ya ibada kupata rehema/neema za Muumba ili upate nafasi ila ukweli tunaojua wote kuwa kujutia sio jambo wakati wa hesabu ukifika kulipa ipo pale pale. Kama unabisha si ujaribu ujionee.

Sijui anachopitia ila najua anatamani aamke iwe ni ndoto kuwa katika wakati huu ili awe serious na kila anachoamua na kuweza kujenga njia kama wenzake ambao hawana michezo na maisha.

Baada ya kusema hayo niwatakie jioni njema na kuwasihi wale ambao bado wanaona wanaume tunawafuatilia,tunawadharau,tunawakejeli,tunawaponda waendelee hayo maisha ya kuruka ruka hovyo ili uzeeni waje kupewa hesabu ya ujanani.
Kwani alishawahi toa mimba???
 
Japo alishakiri kutoa mimba za kanumba lakini huwa simcheki binadamu mwenzangu akiwa katika hali kama hiyo.

Ukifikiria ni hatari ngapi tumepitia lakini Mungu akatuvusha, utajua tu si kwa kuwa werevu Ila ni neema yake tupo salama.
Kama alitoa mimba.......alishiriki kufanya mauaji kwa damu isiyo kuwa na hatia........
Na hiyo damu ndiyo inayomtesa.....
 
Back
Top Bottom