Machache kuhusu Thomas Sankara

Machache kuhusu Thomas Sankara

Echazzy

Member
Joined
Jan 20, 2018
Posts
65
Reaction score
67
Thomas sankara alikua ni raisi wa Burknafaso kati ya miaka ya 1983 hadi 1987
Haya ni moja ya machache yaliyo fanywa na Thomas Sankara enzi za uongozi wake[emoji116]

[emoji117]Aliuza Mercedes Benz zote za wabunge na mawaziri na kuzipeleka katika maendeleo ya nchi na kisha akafanya gari aina ya Renault 5 kuwa gari za serikali kwa viongozi wote, gari hiyo ilikuwa inatengenezwa nchini mwake kipindi hiko na ndio gari rahisi zaidi.

[emoji117]Alipunguza mishahara ya viongozi wote wa juu ukiwemo wa kwake na kisha akaondoa madereva binafsi wa viongozi wa juu na kuwaondolea mawaziri tiketi za ndege za daraja la kwanza na kuwataka kusafiri kwa ndege za kawaida tu.

[emoji117]Alikwapua ardhi kutoka kwa mabeberu na watu waliohodhi maeneo makubwa na kuyagawa kwa wakulima.
Zao la ngano liliimarika sana nchini mwake, kutoka kilo 1700 kwa heka moja hadi kilo 3400 kwa heka moja. Burkina Faso ikawa inajitosheleza kwa chakula.

[emoji117]Alikataa kabisa misaada kutoka nje, ikisema kuwa, “Anayekulisha basi atakuendesha tu”

[emoji117]Aliweza kuzungumza hadharani bila kificho hasa kwenye mikutano ya kimataifa kama mkutano wa umoja wa nchi za Afrika akisema kuwa Mabeberu wanapenyeza wizi wako kupitia biashara na maswala ya fedha barani Afrika.

[emoji117]Alikuwa kinara wa kuyataka mataifa ya Afrika kugoma kabisa kulipa madeni ya nje hasa ulaya akidai kuwa Afrika mataifa masikini hayastahili kulipa madeni ya matajiri hasa walionyonya utajiri huo kutoka Afrika.

[emoji117]Thomas Sankara alichukua ghala la jeshi la kuligeuza kuwa soko la kisasa (Super Market) kwa ajili ya kila mtu ndio super market yaa kwanza kabisa nchini Burkina Faso.

[emoji117]Wale viongozi wenye mishahara mikubwa rais Thomas Sankara aliwataka watumie mshahara wao wa mwezi mmoja katika mwaka katika kusaidia jamii.

[emoji117]Alikataza kabisa matumizi ya viyoyozi katika ofisi za umma akisema kuwa ni anasa na hivyo ni lazima viongozi wafanye kazi kwa bidii kuwaletea maisha mazuri wanabukinabe kabla yao kwanza.

[emoji117]Thomas Sankara aliitoa Burkina Faso kushirikimashindano ya Olympic ya 1984 baada ya kuona UN imekaa kimya kabisa kuhusu vitendo vya ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini. Alifanya hivyo kuonesha kuchukizwa na vitendo vibaya dhidi ya watu weusi na pia kuonesha msimamo wake kama Rais.

[emoji117]Mnamo tarehe 15 october 1987 Thomas Sankar hadi anauwawa kwa kupigwa risasi mshahara wake ulikuwa ni dola 450 tu na alikuwa ana miliki gari moja Renault 5, Baiskeli 4, Gitaa 3, pamoja na jokofu, tena bovu[emoji124]

FB_IMG_1634245219802.jpg
 
Alikuwa mzalendo wa kweli na alihakikisha elimu inaimarishwa ambapo kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kiliongezeka kutoka asilimia 13 hadi 73! Aliboresha kilimo cha pamba ili nchi yake ijitosheleze kwa mavazi na kuuza ziada, na pia alipanda miti mingi sana kukabiliana na makali ya jangwa la Sahara.

Aidha, tukumbuke kuwa Thomas Sankara ndiye aliyebadili jina la nchi yake kutoka Upper Volta na kuitwa Burkina Faso hadi leo hii.

Jina hili humaanisha nchi ya watu wanyoofu (the land of upright people kwa tafsiri yangu rahisi na isiyo rasmi). Loh, naumia sana! Sijui kama atakuja kutokea mzalendo wa Afrika kama Sankara - Che Guevara wa Afrika.
 
Ogaaah! Alkuwa pia akihimiza watu wafanye KAZI, aliwapa wakulima pembejeo za kilimo pamj na mashamba na alkuwa anapita na baskeli yake kukagua mashamba ya kila kijiji KWA namna hyo watu wengi walipambana na umaskini KWA vitendo na sio kuandaa andaa seminar za uongo na kweli na kujidai unawaelimisha watu halafu unawaacha hawajui la kufanya, huyu Rais aliyepindulwa hivi karibu Bwana Alfa Kounde alkuwa mojawapo ya watu waliohusika kumuua na huyu jamaa wa kijesh aliyeshika nchi anaonesha dalili nzuri ya kuzaliwa upya KWA Thomas Sankara mwingine.
 
Ogaaah! Alkuwa pia akihimiza watu wafanye KAZI, aliwapa wakulima pembejeo za kilimo pamj na mashamba na alkuwa anapita na baskeli yake kukagua mashamba ya kila kijiji KWA namna hyo watu wengi walipambana na umaskini KWA vitendo na sio kuandaa andaa seminar za uongo na kweli na kujidai unawaelimisha watu halafu unawaacha hawajui la kufanya.
 
Ogaaah! Alkuwa pia akihimiza watu wafanye KAZI, aliwapa wakulima pembejeo za kilimo pamj na mashamba na alkuwa anapita na baskeli yake kukagua mashamba ya kila kijiji KWA namna hyo watu wengi walipambana na umaskini KWA vitendo na sio kuandaa andaa seminar za uongo na kweli na kujidai unawaelimisha watu halafu unawaacha hawajui la kufanya.
 
Alikuwa mzalendo wa kweli na alihakikisha elimu inaimarishwa ambapo kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kiliongezeka kutoka asilimia 13 hadi 73! Aliboresha kilimo cha pamba ili nchi yake ijitosheleze kwa mavazi na kuuza ziada, na pia alipanda miti mingi sana kukabiliana na makali ya jangwa la Sahara.

Aidha, tukumbuke kuwa Thomas Sankara ndiye aliyebadili jina la nchi yake kutoka Upper Volta na kuitwa Burkina Faso hadi leo hii.

Jina hili humaanisha nchi ya watu wanyoofu (the land of upright people kwa tafsiri yangu rahisi na isiyo rasmi). Loh, naumia sana! Sijui kama atakuja kutokea mzalendo wa Afrika kama Sankara - Che Guevara wa Afrika.
Ogaaah! Alkuwa pia akihimiza watu wafanye KAZI, aliwapa wakulima pembejeo za kilimo pamj na mashamba na alkuwa anapita na baskeli yake kukagua mashamba ya kila kijiji KWA namna hyo watu wengi walipambana na umaskini KWA vitendo na sio kuandaa andaa seminar za uongo na kweli na kujidai unawaelimisha watu halafu unawaacha hawajui la kufanya.
 
Alikuwa mzalendo wa kweli na alihakikisha elimu inaimarishwa ambapo kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kiliongezeka kutoka asilimia 13 hadi 73! Aliboresha kilimo cha pamba ili nchi yake ijitosheleze kwa mavazi na kuuza ziada, na pia alipanda miti mingi sana kukabiliana na makali ya jangwa la Sahara.

Aidha, tukumbuke kuwa Thomas Sankara ndiye aliyebadili jina la nchi yake kutoka Upper Volta na kuitwa Burkina Faso hadi leo hii.

Jina hili humaanisha nchi ya watu wanyoofu (the land of upright people kwa tafsiri yangu rahisi na isiyo rasmi). Loh, naumia sana! Sijui kama atakuja kutokea mzalendo wa Afrika kama Sankara - Che Guevara wa Afrika.
[emoji24][emoji24][emoji24] Ni miongoni mwa Viongozi wakubwa sana Afrika, Pia walikuwa na maono ya yakututoa hapa tulipo na kutupeleka kwenye maendeleo na mafanikio makubwa san! R.I.P Capt. Sankara!

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom