mbona siielewi hii video.... wanahamasisha ngono au kampeni!! "ETI LILE FATAKI LAKO VIPI "....
Kwa kuwa mimi ni mtaalam wa communications, nitafafanua nia mbaya iliyotumika kumpaka matope Mbowe na chama chake, CHADEMA, kama ifuatavyo:
1. Kwanza, kuna innuendo (dhana mbaya) kwamba "lile fataki lako" ambalo ni la "CHADEMA", yaani "Mwenyekiti wa CHADEMA", Freeman Mbowe, anajihusiha na vitendo vya kushiriki ngono na "watoto", kwani kwenye picha, ni dhahiri kwamba hawa ni watoto, tena ambao hawazidi umri wa miaka 22! Ni watoto.
2. Dhana ya pili ni kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA anachukua Shs. Milioni 10 kati ya Shs. Milioni 60 za ruzuku inayotolewa serikalini kwa CHADEMA. Je, kuna ushahidi wowote juu ya hili? Je, ni kweli?
3. Dhana ya tatu ni kwamba, Shs. Milioni 10 kati ya Shs. Milioni 60 i sawa na asilimia 16-17.
4. Dhana ya nne ni kwamba, kwa mujibu wa madai hayo, kutoka kwenye pato la taifa, CHADEMA inachukua Dola Milioni 400, kwa mtazamo wa mgao kutoka kwenye GDP (Gross Domestic Product, au Pato la Taifa).
Napenda kuwajibu hawa mafisadi kama ifuatavyo:
1. Kuhusu hao mabitinti, WAMEJIDHALILISHA wenyewe - kwa umalaya wao - kwani, kutokana na ukweli kwamba WAMELIPWA ili kupayuka maneno yasiyo na msingi, ambazo ni kashfa kubwa, wamedhihirisha kwamba wao ni mashabiki wa matendo ya UFATAKI! Kwa hiyo, kama ni maigizo, walikuwa WANAFANYA KWELI, kwamba wao wanashiriki ngono na watu wazima! Madai ya kwamba Mbowe anajihusisha na vitendo hivyo hayana msingi, kwani hakuna ushahidi wowote ule uliotolewa, wa maandishi au picha. Hii ni CHARACTER DEFAMATION, Mbowe anaweza kuamua kumchukulia hatua yeyote yule ambaye amediriki kusambaza tangazo hili chafu, au hata (kwa mtazamo wa ushahidi wa mazingira), kuishtaki mahakamani CCM na kudai fidia ya kuchafuliwa jina. Kwa hao mabinti, hawa ni sehemu ya KIZAZI KILICHOPOTEA (GENERATION LOST), na kwa upande wa Tanzania, WAKO WENGI wa aina hii! Tusitarajie lolote jema kutoka kwao! Wamepotea njia, kamwe hawatarejea kwenye mstaari! IMEKULA KWAO!
2. Nijuavyo mimi, chama chochote cha siasa hupata ruzuku kutokana na uwingi wa wabunge wake na madiwani wake. Ushahidi unaotakiwa hapa ni kwamba ITHIBITISHWE kwamba CHADEMA inapokea ruzuku ya Shs. Milioni 60 kila mwezi, na ushahidi huu anapaswa kuutoa Katibu wa Bunge na/au Msajili wa Vyama vya Siasa. Pili, ithibitishwe, kwa mujibu wa Kanuni na/au Katiba ya CHADEMA, kwamba Mwenyekiti wake anastahili kulipwa Shs. Milioni 10 kila mwezi, kama mshahara wake, na uthibitisho huo ufanyike kwa kutumia hati rasmi za malipo za CHADEMA. Vinginevyo, hii ni kashfa nzito, ambayo inakwenda moja kwa moja mahakamani.
3. na 4. Hizi nazijibu kwa pamoja. HAKUNA USHAHIDI uliooneshwa kwamba CHADEMA ina haki ya kupata Dola Milioni 400, ambazo ni asilimia 16-17 za Pato la Taifa. HAKUNA USHAHIDI wa moja kwa moja kuihusisha CHADEMA na malipo hayo, kwani, HAKUNA USHAHIDI wala HAKUNA SHERIA iliyopitishwa na Bunge kuidhinisha vyama vya siasa kulipwa kutokana na pato la taifa. HAKUNA. Kama CHADEMA wangekuwa wanapokea Dola Milioni 400, hata kwa mwaka, kama ruzuku, hawangekuwa na haja ya kudai mabadiliko serikalini, wala kugombea urais, kwani pesa hizo zingeweza kutekeleza ilani yote ya uchaguzi, na pesa nyingi kubakia. Dola Milioni 400 ni takriban sawa na Shs. Bilioni 700 za Kitanzania!
Aliyeandika "script" ya tangazo hilo la kifisadi ni mtu anayejiona kuwa ni MJANJA, kumbe ni mpumbavu! Najua, wapo watu WATAKAOAMINI kwamba ni kweli, malipo ya Mbowe ni sawa na Dola Milioni 400 kwa mwezi. Huu ni ujinga uliopitiliza hadi kufikia ujuha na uzuzu, hatimaye kuwa upumbavu na upunguani! Mtu mwenye akili timamu hawezi kutoa madai yasiyo na kichwa wala mguu kama haya!
Mimi ni mchumi, na hoja hii ya GDP haioneshi uhusiano wa moja kwa moja kwa CHADEMA na Pato la Taifa la Tanzania. CHADEMA inahusika kwa namna gani na GDP ya Tanzania?
Ama kweli, maji yameifika shingoni CCM! Inatapatapa, inatapatapa sana, na kadri inavyozidi kutapatapa, kumbe ndivyo inavyozidi kuharibu!
Huu ni mfano mwingine wa jinsi ujinga unavyopitilia hadi kuwa UPUNGUWANI na UHAYAWANI! Haiyumkini tukatarajia UONGOZI BORA kwa watu wanaodiriki kusema uongo kama huu!
Wanasheria wangu, Tundu Lissu na Mabere Marando, mna kazi ya kuipeleka CCM kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) na pia Mahakama Kuu, kupinga ukiukwaji wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi na kudai fidia!
-> Mwana wa Haki
P.S. Unaweza kuwadanganaya watu wachache mara chache, lakini huwezi kuwadanganya watu wote mara zote!