Maboresho ya mita za luku kwa wateja wa kanda ya kati na kanda ya kaskazini

Kadodo1

Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
25
Reaction score
24
Jumamosi, 17 Agosti 2024
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuhusu zoezi la maboresho ya mfumo wa mita za Luku ambapo sasa ni zamu ya mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Zoezi hilo litaanza kufanyika katika mikoa hiyo kuanzia tarehe 26 Agosti 2024. Maboresho haya yanalenga kuendana na viwango vya mifumo ya LUKU vya kimataifa na kuongeza ufanisi na usalama wa mita za LUKU nchini.

Mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe tajwa atapokea tarakimu kwenye makundi matatu, kila kundi likiwa na tarakimu ishirini. Kundi la kwanza na la pili la tarakimu yatakuwa kwa ajili ya maboresho na kundi la tatu la tarakimu litakuwa ni la umeme ulionunuliwa.

Mteja ataingiza tarakimu za kila kundi kwa kufuata mpangilio unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa simu (sms) na kila atakapoingiza kundi moja Mteja atapaswa kubonyeza alama ya kukubali ya # au mshale wa kukubali na hapo atakuwa amefanikiwa kuboresha mita yake na kupokea kiwango cha umeme alichonunua.

Zoezi hili ni bure na litafanyika mara moja tu kwa mteja, baada ya kufanya hivyo mteja atakuwa amefanya maboresho hayo na ataendelea kupata kundi moja la tarakimu ishirini kila anapofanya manunuzi ya
umeme.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia namba ya huduma kwa wateja 0748 550 000 au namba za huduma kwa wateja mikoa husika au WhatsApp 0748 550 000 na mitandao yetu ya kijamii.

Shirika linawahimiza wateja wake wote kuendelea kununua umeme ili kuweza kufanya maboresho hayo kwenye mita zao ambapo ukomo wa zoezi hili katika maeneo yote nchi nzima utakuwa tarehe 24/11/2024.
Imetolewa Na;

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA
TANESCO-MAKAO MAKUU
DODOMA
1b27b243f2644f4fb4cebb177c7d7c77.jpg
 
View attachment 3072958
Hivi na ulaya kwenye maghorofa marefu sana nako wanapanda kwenye stuli kubonyeza kwenye mita?
 
Mteja mpya anatakiwa kuingiza vipi kulipia umeme wa kuanzia kama ndio kafungiwa kwa mara ya kwanza
 
Back
Top Bottom