Mabinti wahitimu wa vyuo Amkeni

Mabinti wahitimu wa vyuo Amkeni

Habari za muda huu wana jamvi


Naandika uzi huu nikiwa kwenye daladala nikirejea nyumbani kutoka kwenye "mihangaiko" ya Kila siku
Ndani ya daladala nmekaa karibu na wakina mama wawili wakipare(nimesikia wakiongea kipare). Hawa kina mama wanaelezana kuhusu tabia mbaya za mabinti zao waliohitimu vyuo ambao umri unaenda na hawajapata kazi Wala hawajachumbiwa.

Kinachowauma zaidi ni tabia ya Hawa "mabinti" kushinda ndani na kutizama movie muda wote badala ya kutoka nje watembee tembee huwenda wakakutana na "ngekewa".

Namnukuu mmoja akisema "Yani Bora wa kwako hata kanisani anaenda, Mimi huyu wangu hatoki hata kwenda dukani hataki, hana hata marafiki akatembee huko anaweza akapata mume njiani lipo lipo tu"

Wadogo zangu wa kike jitahidini kutembea tembea mama zenu wanataka muolewe mtazeekea ndani.
Nipe namba za hao mabinti...
 
Ushauri murua. Kwa kuwa wamehitimu vyuo na wanadoda nyumbani bora wachangamkie fursa ya kuolewa chapchapu wapate watoto huku wakiendelea kutafuta ajira tayari wakiwa ndani ya ndoa, watakuwa wamepunguza stress upande mmoja huku wakijishughulisha na ujasiriamali/kilimo. Ila waolewe na wanaume ambao wataheshimu taaluma zao na watawapenda kwa dhati
Nakazia ujumbe wako mkuu
 
Wangejua wenzao kwa miaka mitatu/minne chuo walishaolewa nakuachika mara 3 + michepuko juu hata wasingesema.

Hao ni wanandoa wastaafu. Ni akina Shusho Jr.

Kwa tabia ninazoziona vyuoni, nitakuwa wa mwisho kushawishika kuoa graduate, japo wapo wachache sana waliotulia.
 
Wow! Unaishi kwenye jamii gani ambayo wanaume wote wameshajipata na wako tayari kuoa na kubeba majukumu ya kifamilia kikamilifu?? Sio hii jamii ambayo wanaume pia wanastruggle kujitafuta kwa zaidi ya 15 years?

Unaamini kila anayepigania kuolewa basi atafanikiwa kuolewa? Bahati isipokuwa yake akawa hajaolewa je??

Ukiolewa ni guarantee ya kutimiziwa mahitaji yako yote? Have you ever heard women who are single mothers although they are married???

Come on, una binti? Wadogo wa kike je? You can do better with them, ndoa inaweza isiwe destiny, lakini as long as huyu binti yuko hai atatakiwa kumove around, kula, kuwa na makazi etc....... na hayo yanapatikanaje? Lazima kila mtu awe na kipato cha kulipwa au kujilipa!
Nyie mna added advantage ya " kupeleka mbususu sokoni" ndo maana unaongea "Lazima kila mtu awe na kipato cha kulipwa au kujilipa!"
 
Waoaji ndio ninyi mna ajira za kuwapa sio? What a joke!!
Wewe binti kiziwi ni mwanaharakati au? Unaishi mitaa hipi? Piga hesabu ya kawaida ya kuchukua nyumba 20 hapa mtaani kwako na angalia chanzo chao cha kipato kwa asilimia kubwa kinatoka kwa mama au baba! Don't underestimate wanaume! Still probability kubwa ya mwanamke kuishi na kupata angalau kwa uchache mahitaji yake ya msingi LAZIMA awe connected na mwanaume; ama kwa njia ya ndoa, mchepuko, au "social engineering". "Social engineering" nikiwa na maana njia za kiulaghai na kitapelitapeli kujipatia kipato kutoka kwa mwanaume
 
Kama kuna mwenye GPA kuanzia 4 atoke nimuoe
Niliwahi kuleta andiko hapa nikasema: watu wanakalili kuwa ukisoma mpaka chuo ukapata degree ndo utatoboa kirahisi! SIO HIVYO nyie vijana! Hawa wanasiasa wamewadanganya mkaingia kingi. Kama uwezo wako wa akili haukupi uhakika wa kupata GPA ya kuanzia 4.2 mpaka 5.0 usiende Chuo. Unapoteza muda, umri na rasilimali za wazazi maana ukimaliza ajira hakuna. Pia angalia unaenda chuo kusomea course hipi? Kuna course za "kindezi" <kwa lugha ya vijana> Hizo course za kindezi hata ukipata GPA kali msoto ni palepale sembuse GPA za "pass &lower second"?
 
Wewe binti kiziwi ni mwanaharakati au? Unaishi mitaa hipi? Piga hesabu ya kawaida ya kuchukua nyumba 20 hapa mtaani kwako na angalia chanzo chao cha kipato kwa asilimia kubwa kinatoka kwa mama au baba! Don't underestimate wanaume! Still probability kubwa ya mwanamke kuishi na kupata angalau kwa uchache mahitaji yake ya msingi LAZIMA awe connected na mwanaume; ama kwa njia ya ndoa, mchepuko, au "social engineering". "Social engineering" nikiwa na maana njia za kiulaghai na kitapelitapeli kujipatia kipato kutoka kwa mwanaume
Sikumbuki hii discussion ilianzia wapi, lakini may be I was just being sarcastic. Lakini pia sifurahii mabinti kuambiwa watafute ndoa kabla ya kujitafuta angalau sio kwa viwango hivyo.... hata tu kwa kuanzia.

Kuna usemi siku hizi tunawauliza, usipoolewa... plan B yako ni ipi!??

Yes mimi ni mwanaharakati, lakini haimaanishi nawadogosha wanaume, usinilishe maneno bwana! Tena kati ya vitu wanaume wametuzidi, ni nguvu za mwili, ushapu na ujanja.... mwanaume na mwanamke mkifanya biashara moja au mkafanya kazi yenye mshahara mmoja atakuzidi kipato na maendeleo mwisho wa siku....

Maana yangu umeielewa?
 
Back
Top Bottom