Mabinti kutopenda hisabati

Alola

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
476
Reaction score
299
Wakuu habari zenu.
Nimekuwa nikijiuliza kwanini mabinti wengi wanachukia somo la hisabati?. Katika kusoma kwangu O-level (additional math) mwanamke alikuwa m1 kati ya wavulana 20. A-level (PCM) walikuwa wa3 kati ya wavulana zaidi ya 20. Wakati huo huo wameonekana wakimudu sana masomo ya lugha ukilinganisha na wavulana. Je wengi wao wameumbwa na uwezo mdogo wa kulimudu somo la hisabati au huwa wanapotoshana kuwa ni 'somo la kiume'?
 
Usilinganishe zamani na sasa Mkuu !

Saizi watoto wakike Havijaiva Wanaipua !

Na mashuleni ndo wanapeana bila mizani !

Na ma binti wakijiingiza tu kwenye mtelezo huo ! Usitegemee kama ata concentrate na elimu ! Atakuwa ana act tu !

:closed_2:
 

Hisabati ni janga la kitaifa siyo mabinti tu,mimi naamini kufaulu somo lolote asilimia kubwa ni bidii ya mwanafunzi.Watoto wa .com wanazani akifundishwa na mwalimu mzuri wa Maths by default watafaulu,utawakuta busy wanatafuta walimu wazuri,wakifundishwa wanatia notice kapuni.
Namkumbuka mwalimu wangu mmoja wa maths na Additional mathematics alikuwa anapenda kusema "we learn Mathematics by doing not by listening".Nikiwa shule hesabu lilikuwa ni somo langu la kwanza kujihakikishia ufaulu cause kama uko fiti,unajisahihisha kabisa kabla ya mwalimu.
Walimu nakumbuka walikuwa wanatuambia walau usolve maswali 10 kila siku ya Maths tatizo wanafunzi hawafuati ushauri wa walimu,ingawa si walimu wote wako vizuri sana katika Maths.
Bidii yako ,vitabu vingi vina maswali na majibu yake,vingine na solution kabisa sasa tatizo ni nini?Tunatofautiana uwezo,kuna mwingine anaelewa baada ya wiki moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…