Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,442
Sasa kama hawajui kupika hii nyama kwanini aweze kupika ile nyama?, au kila nyama ina mapishi tofauti ?mwisho wa siku wanatamani nyama ya bucha la kwanza.Wengine kupika hawajui wanasingizia nyama.
Well huko kutembelea mabucha kwa mchungaji kunaendana na kuonja au kuangalia tu na kutathmini kwa macho?!Ubora wa Bucha unashambihiana na ubora wa nyama.Kwa wale wataalamu wa nyama wanajua kabisa Postslaughter handling has a tremendous effect on the quality of meat. Nyama ikiwa kwenye bucha lenye jua bila kiyoyozi hiyo nyama hupoteza maji maji na kuwa kavu haina utamu.Lairage time and Lairage conditions Nyama kama imening'nizwa sana buchani ubora utapungua. Nyama ikiwa buchani imewekwa vibaya na nzi wameweka makazi nasema hapana. Mchungaji lazima nitembelee bucha nyingi nipate kile kilicho bora. Mikoa ya Mtwara, Mwanza Shinyanga na Lindi huusani Kagera, kule Katelero Bucha zao nzuri na nyama zao, nchi za Uganda, Burudi na Rwanda wanafahamika hao. Tukirudi Tanzania wapishi wazuri wa Nyama wako Zanzibar, Tanga, Tabora, Kigoma hasa UvinzaNaangalia ubora si mradi nyamaMch Rev Fr Masa
Kwahiyo mpaka ule..uharishe ndo ujue kumbe pale sio?!
Sasa wewe kama mhusika mkuu kwenye swala zima la kupika na kuandaa mbona yote uliyosema yapo ndani ya uwezo wako kurekebisha?! Ni kiasi tu cha kuiserve nyama kwenye sahani inayovutia...juu ya meza safi na ndani ya sebule safi.Mhhh nimeshindwa kujizuia kutojibu ila hata kama ni mapishi Lizzy si unajua yanatofautiana na ndo yanayoifanya nyama iwe tamu. Kwa mwingine ataweka nyanya na vitunguu mwingine ataongeza na karoti na pilipili hoho na mwingine ataweka manjonjo mbalimbali ili kuipendezesha nyama husika. mpishi naye si unajua ni lazima awe na usafi na apike nyama yake kwa usafi maana inaweza ikawa paishi yake ni matamu na mazuri ila mpishi mwenyewe hana mvuto. Na pia si unajua tena hata upakuaji wa mpishi nao ni issue nyingine hana mvuto kwenye kukupa nyama yenyewe aliyopika so hayo yote ukichanganya ndo maana tunavuka kwenda mtaa wa tatu kutafuta bucha na mpishi mzuri
Tuwafanyeje hawa mkwe?!Mtu tatizo liko kwako ila lawama anaelekeza kwingine.mamkwe bana kuna visingizio kibao mara bucha ulilolizoe linabadili style linaanza kuleta nyama mara zimekonda sana au mifupa mingi wakati mwanzo alikuwa analeta nyama ya kiwango........kinachofuata anakwenda bucha la Kassimu nako baada ya muda anaona nyama haifai.....................mwisho anajikuta amezungukia mabucha mji mzima
wanapoipika vibaya 'hii' nyama wanahisi nyama yenyewe ndio mbaya wanaanza kutafuta 'ile' nyama. Utofauti wa nyama ni kwenye mapishi, kama leo utachemsha supu basi kesho ikaange, siku nyingine iunge. We kila siku michemsho lazima ukinai.Sasa kama hawajui kupika hii nyama kwanini aweze kupika ile nyama?, au kila nyama ina mapishi tofauti ?
Mtu anaweza akajua kupika ila asiwe mbunifu na mapishi yake.Wengine wanadhani hata chai ni sukari na majani tu...kumbe wengine siku wakitaka kitu tofauti kidogo wanaweka maziwa..limao...iliki...tangawizi...mchai chai..vanilla (kwa hisani ya BOSS) na vikorokoro vingine kibao badala ya kuanza kunywa bia asubuhi kisa ladha ya chai yake kaichoka.Sasa kama hawajui kupika hii nyama kwanini aweze kupika ile nyama?, au kila nyama ina mapishi tofauti ?
Tuwafanyeje hawa mkwe?!Mtu tatizo liko kwako ila lawama anaelekeza kwingine.
Kwani kuna haja ya kula hizo nyama, Sisi wala mbogamboga tuna afadhali. hatuchagui jani, mradi laliwa, twala. majani hayana kinyaa wala hayahitaji ufundi kupika.
Muuzaji abadili mapishi yeye ndio mpishi/mlaji!?Wewe unaenunua ndo unaetakiwa kubadili mapishi badala ya mabucha.