Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Wengi uenda tukawa tunafahamu mabwawa yaliyopo Mabibo Mwisho karibia na Chuo cha NIT, katika kipindi ambacho nimeishi maeneo ya pale karibu na yalipo Mabwawa nimekuwa nikisikia harufu kali ya kemikali lakini baada ya kudodosa huku na kule nilifahamishwa kwamba yale maji yanatoka kwenye Viwanda vilivyopo maeneo ya Urafiki.
Mabwawa hayo yapo matano ambayo yanahifadhi maji machafu na kuyatiririsha katika mwelekeo mwa yalipo makazi, ambapo ikitokea mvua zimenyesha maji hayo usambaa hadi kwenye makazi jambo ambalo ni hatari kwa afya za Wananchi.
Najiuliza kulikuwepo na sababu zipi za kuweka mabwawa hayo ingali maji hayo yanaachwa yaelekee kiholela kwenye mijereji inayokatiza kwenye makazi ya Wananchi bila kuwepo na miundombinu rafiki.
Nitoe wito kwa mamlaka ikiwemo NEMC kufuatilia kwa ukaribu suala hilo ambalo linahatarisha sana usalama wa Wananchi kupitia mazingira niliyoeleza.
Ni muhimu miundombinu ikaboreshwa kwa kuzingatia teknolojia bora ambazo zinaweza kufanya maji taka hayo kuhifadhiwa na kutiririshwa bila kuleta athari kwa wananchi.