Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Wiki chache zilizopita kila mmoja ambaye ni shabiki wa masumbwi bila shaka alisikia tambo za mdigo kwamba kwa hapa bongo hakuna bondia yoyote wa uzito wake anayeweza kupigana na yeye round 10 na akafanikiwa kuzimaliza salama.
Mdigo akaendelea kubwata kwamba mabondia wote hapa bongo ni wanawake tu si lolote wala si chochote, kama kuna bondia anabisha yeye si mwanamke basi apigane na yeye round 10 na kila round watapigana kwa dakika 5, kama kuna bondia anajiamini basi aende wapigane na akifanikiwa kuzimaliza hizo 10 rounds basi atamlipa milioni 5 ( laki 5 kwa kila round).
Kwa kifupi mpaka sasa sijaona bondia yoyote aliyejitokeza kukubali kupigana na Mwakinyo hivyo ni uthibitisho tosha kweli wao ni wanawake maana wamemuogopa na hawana la kumfanya kabisa.
Cha ajabu Mfaume Mfaume alijitokeza tu kutupa umbea kwamba jamaa maneno ya shombo yanamtoka kisa Kuna bondia kutoka tanga alimzidi kete Mwakinyo licha ya gharama alizotumia kumsomesha huyo binti akaambulia patupu na binti kuchukuliwa na bondia mwingine ndo maana Mwakinyo akaona awakatae mabondia wenzake huko tanga akihisi walisamsagia kunguni Ili demu amkatae.
Yote kwa yote sisi mashabiki tunachotaka kuona bondia yoyote wa bongo kujitosa kupigana na Mwakinyo na sisi tutakuwa tayari kulipia hilo pambano hata kama litakuwa pambano la maonyesho (Exhibition Fight)
Tambo alizoleta Mwakinyo kwenye boxing ni za kawaida sana na ndizo zinazotakiwa kwenye boxing ,maana boxing ni mchezo wenye majivuno na maneno yenye kuudhi baina pande zote mbili ili kuvutia zaidi watazamaji na mauzo ya tiketi yawe makubwa achilia mbali masuala ya Pay Per View (PPV).
Hata mabondia wa huko mbele ni kawaida sana kuleta tambo kama hizi tena wao huenda mbali zaidi mpaka kuleta ubaguzi wa rangi, matusi ya nguoni mpaka kwa wazazi lakini mabondia hao hao nyuma ya pazia ni washkaji wakubwa Mf Deontay na Fury ilivyokuwa.
Mabondia wa bongo jitokezeni basi mtu prove wrong kwamba kweli nyie sio wanawake kama alivyowaita Mwakinyo.