Mabondia 19 wa Afrika kupanda ulingoni katika Nusu Fainali ya Jumuiya ya Madola

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Vita ya kutumia akili, kasi, uvumilivu na nguvu sasa imeshika kasi ambapo mabondia 19 wa Afrika wameingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya ndondi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, Jumamosi Agosti 6, 2022 kwenye Ukumbi wa Nec, Birmingham.

Nigeria inaongoza kwa kuwa na mabondia wanne, Ghana na Msumbiji zna mabondia watatu, Tanzania, Zambia na Afrika Kusini zina mabondia wawili wakati Botswana, Mauritius na Uganda zina mabondia wawili.

Mtanzania Kassim Mbundwike atapanda ulingoni kupigana na Tiago Muxanga wa Msumbiji, wakati Mtanzania mwingine Yusuf Lucasi Changalawe atazichapa na Sean Lazerini wa Scotland.

Mapambano ya wanza yanatarajiwa kuanza Saa 4.30 asubuhi (muda wa Birmingham) ambapo mabondia watano wa Afrika watakuwa ulingoni.

Kassim Selemani Mbundwike

Yusuf Lucasi Changalawe​
 
Saa ngapi bosi unatoa habari haijakamilika? Ujue kuna wengine ni wapenzi wa hii michezo iliyosahaulika Tanzania na tangu mashindano haya ya madola yameanza tunakesha kumwagilia roho zetu kwa kuangalia Tv ya Kenya iitwayo KBC maana Tv za bongo hawana habari wala hawajui kuna watu wanangangana huko wakiwa wamebeba bendera ya nchi. Tv za bongo na redio wako bize kuanzia asubuhi hadi usiku na Simba day, Yanga day , manara nk
 
Kila lakheri kwao warudi na medal ya dhahabu au silver pia hata shaba si mbaya
 
Hii bongo kuna sehemu tumejichanhanya. Mabaunsa kibao mjini, wanalinda wasanii wa kike tuu, hata kwenda kurusha tufe nchi ipate medali hakuna? Au yamejaa upepo tu ?
 
Kila lakheri kwao warudi na medal ya dhahabu au silver pia hata shaba si mbaya
Shaba ni hakika tayari 100%
Tuombe washinde itakuwa fedha 100%
Coz fainali ukishinda gold ukishindwa fedha na semi final ukishindwa shaba unachukua
 
Wasimsahau Mandonga tafadhali ...

tuko nyuma yake mpaka afie ulingoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…