Mabondia wabongo wamemuogopa Hassan Mwakinyo?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Wiki chache zilizopita kila mmoja ambaye ni shabiki wa masumbwi bila shaka alisikia tambo za mdigo kwamba kwa hapa bongo hakuna bondia yoyote wa uzito wake anayeweza kupigana na yeye round 10 na akafanikiwa kuzimaliza salama.

Mdigo akaendelea kubwata kwamba mabondia wote hapa bongo ni wanawake tu si lolote wala si chochote, kama kuna bondia anabisha yeye si mwanamke basi apigane na yeye round 10 na kila round watapigana kwa dakika 5, kama kuna bondia anajiamini basi aende wapigane na akifanikiwa kuzimaliza hizo 10 rounds basi atamlipa milioni 5 ( laki 5 kwa kila round).

Kwa kifupi mpaka sasa sijaona bondia yoyote aliyejitokeza kukubali kupigana na Mwakinyo hivyo ni uthibitisho tosha kweli wao ni wanawake maana wamemuogopa na hawana la kumfanya kabisa.

Cha ajabu Mfaume Mfaume alijitokeza tu kutupa umbea kwamba jamaa maneno ya shombo yanamtoka kisa Kuna bondia kutoka tanga alimzidi kete Mwakinyo licha ya gharama alizotumia kumsomesha huyo binti akaambulia patupu na binti kuchukuliwa na bondia mwingine ndo maana Mwakinyo akaona awakatae mabondia wenzake huko tanga akihisi walisamsagia kunguni Ili demu amkatae.

Yote kwa yote sisi mashabiki tunachotaka kuona bondia yoyote wa bongo kujitosa kupigana na Mwakinyo na sisi tutakuwa tayari kulipia hilo pambano hata kama litakuwa pambano la maonyesho (Exhibition Fight)

Tambo alizoleta Mwakinyo kwenye boxing ni za kawaida sana na ndizo zinazotakiwa kwenye boxing ,maana boxing ni mchezo wenye majivuno na maneno yenye kuudhi baina pande zote mbili ili kuvutia zaidi watazamaji na mauzo ya tiketi yawe makubwa achilia mbali masuala ya Pay Per View (PPV).

Hata mabondia wa huko mbele ni kawaida sana kuleta tambo kama hizi tena wao huenda mbali zaidi mpaka kuleta ubaguzi wa rangi, matusi ya nguoni mpaka kwa wazazi lakini mabondia hao hao nyuma ya pazia ni washkaji wakubwa Mf Deontay na Fury ilivyokuwa.

Mabondia wa bongo jitokezeni basi mtu prove wrong kwamba kweli nyie sio wanawake kama alivyowaita Mwakinyo.
 
Na wewe unaingia kwenye line za Mwakinyo. Unadhani hilo linawezekana?

Anaongea kwa sababu anajua fika serikali haiwezi kukubali kuona watu wanapigana na yenyewe ikakaa kimya.

Kama anaona kweli, wapange pambano rasmi linalotambulika. Kitu ambacho anakikimbia kwa madai ya kushusha ranking.
 
Nakumbuka kuna kipindi Cosmas Cheka alikuwa ana pambano hivyo akamuomba Mwakinyo Sparring ili ajiweke sawa kuelekea hilo pambano lake.

Mwakinyo akamwambia sawa haina shida mapema tu nitaibuka kwako tufanye sparring.

Kweli bwana , Mwakinyo kesho yake akatimba kwa Cosmas mapema tu, ila muda amefika Cosmas alikuwa ametoka kidogo.

Mwakinyo alimsubiri Cosmas mpaka alipofika na kipindi hicho Cosmas Cheka ni wa moto sana.

Kwenye hiyo sparring Cosmas alipigwa kama ngoma 🤣🤣🤣🤣🤣yeye kila akirusha holaaaa.

Cosmas ikabidi asalimu amri kwa Mwakinyo.

NB:Kwenye pambano lake official Cosmas alishinda
 
Sio lazima iwe official fight , wanafanya tu exhibition fight hivyo bondia yoyote atakayepigwa rekodi yake haiwezi kuathirika kivyovyote.
 
Huu ni uzushi mkuu! Jamaa hajasomesha demu na hana pigo za kushobokea wanawake kabisa..
Wewe unajuaje?

Kwani kila anachofanya nje ya ulingo lazima akiweke bayana?

Sasa ubuyu tumepewa huo na mtu ambaye yupo kwenye kazi moja na yeye .

Na Mfaume hawezi kuibuka tu from nowhere aanze kumsingizia shutuma kama hiyo.
 
Wewe unajuaje?

Kwani kila anachofanya nje ya ulingo lazima akiweke bayana?

Sasa ubuyu tumepewa huo na mtu ambaye yupo kwenye kazi moja na yeye .

Na Mfaume hawezi kuibuka tu from nowhere aanze kumsingizia shutuma kama hiyo.
Sasa kuwa wote kwenye kazi moja ndio kwamba anajua ya mwenzie hapana! Mimi nakueleza yenye uhakika, Namjua vizuri Hassani.
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…