Maboresho Mwongozo biashara ya Kaboni yaiva

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeanza kufanyia maboresho Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni za mwaka 2022 ili ziweze kuwatambua na kuwanufaisha wakulima na wafugaji nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ( Chilo) wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Jacqueline Ngonyani Msongozi bungeni jijini Dodoma Juni 28, 2023.

Amesema kanuni hizo zinalenga kuhakikisha kuwa jamii, wadau mbalimbali wanaohusika na biashara hiyo ikiwa pamoja na Serikali kunufaika kikamilifu kutokana na faida zake.

Aidha, Mhe. Khamis ameeleza kuwa Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kutoa elimu ya mazingira kwa umma ikiwemo ya Biashara ya Kaboni.

Amesema ni matumaini ya Serikali kwamba, kupitia jitihada hizo wananchi wataweza kupata uelewa na kunufaika na biashara hiyo wakiwemo wakulima na wafugaji.

Naibu waziri amefafanua kuwa Biashara ya Kaboni ni moja ya mbinu za kupunguza uzalishaji wa Gesijoto (Mitigation) ambayo iliridhiwa katika itifaki ya Kyoto ikizitaka nchi wanachama kupunguza uzalishaji wa gesijoto iliyorundikana angani.

Hali kadhalika amesema kuwa biashara hii ipo katika masoko ya aina mbili ambayo ni Soko la hiari/huria (Voluntary Carbon Market) na Soko la Umoja wa Mataifa (Official Carbon Market).

Pamoja na Mwongozo huo, tayari Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo, Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Wizara zote za kisekta pamoja na taasisi zake, Wakuu wa Wilaya wote, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mkoa na kwa wadau mbalimbali.

Itakumbukwa Juni 19, 2023 Ofisi ilitoa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari. Semina hiyo ililenga kujenga uelewa kuhusu Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni.

Fzsq248XoAAo2Zt.jpg
 
Dahhh....Nikipewa mtihani niwataje Mawaziri na wasaidizi wao kwenye hii serikali, nitafeli vibaya sana. Huyu kwakweli ndio nimemfahamu sasa.
 
Mkuu hivi haya maeneo tutakayo toa kwaajili ya hewa ukaa ndo tutakuwa tumeyauza moja kwa moja au maana hakuna elemu ya kutosha imetolewa
 
Huyauzi bali unayahifadhi na unalipwa kwa kuyalinda na kwa kuyahifadhi kulingana na namna ambavo unayahifadhi.
 
Mkuu hivi haya maeneo tutakayo toa kwaajili ya hewa ukaa ndo tutakuwa tumeyauza moja kwa moja au maana hakuna elemu ya kutosha imetolewa

Hii biashara ya hewa ukaa au carbon credits business ni somo pana sana sisi wengine tuliosoma course za maliasili chuo kikuu tulijifunza complete package na Ina credit hours za kutosha kabisa.

Watanzania wanahitaji somo kubwa ili waweze kulielewa bahati mbaya sana nilikuta kwenye page za social media za socialite mmoja bongo anafanya upotoshaji wa waziwazi niliumia sana.

Iko hivi kiongozi, baada ya nchi zilizoendelea kukosa misitu mingi kutokana na maendeleo ya viwanda, kiasi cha hewa chafu isiyo rafiki zikiwemo carbon monoxide, dioxide na Chlorofluorocarbons carbons, CFC’s zinapelekea uharibifu wa Ozone layer ambayo inafanya kazi Kama shield/kikingo cha miale ya jua kutufikia moja kwa moja na hivyo kuwa na athari mbalimbali Kama vile kuongezeka kwa joto duniani na mabadiriko mbalimbali ya tabia nchi.

Sasa wenzetu huko duniani wakaona waje na wazo la kuzifaidisha nchi zilizo na misitu haswa ya asili na kupandwa kwa sababu miti inasaidia sana kuondoa carbon dioxide na circulation ya hewa hivyo kupunguza ozone layer depletion through emission of carbon gases. Kwaiyo inapimwa misitu yako in metric tonnes yanafanyika mahesabu then unapewa pesa ili kusaidia juhudi za uhifadhi wa misitu hiyo na kuiendeleza na kupanda misitu mingine ili Haya mabadiriko ya tabia nchi yapungue.

Sasa hapo swala la kuwauzia sijui misitu linatoka wapi? Wao wanachochea uhifadhi zaidi sababu kwenye nchi zao tayari uharibifu mkubwa umeshafanyika kutokana na maendeleo ya viwanda na matumizi makubwa ya magari ya diesel petrol. Sasa Vigezo na masharti vikizingatiwa unagundua nchi yetu ni mnufaika mkubwa wa biashara hii tayari serikali kupitia agency za uhifadhi za TFS na TAWA wameashaingia makubaliano ya awali, MoU na kampuni zinazofanya biashara ya hewa ukaa na kwa habari nilizoziona TAWA ilipata kiasi cha billion 8 kusaini MoU hiyo. Fedha hizo zinaingia serikalini na kuendeleza juhudi za kiuchumi na kadharika.
 
Je nikiingia mataba wa kuuza hewa ukaa kwenye shamba langu naweza vunja mkataba nikitaka kujitoa
 
Je ni namna gani mtu binafsi naweza kujngia kwenye biashara hii ya carbon credit nikiwa na hekari zangu chache. Maelezo tafadhali
 
Back
Top Bottom