Macelebrities kutaka kuingia kwenye siasa ni kukua au kuporomoka kwa siasa nchini?

Macelebrities kutaka kuingia kwenye siasa ni kukua au kuporomoka kwa siasa nchini?

Verdy CB

Senior Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
149
Reaction score
66
MACELEBRITIES wengi nchini wamekua wakizungumzia nia zao za kugombea ubunge 2015... Wakiwa hawana sababu nyingi... Mfano Loveness malinzi "diva" juzi kachukua kadi ya chadema na kusema nia yake.. JB pia katangaza nia yake.. Na wengine kama Mange kimambi,Briggite(ms TZ),wema sepetu na wengineo kibao... Je hii inaonyesha siasa imekua au inaporomoka kwa watu kutaka kusaka faida tu na c kwa ajili ya watu
 
ni kuporomoka kwa sababu waingiao hawana dira wala mwelekeo, tangu wajue kwenye siasa ni sehemu ya kuchuma pesa na si kwenda kujadili mstakabali wa nchi kila mtu anataka, hahaha, imagine Mhe. Wema Sepetu kipi atakachojadili kuitetea nchi yake ili hali yeye mwenyewe hajitambui. Si ajabu na Lulu naye akasema anagombea mwe!

Hivi anaweza kujadili maadili yameporomoka wakati yeye mwenyewe kwanza kajikoboa, kutembea uchi, masuala ya ngono kwake ni sifa, kuchora matatuu mwilini siamini kama kuna mzazi anayezingatia maadili atapenda mwanawe awe na tabia kama za Wema. eti huyo mtu kesho awe mbunge. Ndio maana siasa za siku hizi kweli maji taka kwa sababu waliomo wengi ni taka.

ki ukweli na huu ushabiki wa vijana wa siku hizi ambao kila uchao wanazidi kuzungusha mashuleni kinazidi kukosa ufahamu, weledi na uelewa, so tusishangae miaka ijayo aina za kina Wema wakawa waheshimiwa wetu wanaojadili mstakabali wa taifa. tusipokuwa macho miaka 50 ijayo tukuwa wote hatujitambui na hao majirani zetu wana hamu tufikie hali hiyo watutawale kirahisi.

Wazazi wajengeni watoto wenu ili angalau kizazi kijacho kijitabue. maana hichi cha sasa facebo imekiharibu.
 
Ukweli ni kuwa siasa imeporomoka na ndo maana kila mtu akipata kaumaarufu kidogo tu anafikiria kwenda huko.Sasa kama mpaka Afande sele ana ndoto za kuwa mbunge kuna Siasa tena hapo..??
 
dah hii nchi kila mtu akiwa famous kidogo tu anataka kuwa mwanasiasa.
 
Ucelebrity ndo mavi gani mpaka yakutokeni mapovu na kuwajadili hawa watu? mi nawaona watu wa kawaida tu kama wengine kwan nao pia wana haki katika nchi hii, so sioni tatizo la wao kugombea, ni wajibu wenu wapiga kura kuwachagua au kutowachagua!
 
Ndugu Yangu Verdy CB, nadhani matokea ya hilo unalo liongelea tayari unaliona Bungeni. Sasa ili uwe Mbunge Mahiri, inahitajika uwe na uwezo wa kuporomosha Matusi kadri ya Uwezo wako, Ngumi Mkononi, Kufoka kwa sana, Hasa hasa Muongozo wa Spika na hasa Kuunga mkono Hoja kwa asilimia 100% ni Ndio Sifa Muhimu za kua mbunge.
 
MACELEBRITIES wengi nchini wamekua wakizungumzia nia zao za kugombea ubunge 2015... Wakiwa hawana sababu nyingi... Mfano Loveness malinzi "diva" juzi kachukua kadi ya chadema na kusema nia yake.. JB pia katangaza nia yake.. Na wengine kama Mange kimambi,Briggite(ms TZ),wema sepetu na wengineo kibao... Je hii inaonyesha siasa imekua au inaporomoka kwa watu kutaka kusaka faida tu na c kwa ajili ya watu

Bunge la Tanzania ni sehemu ya kutokea kimaisha.
 
Kwani mbunge kama Lusinde mnadhani anaweza kumzidi ufahamu Kingwendu? Au Majuto? Kuliko kuendelea na kina Lusinde,Komba ni sawa tuu na wengine waingie

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kiukweli hali ya bunge kwa sasa inatisha,kila siku ni afadhali ya jana, mpaka inakatisha tamaa kuwaangalia hawa wabunge...
Sasa nikiimagine bungeni nkimwona wema sepetu analia katukanwa na lulu bungeni,kingwendu anamng'ong'a speaker mmmh... Cjui wanachoenda kufanya labda kusaka tu chapaaa ila kututetea NO..
 
Ndugu Yangu Verdy CB, nadhani matokea ya hilo unalo liongelea tayari unaliona Bungeni. Sasa ili uwe Mbunge Mahiri, inahitajika uwe na uwezo wa kuporomosha Matusi kadri ya Uwezo wako, Ngumi Mkononi, Kufoka kwa sana, Hasa hasa Muongozo wa Spika na hasa Kuunga mkono Hoja kwa asilimia 100% ni Ndio Sifa Muhimu za kua mbunge.

Nyerere akichungulia akaona hii hali atalia sana
 
Back
Top Bottom