Maboss wa JamiiForums kuna gari lenu hapa la umeme: Rolls Royce Spectre

Maboss wa JamiiForums kuna gari lenu hapa la umeme: Rolls Royce Spectre

Katika press conference mwaka 2010, wakati iPhone 4 imetoka, Steve Jobs alivyoulizwa kama Apple wana mpango wa kutoa simu kubwa alijibu "no one is going to buy a big phone", akiamini kwamba size ya 3.5 inch ni perfect kwa simu. Muda huo ilikua kijembe kwa Samsung S1 iliyokua na 4 inch.

Kwa muda huo CEO wa Apple aliamini kwamba size kubwa ya screen sio future. Ni kama ambavyo miaka michache iliyopita, makampuni mengi ya magari yalivyoulizwa kuhusu kuhama kutoka ICE kwenda EV waliona kama haina haja kabisa, ila sasa kila mtu anaangalia EV au PHEV.

Na ndio kilichotokea kwa mkali wa luxury cars kutoka Manchester, United Kingdom, Rolls Royce alivyoamua kuingia EV mazima na kuanza na Rolls Royce Spectre.

View attachment 3054546View attachment 3054547
Hii ni grand tourer (GT) coùpe ya milango miwili kutoka kwa RR ilioanza kuuzwa mwaka 2024 na ndio gari ya kwanza ya umeme kutoka kwa hawa wakali.

View attachment 3054548

Hii gari imechukua platform ya Rolls Royce Phantom na Cullinan. Ili chuma ni kubwa sana, Pamoja na kua na milango miwili tu ila ni refu.

Kwa mfano, urefu wa Toyota Crown ya 2007 ni mita 4.8 ila hii ina urefu wa mita 5.5 ikiwa imemzidi Crown sentimita 70. Kwa lugha nyepesi rula mbili na kidogo za mwanafunzi.

View attachment 3054549
Pamoja na kutokua na engine ya V12 kama tulivyozoea, hii EV sio ya kuichukulia poa, kwani inatoa jumla ya horsepower 577, kutoka kwenye motors mbili (hizi wametengenezewa na BMW) zitakazosaidia kwenye AWD.

View attachment 3054550
(Pichani juu kushoto BMW i7 (electric version ya BMW 7 series) against pacha wake Rolls Royce Spectre wakichajiwa) ambae wameshare motors na baadhi ya technical features.

Battery yake ni kubwa, ina 102 kWh lakini itakupeleka maximum kilometa 530 tu ikiwa full charge. Najua utajiuliza kwann battery kubwa ivyo hafu range ndogo, hapa mchawi wetu ni uzito. Hii chuma ina uzito wa Kilo 2,975 hivi.
View attachment 3054551

Kwa reference, Tesla Model 3 2024 ina battery lenye ukubwa wa 82 kWh ila ina maximum range hadi ya kilometa 584, na uzito wake ni Kilo 1,830 tu. Karibia Kilo 1,000 pungufu.

View attachment 3054552

Ataivyo matajiri mtakaomiliki hii chuma sidhani kama mtataka kusafiri more than 500 km, otherwise mtachukua helicopter zenu.

View attachment 3054553

Bei yake ya kuanzia ni $750,000 na itapanda zaidi kutegemea na options utakazochagua.

Mkileta tutaomba ata lift.
Hybrid cars ndio future huko US mauza ya hybrid yameongezeka ya full electric yameshuka
 
Hybrid cars ndio future huko US mauza ya hybrid yameongezeka ya full electric yameshuka
Kwa kutumia kigezo cha nchi moja Marekani sawa. Ila on average Dunia nzima, EV kampush Hybrid parefu sana.

BTW hybrid, plugins, EV, REEV mimi zote nazipa go-ahead.
 
Back
Top Bottom