Mabucha tofauti......

Mabucha tofauti......

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Well...well..well....nani anaamini kwamba hata “Bucha likiwa tofauti nyama ni ile ile?!“ Na wale wanaoamini tofauti hata wasiishe kubadili mabucha kila siku ni nini haswa hua kinawashawishi kuamini tofauti?

Ukweli ni kwamba nyama ya ng‘ombe ni ya ng‘ombe...ya kuku ni ya kuku...ya sungura ni ya sungura na haziwezi kuwa na ladha ya aina nyingine ya nyama.Tofauti kubwa ipo kwenye MIFUPA...STEAK na MAFUTA.Hivi ndivyo vitu vikuu vinavyoweza kufanya ladha itofautiane kidogo.Alafu kuna uhifadhi (kwa hisani ya mutu moja yenye kitambi ila inaficha kwa kutochomekea shati) ....kuna mabucha yanayowekwa katika hali ya usafi na mengine yako hovyoo tu...japo hili halibadili ladha linaweza kuongeza au kupunguza hamu ya kula nyama uliyonunua wewe bila kuzingatia usafi wa ulipoinunua.

Pamoja na hayo yote niliyosema ukweli unabaki pale pale kwamba tofauti ya bucha sio tofauti ya nyama.Kwahiyo kwa wale wanaoamini nyama ya kwa Mrombo inatofautiana ya kwa Kassimu ambayo nayo inatofautiana na ya kwa Moleli wakati zote ni ng‘ombe msijidanganye.

Unachotakiwa kufanya ni kujua unapendelea nini zaidi kati ya MAFUTA..STEAK na MIFUPA kisha uchague kimoja.Zingatia afya na hali yako kwenye kuchagua...kama una presha sijui na BP kaa mbali na mafuta...kama huna meno usitake kuumiza fizi zako kwa mifupa na kama unaweza kuafford steak go for it.

Neway ukishachagua nyama yako toka kwenye bucha linalokuridhisha kwa usafi na bei sasa zingatia kilicho muhimu na kinacholeta tofauti ya kweli....MAPISHI.Hapa ndio wengi wanapokosea...na ndio maana hata baada ya mabucha manne matano bado mtu anakua anahangaika kwasababu haoni tofauti kwasababu popote pale anaponunua mwisho wa siku anarudia mapishi yale yale ya jana.Wewe kama mpishi kua MBUNIFU...sio ukishakula unaanza kulalama chakula hakikunoga sababu sijui chumvi ilizidi...mara sijui kilikua kimepoa and the likes wakati wewe ndo uliyekua jikoni.Usijizoeshe mchemsho tu au mkaango tu kila siku...hayo sio mapishi pekee.Jaribu aina tofauti...buni...jifunze FURAHIA.

Ni sawa na ule msemo wa mchele mmoja mapishi mengi...utazunguka weeeee ila mwisho wa siku kama sio mpunifu utamaliza duara bila jipya.

PS...sitaki maswali ya kama usome katikati au pembeni ya mstari...kua mbunifu.
 
Nitarudi b'dae ila mdogo wangu lizzy hujambo?
 
so mwisho wa siku kutafuta mabucha tofauti ni sahihi

since mabucha mengine machafu,mengine masafi..
mengine nyama mifupa mingi,mengine nyama hazina mafuta
nyingine nyama ya juzi,nyingine ya leo....

need i say more??????
 
Lizzy we umejulia wapi mambo ya Bucha na nyama tofauti? njoo shinyanga ule Mbogo na Swala uone kama kweli ziko sawa?
 
Well...well..well....nani anaamini kwamba hata "Bucha likiwa tofauti nyama ni ile ile?!" Na wale wanaoamini tofauti hata wasiishe kubadili mabucha kila siku ni nini haswa hua kinawashawishi kuamini tofauti?

Ukweli ni kwamba nyama ya ng‘ombe ni ya ng‘ombe...ya kuku ni ya kuku...ya sungura ni ya sungura na haziwezi kuwa na ladha ya aina nyingine ya nyama.Tofauti kubwa ipo kwenye MIFUPA...STEAK na MAFUTA.Hivi ndivyo vitu vikuu vinavyoweza kufanya ladha itofautiane kidogo.Alafu kuna uhifadhi (kwa hisani ya mutu moja yenye kitambi ila inaficha kwa kutochomekea shati) ....kuna mabucha yanayowekwa katika hali ya usafi na mengine yako hovyoo tu...japo hili halibadili ladha linaweza kuongeza au kupunguza hamu ya kula nyama uliyonunua wewe bila kuzingatia usafi wa ulipoinunua.

Pamoja na hayo yote niliyosema ukweli unabaki pale pale kwamba tofauti ya bucha sio tofauti ya nyama.Kwahiyo kwa wale wanaoamini nyama ya kwa Mrombo inatofautiana ya kwa Kassimu ambayo nayo inatofautiana na ya kwa Moleli wakati zote ni ng‘ombe msijidanganye.

Unachotakiwa kufanya ni kujua unapendelea nini zaidi kati ya MAFUTA..STEAK na MIFUPA kisha uchague kimoja.Zingatia afya na hali yako kwenye kuchagua...kama una presha sijui na BP kaa mbali na mafuta...kama huna meno usitake kuumiza fizi zako kwa mifupa na kama unaweza kuafford steak go for it.

Neway ukishachagua nyama yako toka kwenye bucha linalokuridhisha kwa usafi na bei sasa zingatia kilicho muhimu na kinacholeta tofauti ya kweli....MAPISHI.Hapa ndio wengi wanapokosea...na ndio maana hata baada ya mabucha manne matano bado mtu anakua anahangaika kwasababu haoni tofauti kwasababu popote pale anaponunua mwisho wa siku anarudia mapishi yale yale ya jana.Wewe kama mpishi kua MBUNIFU...sio ukishakula unaanza kulalama chakula hakikunoga sababu sijui chumvi ilizidi...mara sijui kilikua kimepoa and the likes wakati wewe ndo uliyekua jikoni.Usijizoeshe mchemsho tu au mkaango tu kila siku...hayo sio mapishi pekee.Jaribu aina tofauti...buni...jifunze FURAHIA.

Ni sawa na ule msemo wa mchele mmoja mapishi mengi...utazunguka weeeee ila mwisho wa siku kama sio mpunifu utamaliza duara bila jipya.

PS...sitaki maswali ya kama usome katikati au pembeni ya mstari...kua mbunifu.

Mhhhh Lizzy ngoja ninywe kahawa hapa na then nitarudi kukujibu maana ni mada nzito sana sana
 
so mwisho wa siku kutafuta mabucha tofauti ni sahihisince mabucha mengine machafu,mengine masafi..mengine nyama mifupa mingi,mengine nyama hazina mafutanyingine nyama ya juzi,nyingine ya leo....need i say more??????
Kwahiyo kujua kitu ni kichafu mpaka uonje?!Macho hayaoni pua nayo hainusi?!
 
Lizzy we umejulia wapi mambo ya Bucha na nyama tofauti? njoo shinyanga ule Mbogo na Swala uone kama kweli ziko sawa?
Magu kama hujanielewa ...sijasema nyama za wanyama wote zinafanana ila kama mnyama ni yule yule hamna jipya.Wanyama wa porini baadhi wanajulikana kwa utamu waa sio uongo.
 
Ubora wa Bucha unashambihiana na ubora wa nyama.

Kwa wale wataalamu wa nyama wanajua kabisa Postslaughter handling has a tremendous effect on the quality of meat. Nyama ikiwa kwenye bucha lenye jua bila kiyoyozi hiyo nyama hupoteza maji maji na kuwa kavu haina utamu.

Lairage time and Lairage conditions Nyama kama imening'nizwa sana buchani ubora utapungua. Nyama ikiwa buchani imewekwa vibaya na nzi wameweka makazi nasema hapana. Mchungaji lazima nitembelee bucha nyingi nipate kile kilicho bora.

Mikoa ya Mtwara, Mwanza Shinyanga na Lindi huusani Kagera, kule Katelero Bucha zao nzuri na nyama zao, nchi za Uganda, Burudi na Rwanda wanafahamika hao. Tukirudi Tanzania wapishi wazuri wa Nyama wako Zanzibar, Tanga, Tabora, Kigoma hasa Uvinza

Naangalia ubora si mradi nyama

Mch Rev Fr Masa
 
Waiting.....

Mhhh nimeshindwa kujizuia kutojibu ila hata kama ni mapishi Lizzy si unajua yanatofautiana na ndo yanayoifanya nyama iwe tamu. Kwa mwingine ataweka nyanya na vitunguu mwingine ataongeza na karoti na pilipili hoho na mwingine ataweka manjonjo mbalimbali ili kuipendezesha nyama husika. mpishi naye si unajua ni lazima awe na usafi na apike nyama yake kwa usafi maana inaweza ikawa paishi yake ni matamu na mazuri ila mpishi mwenyewe hana mvuto. Na pia si unajua tena hata upakuaji wa mpishi nao ni issue nyingine hana mvuto kwenye kukupa nyama yenyewe aliyopika so hayo yote ukichanganya ndo maana tunavuka kwenda mtaa wa tatu kutafuta bucha na mpishi mzuri
 
Back
Top Bottom