Mabinti wahitimu wa vyuo Amkeni

Inasikidisha kwakwel.
Lakin baya zaidi ni kwamba vijana wengin wanakosa utayari wa kujitoa , hata ukiwapa kazi hawana morali wala juhudi wala nidhamu, unaishia kuwaangaliaa na kusikitika.

Maisha ya fasta fasta kwa kiwango kikubwa yamewaathiri, hawana utayari kabisaaa wa kujipa muda wa kuhangaikia jambo mpaka likae sawa.
 
Nadhani pia kuna shida mahala katika malezi ya watoto wa sasa.

Nakumbuka wakati sisi tunakua, tulikua na marafiki wengi sana kutokana na mtindo wa maisha wa kipindi kile. Na hii ilikua ni kwa watoto wa kike na wakiume. Michezo mingi sana ya outdoors ilikuwa inatukutanisha na kupelekea kujenga urafiki ambao uliendelea mpaka tumefika sekondari na wengine hadi vyuoni nk.

Ukiacha hayo, pia kulikua na matukio mengi ya kuwaleta vijana pamoja kama madisko vumbi, concert, mabonanza ya mitaani, mechi za mpira, sinema, matamasha nk kwahiyo ilikua ngumu mtu kukaa tu ndani.

Siku hizi watoto tunawalea indoors. Mtu anasoma kuanzia msingi mpaka chuo kikuu hata mtaa anaoishi haujui vizuri maana anapanda gari asubuhi na jioni, hana marafiki, hana cha kufanya, hana pa kwenda, starehe yake kubwa ni kuangalia tv na kulala! Hii ni hatari sana kwa kizazi kinachokuja sijui tutakua na watu wa aina gani?
 
😀 😀 😀
 
Watoto wa siku hizi hata ''skrapa'' hawaokoti , miaka ya nyuma watoto wanatafuta pesa tangu shule ya msingi ila ilikuwa mbaya wananogewa sana mpaka wamnaacha shule ...Sasa hivi hata kesi za child labour hakuna kama zamani ndio inafanya watu wabweteke mpawa wawe wakubwa.

Makadirio wanaomaliza chuo ni miaka 22 na kuendelea hapa hawana mbinu yoyote ya kupata pesa, akifikiria maisha ya chuo then aanzie chini basi anaona jau sana.
 
Mkuu hapo kwenye 'hata vyuma hawaokoti' nimecheka sana

Subiri nimalize kula, nikauze mabeseni yaliyopasuka yapo tu ndani naenda kuyauza kwa wale wananunua chupa
Umeniispire kiaina
 
Kuna mfumo wa maisha ya Tanzania MUNGU ameuweka ila hautumiki, na kama umetumika ni 2% ya software yake imetumika! Waache waendelee kung’ang’ania 🎓 wakati la saba wanaendelea kula mema ya Tanzania life improvement Software tuliyowekewa na MUNGU!
 
Unajua naona kama mipango ya serikali inalenga kuwasabotage watoto wa kike miaka hii[emoji848]

Kampeni nyingi na kelele ni kuwaelekeza watoto wakike kupambana na maswala ya kitaaluma na elimu halafu wakisha accomplish jamii na serikali vinawatenga na kuwaacha solemba.

Sasa mtu anafika 30+ elimu yake haina msaada, hali ngumu kitaa, hana familia, hana mume, yaani wanawapa msongo mkubwa sana hawa mabinti.

Natabiria hapa hadi kufika mwaka 2030 tutaanza kupata kesi nyingi za Psychosis mabinti wa sasa wakianza ingia umri wa menopause watakuwa katika hali ya sonona ya kudumu na pengine tusishangae wakaanza kutumia dawa za kupunguza msongo wa mawazo (antidepressants) na dawa za usingizi (insomnia). Hii naanza kuiona mapema sana kama dalili zake zinaonekana wazi mapema.

Kama wanajamii turejeshe mamlaka yetu ya kuamua jamii yetu inakwenda na mfumo upi wa maisha turejee tamaduni zetu.

Hizi longolongo za serikali na vitaasisi vinavyodhaminiwa na mataifa ya magharibi na story zao za kumkomboa mwanamke naona zinalenga kumharibia future yake zaidi. Wanaokoa wanawake 10 wanaangamiza mamilioni ya watoto wa kike ambao pengine wangekuwa na maisha yao kama wangechagua kuanza kawaida.
 
Inaonekana wewe utakuwa mmbea sana. Watu wanaongea mambo yao ya nyumbani na wewe unawasikiliza na "kuwachora" unayahifadhi kichwani na kuja kuyaandika humu. Kwnai nani kakwambia wanaokaa nyumbani ni mabinti wa chuo peke yao. Kuna watu hawana tabia ya kuzurura hovyo mtaani kama Kibu Denis😀 anavyoruzura uwanjani bila kuscore magoli.
 
Ungewaambia hao wamama kuwa kuolewa sio ajira, wawasisitize mabinti zao kufanya hata biashara ndogondogo.
Usichokifahamu kuna ajira halafu kuna namna ya kuishi. Wewe hapo ukiwa na shida kuna watu wanakupa msaada bila masharti ya kuwapelekea wadhamini wala dhamana yoyote wanakusaidia sababu wanakujali na wewe ni sehemu ya Maisha yao, unaka kunambia hawa watu ni taaisisi au kampuni ya mikopo na wanalipa kodi serikalini kwa wanavyokusaidia? [emoji848]

Then the same goes kwenye mahusiano, yanakutreat kama ajira but si ajira ndio social security area ya mwanamke kuishi na kupata mahitaji yake ya kila siku.

Hizi fikra za ubinafsi na za kimagharibi mnazodanganywa kuwa ndoa haina umuhimu ila ajira ndio muhimu nenda kawaulize wenzako wenye ajira na hawana ndoa halafu watafute wenye ndoa ila hawana ajira halafu watazame ujiulize ni wapi wanaishi vizuri na maisha yanaenda, hata kama wote wanaexperience stress.

Ndoa ndio kitu cha kwanza mwanamke unatakiwa kupigania upate mahusiano imara na ndoa halali na inayokwenda maisha utakuwa umetoboa, kazi kuna muda itakushinda na bado shida zitakuandama hakuna utakachofanya.

Sio unachanganya ndoa na haya mahusiano yenu ya siku hizi ya "sogea tuishi sote" halafu mnavyokuwa hamna adabu mnapata hadi na watoto kabisa as if mlihalalisha mahusiano kwa wazazi na jamii. Mwishowe mambo yakienda kombo mnasema Ndoa ni mateso, swali ni uliolewa?
 
Sio lazima uandaliwe mazingira. Umepelekwa ahule mpaka chuo kikuu sasa hapo unataka mazingira ganj labda mengine kamanda?
Sio kila mtoto anakua na uwezo wa kuingia mtaani na kupambana wengine mpaka washikwe mkono.

Zamani wazee wetu walikua smart sana kwenye kuwajua tabia watoto wao, ambae mwenye uelekeo wa kusoma atapelekwa shule nzuri za private mpaka mambo yake yaende sawa na Kwa wale ambao mambo ya shule hayapandi kichwani atakua mazingira ya home anasaidiana na mzee kuchunga ng'ombe na kulima baada ya mda anaoa home wanampa shamba na mifugo kidogo siku zinaenda maisha yake yanakua vzr
 
Ni kwel uko sahihi kamanda
 
Kutaka urahisi wa maisha ndio sababu iliyowafanya waende shule in the first place ili wapate ajira wapate mali haraka sasa mission ndio imeshakuwa impossible lazima wachakae kiakili na kimwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…